Ufugaji wa Kuku wa Kisasa: Fahamu Mbinu, Faida, Changamoto na Masoko

Ufugaji wa Kuku wa Kisasa: Fahamu Mbinu, Faida, Changamoto na Masoko

ndugu naomba unitumie kitabu cha ufugaji kuku wa kienyej
 
Mkuu Zantsan naomba ufafanuzi kuhusu kuangulisha vifaranga kuku wa kienyeji marambili

Nimeambiwa eti unaweza kuwa labda na kuku wa 5 na wakataga kwa pamoja, utakuwa unawaondolea mayai kila yanapozidi matatu na hii itawafanya watage mayai mengi zaidi kuliko uwezo wao wa kuatamaia

Baada ya kuanza kuatamia utawarudishi maya let say 10 kwa kila kuku, na mengine utayabakisha
Baada kuku kumaliza kuatamia eti unawanyanganya vifaranga na kuwawekea mayai yalio salia na wataanza kuayaatamia tena kwa siku zingine 21 huku wewe ukiendelea kulea vifaranga katika boksi lao maalamu lenye joto la kutosha

Kuna ukweli wowote kuhusu hili mkuu?
 
Last edited by a moderator:
Hey JF Members.
Ee bwana kuna mtu anaweza kunipa msaada wa mchanganuo wa kufuga kuku. naona soko la kuku ni kubwa sana. hii ni biashara ambayo soko lake liko tayari. hotels, functions, vibanda vya chipss.... Yeyote mwenye idea naomba msaada please!!!!!
kaka tembelea website hii Home utajifunza mengi!!!
 
Mkuu Zantsan naomba ufafanuzi kuhusu kuangulisha vifaranga kuku wa kienyeji marambili Nimeambiwa eti unaweza kuwa labda na kuku wa 5 na wakataga kwa pamoja, utakuwa unawaondolea mayai kila yanapozidi matatu na hii itawafanya watage mayai mengi zaidi kuliko uwezo wao wa kuatamaia Baada ya kuanza kuatamia utawarudishi maya let say 10 kwa kila kuku, na mengine utayabakisha Baada kuku kumaliza kuatamia eti unawanyanganya vifaranga na kuwawekea mayai yalio salia na wataanza kuayaatamia tena kwa siku zingine 21 huku wewe ukiendelea kulea vifaranga katika boksi lao maalamu lenye joto la kutosha Kuna ukweli wowote kuhusu hili mkuu?
Mayu,

kuhusu kuwaondelea mayai ni kweli kunawafanya kuku wa kienyeji watage zaidi kuliko uwezo wao.

Baada ya kuku kumaliza kuatamia huwezi kuwarudishia mayai yale yaliyobaki kwani yatakuwa yamekwisha kuharibika. Hata kama ungewatafutia mayai mengine bado hao kuku wasingekuwa na uwezo wa kuatamia tena kwani kuku hawa wananakuwa wapo katika hali ya brooding kitu ambacho hawawezi tena kuatamia wala kutaga mpaka zipite angalau wiki mbili baada ya kuwanyang'anya vifaranga,wataanza tena kutaga na baadae wataweza tena kuatamia.

Pia nitumie fursa hii kuwaomba radhi wadau kwa kuwa wakati mwingine huwa nachelewa kujibu swali lililoulizwa kutokana na majukumu ya hapa na pale, hivyo kama mtu utakuwa na haraka sana unaweza ukanipigia kwenye simu yangu.
Asante
 
Wanajf, Kwasasa niko mkoani Dodoma,kwa wale wafugaji wa dodoma mnaweza kunitafuta kwa msaada zaidi. Tuko pamoja kwenye ujenzi wa Taifa na kijikwamua binafsi.Ujasiriamali unalipa.

Nipo dar natafuta vifaranga chotara wa kuchi na wale wa malawi, tafadhali msaada.
 
Nipo dar natafuta vifaranga chotara wa kuchi na wale wa malawi, tafadhali msaada.
Nimekutumia kwenye private yako namba zangu nipigie ili nikuelekeze kwa huko Dar wapi utapa vifaranga chotara,ingawa hawa vifaranga wa kuchi upatikanaji wake si rahisi sana kama ilivyo kwa kuku wa weusi wa malawi,wanaopatikana ni wale chotara waliokrosiwa kwa kutumia majogoo ya Rhode Island Red wale wekundu.
 
Ndugu wana jamii forum, sasa ni wakati wa kuacha kulalamika, tunapaswa kujituma na kupiga kazi kwa bidii. Vijana graduates kutoka vyuo mbalimbali tuwaze zaidi kwenye kujiajiri kuliko kuajiriwa, kujiajiri kunatoa uhuru wa kufanya kazi na kutoa maamuzi binafsi tena kwa wakati. Kuajiriwa kimsingi hakuna tofauti na utumwa na kama utapiga hesabu vizuri utagundua kuwa kuajiriwa ni hasara na pia huzuia mtu kuitumia elimu yake ipasavyo hasa ukiajiriwa serikalini. Kwa wastaafu pia wana fursa ya kutumia mafao yao vyema kwenye miradi ya ufugaji.

Kwa kuanzia tu naruhusu kuulizwa maswali kutoka kwa wale wote wanaojihusisha na ufugaji wa kuku, kama kuna jambo lolote linasumbua na kutaka kupata ufafanuzi. Pia kwa wanaohitaji kuanzisha mradi wa ufugaji wa kuku,utotoreshaji wa vifaranga,biashara ya uchanganyaji na uuzaji wa vyakula vya kuku nk , kama watanzania tunaweza kusaidiana ili hatimae tuondokane na umasikini. Kila mtu awe msaada kwa watu wengine kwa fani aliyesomea.

Karibuni kwa mjadala.

Mkuu naomba mawasiliano yenu
 
Kwa wale wenye maeneo madogo ni vema kufuga kwa mtindo wa cage kama unavyoonekana kwenye picha.
 

Attachments

  • 1390931015793.jpg
    1390931015793.jpg
    57.1 KB · Views: 459
Mkuu, kuhusu chakula hesabu zako si sahihi sana, kifaranga hakili msosi sawa na kuku mkubwa, hebu cheki mchanganuo huu,

Hebu tuone hesabu hii:
Kuwanunua 2000 @2400 = 4,800,000/=

Chakula:

Mwezi wa kwanza (Wiki 0- 4) average kilo 75 kwa siku ( Mfuko mmoja na nusu hii ni Stater) @ 34,000 = 51,000 X 30 days =1,530,000/=
Mwezi wa pili ( Wiki ya 5 - 8) average kilo 100 kwa siku ( Mifuko miwili finisher) @ 34,000 = 2,040,000/=
Glower (wiki ya 9 - 11) siku 14, kila siku mifuko 3 @28,000 = 1,176,000/=
Glower (wiki ya 12 - 18) siku 42, kila siku mifuko 5 @28,000 = 5,880,000/=
Layers (wiki ya 19 -23) siku 28, kila siku mifuko 5 @32,000 = 4,480,000/=

------------------------
15,070,000
add Manunuzi 4,800,000

------------------------

19,870,000

-------------------------



Wiki ya 19 wataanza kutaga kidogo kidogo mpaka wiki ya 24 utaanza sales ya 50% ikiongezeka kadri siku zinavyosonga. Kwa hiyo mtu anayetaka kuanza ufugaji kwa kuku 2000 anahitaji mil 20,000,000/=. Ukiweka na gharama za banda na uendeshaji hadi waanze kutaga ni lazima uwe na 27m- 30million.

shughuli pevu hii, nashauri anayeanza, ni vyema basi aanze na kuku 500 then aongeze taratibu taratibu huku akijifunza challenges.

Well said mkuu! Tusitake kutembea wakati ndo tumezaliwa, mwisho wa siku utarudi kukaa, utasimama dede then utatembea.

Kuanza biashara hii kwa kuku 2000 au 5000 utakufa kwa pressure unaweza ukauguwa kichaa mambo kama hayakuenda vizuri kwa cost analysis za mdau hapo juu. tukubali kuanzia chini ili tupande adoado huku tukijifunza, mafunza hasa ya jukwaani tukaya practice kwa vitendo.

Biashara hii ni nzuri pamoja japo risks zake ni nyingi lakini ni vizuri, tuanzia padogo faida tupate kidogo na hata hasara kidogo huku tukiendelea kujifunza changamoto mbalimbali.
 
Habari wana Jf,
Kuanzia kesho Ijumaa hadi Jumapili panapomajaliwa nitakuwa DSM kwa shughuli za kutoa ushauri kwa wafugaji, kwa yeyote atakae nihitaji basi tuwasiliane ndani ya siku hizo ili tuweze kusaidiana.
 
Naombeni msaada wa kujua gharama za chakula , madawa kwa kuku wa mayai 200 toka vifarnga hadi kutaga na wastani wa trei
 
Naombeni msaada wa kujua gharama za chakula , madawa kwa kuku wa mayai 200 toka vifarnga hadi kutaga na wastani wa trei
Ungesema kwanza upo wapi..kwa kuwa gharama hutofautina toka eneo moja mpaka jingine....
Pia gharama za chakuka kama umefuatilia thread hii kwa makini bila shaka mtaalam wetu Zantsan alishaweka mchanganuo wa Chakula kwa kuku wa Mayai,nyama pamoja na Chanjo/Dawa na ratiba za kuwapa.....
Jaribu kusoma Post zote kwa makini then kama unaona kuna sehemu hujaelewa rudi Usaidiwe....
Hii itasaidia kutorudia rudia Ya nyuma...
 
Back
Top Bottom