Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ni hawa njiwa wa kawaida?Hawa ndege ni urembo yani wanapendezesha nyumbani [emoji3589]View attachment 1792078
Nadhani boss hiyo ndio knowledge gap. Ungekuja kwa mfumo wa maswali tu sio kumshambulia nadhani atatuongezea mengi.🙏Umeandika Kama unakimbizwa mkuu ...
Hujasema Ni mbuzi wangapi...
Breed gani?
Changamoto?
Faida ?
Masoko?
Kaa kwa kutulia au ulitaka Tuu tuone unae mbuzi ,kanga na kuku?
Kunywa maji andaa Uzi uliojitosheleza.
Samahani boss, ukishamtambua inakuwaje? Em tuchambulie ubora wa huyu mbuzi kwa kufuga ili kutengeneza kipato...jinsi ya kumtambua mbuzi wa aina ya galla.
Samahani boss, ukishamtambua inakuwaje? Em tuchambulie ubora wa huyu mbuzi kwa kufuga ili kutengeneza kipato.
Ndugu yangu JOKA asante kwa ufafanuzi. Ubarikiwe. Ila kwa uzoefu wako kibiashara ni bora mtu afuge mbuzi wa kisasa au kienyeji mfano hao galla?. Ukinipa sababu ntakubariki zaidi🙏NGepard ,
..Galla wanastahimili magonjwa na ukame hivyo ni rahisi kuwafuga.
..wanakua haraka na kutoa maziwa mengi kuliko mbuzi wa asili / east african small goats.
..bei yao siyo kubwa ukilinganisha na mbuzi wa kisasa kama Boer, Alpine, Saanen nk.
..wanapatikana Tanzania maeneo ya Longido, au nchi jirani ya Kenya.
Ndugu yangu JOKA asante kwa ufafanuzi. Ubarikiwe. Ila kwa uzoefu wako kibiashara ni bora mtu afuge mbuzi wa kisasa au kienyeji mfano hao galla?. Ukinipa sababu ntakubariki zaidi🙏
Hongera sana Mungu akusimamie ktk ufugaji wako, nakuomba tu kila unapo kwama usisite kuuliza itakusaidia kufikia malengo yako ktk ufugaji, maana hata sisi tulikubali kufundishika ndio tukafikia hapa tulipo. Una fugia wapi ndugu yetu?Ndo nimeanza wadau nimechukua jike huyo na watoto wake mapacha wote nao ni majikeView attachment 1835211
HongeraKaribu Mzee japo kanga ni mayai ikiwa utahitaji kutotolesha yanapatikana.
Nipo mkoa wa mara wilaya ya Serengeti hapa mkuu,nimefika huku naona wenyeji wanafuga nimeshawishika sanaHongera sana Mungu akusimamie ktk ufugaji wako, nakuomba tu kila unapo kwama usisite kuuliza itakusaidia kufikia malengo yako ktk ufugaji, maana hata sisi tulikubali kufundishika ndio tukafikia hapa tulipo. Una fugia wapi ndugu yetu?
hongera mkuu. unafugia mkoa gani?Hapa wanagonga pumba kidogo
..mchangiaji mwenzetu anaitwa wakaliwetu alisema kuna wafugaji wakubwa wa Mbogo Farms wanasaidia Watanzania ktk kuagiza mbuzi wa Boer kutokea South Afrika. Mbuzi wa Boer, Savanna, na Kalahari, asili yao ni South Afrika.
..nilipowacheki jamaa wa Mbogo Farms nimekuta wana namba 784 785 785, wameitoa kwa watu wenye interest za kununua mitamba ya ng'ombe kutoka katika mashamba yao. Nakushauri ujaribu kuwatafuta ktk namba hiyo labda watakuwa na majibu kuhusu suala lako la mbuzi breed ya Boer.
..Ukishindwa kuagiza Boer, kuna mbuzi mwingine hapa Tanzania na Kenya wa breed ya Galla/Isiollo. Ni mbuzi mzuri, anastahimili magonjwa, anakua haraka, majike wanatoa maziwa mengi,na madume wako active kwelikweli ktk kuwapanda mbuzi jike. Mbuzi wa Galla/Isiollo kwa hapa Tanzania anapatikana zaidi ktk jamii za Wamasai maeneo ya Longido.
..Mbuzi wa Galla huyu hapa:
Thanks for your info..lkn sijaelewa Hilo jiwe la kulamba liko je na linacontain nn labdaUzi wako umekaa vyema sana nakupongeza sana kwa hatua uliyo ifikia, nakushauri tu unapochukuwa Mbuzi mnadani uwapatie huduma za afya kwanza kabla ya kuwachanganya na hao wengine hasa unapokuwa na Mbuzi wachanga.
usiwe mbali na kijana wa kazi hasa hichi kipindi ambacho wana zaa, pili usiruhusu hao watoto kwenda machungani na mama zao mpaka wamalize wiki 4.
Mama anae nyonyesha mpatie pumba na mchanganyiko wa mashudu ya alizeti au pamba, chumvi,chokaa na kuwawekea jiwe la kulamba maana lina madini ya kutosha, na uwapatie dawa za minyoo kwa muda muafaka.
mkuu unachosema ni kweli, hizo picha alozoweka mkuu wakaliwetu nikama hazielezei ukubwa halisi ya hayo mambuzi. nimekaanayo longido kwa siku 50 kwa kweli ni wakubwa na wanapatikana sana tu lakini bei sasa utadhani unanunua ndama - ng'ombenaomba kutoa mrejesho wa hawa mbuzi baadaya kufika waliopo. nilipata baraka ya kufika kwa kaka aisee sikuamini nilicho kiona wana JF KUNA WATU WANA MBUZI. Hilo galla ni bonge moja la mbuzi tofauti na picha hzi hapo kwenye picha huwezi gundua ukubwa wake ni tofauti na uhalisia (uhalisia ni likubwa sana nahisi yupo kwenye 120 kg), na kuna aina nyingine nyingine za mbuzi ambazo ata kuziona sijawahi. nilijifunza baadhi ya aina ya mbuzi namna ya ufugaji wake, chakula, banda, alama ambavyo kwangu imekua funzo na kupata namna ya kuboresha na mimi shamba langu. Kwa moyo ya dhati nasema asante sana kaka kwa fursa hiyo na uzidi kubalikiwa
Aiseee hii kitu ni nomaa,,mungu anijaalie nipate ardhi yangu nifungue mradiGalla huyu kanunuliwa sh laki5