Ufugaji wa Mbuzi, Kanga, Bata Mzinga na Kuku

Umeandika Kama unakimbizwa mkuu ...
Hujasema Ni mbuzi wangapi...
Breed gani?
Changamoto?
Faida ?
Masoko?

Kaa kwa kutulia au ulitaka Tuu tuone unae mbuzi ,kanga na kuku?

Kunywa maji andaa Uzi uliojitosheleza.
Nadhani boss hiyo ndio knowledge gap. Ungekuja kwa mfumo wa maswali tu sio kumshambulia nadhani atatuongezea mengi.🙏
 
Gepard ,

..Galla wanastahimili magonjwa na ukame hivyo ni rahisi kuwafuga.

..wanakua haraka na kutoa maziwa mengi kuliko mbuzi wa asili / east african small goats.

..bei yao siyo kubwa ukilinganisha na mbuzi wa kisasa kama Boer, Alpine, Saanen nk.

..wanapatikana Tanzania maeneo ya Longido, au nchi jirani ya Kenya.
 
Ndugu yangu JOKA asante kwa ufafanuzi. Ubarikiwe. Ila kwa uzoefu wako kibiashara ni bora mtu afuge mbuzi wa kisasa au kienyeji mfano hao galla?. Ukinipa sababu ntakubariki zaidi🙏
 
Ndugu yangu JOKA asante kwa ufafanuzi. Ubarikiwe. Ila kwa uzoefu wako kibiashara ni bora mtu afuge mbuzi wa kisasa au kienyeji mfano hao galla?. Ukinipa sababu ntakubariki zaidi🙏

..nina kaka yangu yuko kijijini anafuga mbuzi wa kienyeji, kwa hiyo bado sijaingia rasmi ktk ufugaji.

..ninafanya jitihada kumshawishi aboreshe mbuzi wake kwa kuingiza mabeberu wa galla.

..ushauri wangu ni utafute mabeberu wa galla uwapandishe kwa mbuzi jike wa kienyeji.

..ukiwa na mbuzi wa kutosha unaweza kuboresha stock yako mpaka ukawa na mbuzi galla pure.

cc wakaliwetu, Manchid
 
Ndo nimeanza wadau nimechukua jike huyo na watoto wake mapacha wote nao ni majikeView attachment 1835211
Hongera sana Mungu akusimamie ktk ufugaji wako, nakuomba tu kila unapo kwama usisite kuuliza itakusaidia kufikia malengo yako ktk ufugaji, maana hata sisi tulikubali kufundishika ndio tukafikia hapa tulipo. Una fugia wapi ndugu yetu?
 
Hongera sana Mungu akusimamie ktk ufugaji wako, nakuomba tu kila unapo kwama usisite kuuliza itakusaidia kufikia malengo yako ktk ufugaji, maana hata sisi tulikubali kufundishika ndio tukafikia hapa tulipo. Una fugia wapi ndugu yetu?
Nipo mkoa wa mara wilaya ya Serengeti hapa mkuu,nimefika huku naona wenyeji wanafuga nimeshawishika sana
 
mkuu kweli nilikua huko napiga kaz hao mbuz wanapatikana sana na niwakubwa. nilionyeshwa mbuz ambae bado mdogo ananyonya nilishangaa jinsi alivyo na umbile kubwa. ila bei nayo imechangamka sana hapo longido
 
Thanks for your info..lkn sijaelewa Hilo jiwe la kulamba liko je na linacontain nn labda
 
mk mkuu unachosema ni kweli, hizo picha alozoweka mkuu wakaliwetu nikama hazielezei ukubwa halisi ya hayo mambuzi. nimekaanayo longido kwa siku 50 kwa kweli ni wakubwa na wanapatikana sana tu lakini bei sasa utadhani unanunua ndama - ng'ombe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…