Ufugaji wa Mbuzi, Kanga, Bata Mzinga na Kuku

Galla huyu kanunuliwa sh laki5
naomba kutoa mrejesho wa hawa mbuzi baadaya kufika waliopo. nilipata baraka ya kufika kwa kaka aisee sikuamini nilicho kiona wana JF KUNA WATU WANA MBUZI. Hilo galla ni bonge moja la mbuzi tofauti na picha hzi hapo kwenye picha huwezi gundua ukubwa wake ni tofauti na uhalisia (uhalisia ni likubwa sana nahisi yupo kwenye 120 kg), na kuna aina nyingine nyingine za mbuzi ambazo ata kuziona sijawahi. nilijifunza baadhi ya aina ya mbuzi namna ya ufugaji wake, chakula, banda, alama ambavyo kwangu imekua funzo na kupata namna ya kuboresha na mimi shamba langu. Kwa moyo ya dhati nasema asante sana kaka kwa fursa hiyo na uzidi kubalikiwa
 
Hongera Sana mkuu Kwa kujifunza Mambo mapya
 
Karibu sana kaka hili ni letu sote hata maandiko matakatifu yanatuasa tupendane, ukikwama popote kaka tutafutane kikubwa sote tufikie malengo na baraka za Mungu ziwe juu ya wafugaji wote, tugawane tone la upendo kwetu sote ili tufikie malengo.
 
naunga mkono hii hoja maana inawezekana sehemu moja kukawa na urahisi wa bei, maarifa au upatikanaji mkubwa wa vitu aidha dawa/ chanjo au vifaa vinginevyo vya mifugo
Naomba niwaambie kitu kimoja tushirikishane juu ya upatikanaji wa dawa/chanjo za mifugo yetu na vifaa mbali mbali vinavyohitajika kwa mfugo wetu ili kama inatakiwa kusaidiana jinsi ya kuvipata iwe rahisi naomba kuwakilisha.
 
Naomba niwaambie kitu kimoja tushirikishane juu ya upatikanaji wa dawa/chanjo za mifugo yetu na vifaa mbali mbali vinavyohitajika kwa mfugo wetu ili kama inatakiwa kusaidiana jinsi ya kuvipata iwe rahisi naomba kuwakilisha.
hakika tukishilikiana kwa pamoja lazima mambo yaende vizuri hata Mungu anaachia baraka zake
 
This is a real deal mwanangu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…