Ufugaji wa Mbuzi, Kanga, Bata Mzinga na Kuku

Ufugaji wa Mbuzi, Kanga, Bata Mzinga na Kuku

Wazo zuri Sana mkuu tupo pamoja ktk hili
Naomba niwaambie kitu kimoja tushirikishane juu ya upatikanaji wa dawa/chanjo za mifugo yetu na vifaa mbali mbali vinavyohitajika kwa mfugo wetu ili kama inatakiwa kusaidiana jinsi ya kuvipata iwe rahisi naomba kuwakilisha.
 
Habari za asubuhi ndugu zangu leo naomba niwashirikishe jambo kidogo. Hizi ni sehemu za mbuzi wetu kucheza na kupumzika hapo pindi warudipo toka kwenye malisho au watoto wakibakia nyumbani pindi mama zao wakienda malishoni. Karibuni sana.

20210331_065516.jpg

20210331_065519.jpg
 
Habari zenu wafugaji wenzangu nina changamoto kwa mbuzi wangu huyu kapata uvimbe mkubwa sehemu ya juu ya paja na ni mwezi mmoja na nusu baada ya mimba yake kutoka. naomba saada wa kiushauri namna ya kukabiliana na changamoto hii

photo_2021-03-31_13-17-01.jpg

photo_2021-03-31_13-17-12.jpg

photo_2021-03-31_13-17-17.jpg

photo_2021-03-31_13-17-18.jpg
 
Umeandika Kama unakimbizwa mkuu ...
Hujasema Ni mbuzi wangapi...
Breed gani?
Changamoto?
Faida ?
Masoko?

Kaa kwa kutulia au ulitaka Tuu tuone unae mbuzi ,kanga na kuku?

Kunywa maji andaa Uzi uliojitosheleza.
Wabongo bwana!
 
Changamoto sijakutana nazo bado kutokana na maeneo niliopo, soko la Mbuzi ni la uhakika kila mtu analifahamu, breed nmesema ni kienyeji pure,faida nmeizungumzia ya uzalianaji wa haraka maana bado sijaanza kuuza, nawewe kaa chini Kwa kutulia usome Kwa makini usikurupuke
Jibu mujaarabu
 
Habari zenu wafugaji wenzangu nina changamoto kwa mbuzi wangu huyu kapata uvimbe mkubwa sehemu ya juu ya paja na ni mwezi mmoja na nusu baada ya mimba yake kutoka. naomba saada wa kiushauri namna ya kukabiliana na changamoto hii

View attachment 1739401

View attachment 1739402

View attachment 1739403

View attachment 1739404
Kaka pole na hiyo changamoto, kwanza naomba nikuulize alipotoka mimba uliita vet aje kumchoma sindano ya kuzuia maambukizi? Antibiotic.
Kuhusu huo uvimbe usihofu hilo ni tezi nalo ukimwita vet atamshughulikia huwa yanawaletea homa, mpatie matibabu stahiki mara moja ili ustawi wa mwili wake uwe sawa.
 
Ukitaka kupata Mbegu iliyo bora sio cross inabidi kuwatafuta huko, na itakuwa vyema ukipata kwa wafugaji kuliko kuwafwatilia mnadani
Tofauti ya mbuzi wa kienyeji pure na hao cross inaleta madhara gani mkuu? Nisaidie, asante
 
Niseme kitu kimoja jamani tuliopo kwenye ajira tuanze sasa kutayarisha mashamba yetu kwa anae weza mifugo na kilimo na aliyepo na nafasi ayaendeleze pale alipo fikia kuna maisha ya baadae yanayo tuhitaji hasa sisi waajiriwa baada ya ajira.
Hapa nakuelewa sana mkuu, wewe umepevuka hasa.
 
Niseme kitu kimoja jamani tuliopo kwenye ajira tuanze sasa kutayarisha mashamba yetu kwa anae weza mifugo na kilimo na aliyepo na nafasi ayaendeleze pale alipo fikia kuna maisha ya baadae yanayo tuhitaji hasa sisi waajiriwa baada ya ajira.
Samahani mkuu unao uzoefu wa kufuga na ng'ombe wa maziwa? Asante
 
Kaka pole na hiyo changamoto, kwanza naomba nikuulize alipotoka mimba uliita vet aje kumchoma sindano ya kuzuia maambukizi? Antibiotic.
Kuhusu huo uvimbe usihofu hilo ni tezi nalo ukimwita vet atamshughulikia huwa yanawaletea homa, mpatie matibabu stahiki mara moja ili ustawi wa mwili wake uwe sawa.
Ki ukweli sijawahi kuita vet na huwa wakipata changamoto kuna daktari wa mifugo alikua ananielekeza dawa sahivi hayupo na nahisi madaktari wengi wa mifungo hawajui kuusiana na mbuzi ukilinganisha na ng'ombe, kuku na nguruwe.
 
Tofauti ya mbuzi wa kienyeji pure na hao cross inaleta madhara gani mkuu? Nisaidie, asante

..nadhani mchangiaji alikuwa anamaanisha kuwa ni muhimu kupata mbegu ambayo ni PURE.

..yaani kama ni kienyeji awe ni pure kienyeji. Na kama ni kisasa awe pure kisasa.

..sasa ukishapata mbegu zako ambazo ni pure, ndipo unaposhauriwa kuanza ku-cross kuelekea kwenye malengo yako.

..kama unataka cross ya mbuzi galla na mbuzi gogo white, ni vizuri ukawa na pure galla na pure gogo white.

..Ukiwa huna uhakika na purity ya mbuzi unaowa-cross maana yake hata MATOKEO yako yatakuwa sio ya uhakika.

NB:

..Tofauti ya mbuzi kienyeji vs cross.

..Kienyeji hawakui haraka, lakini wanavumilia magonjwa, na ni rahisi kuwatunza.

..Cross [ kienyeji + mbegu ya nje] wanakua haraka, wana gharama kuwatunza, wako wanaovumilia magonjwa, na wapo wasiovumilia.

..Mbegu za nje ni aghali, wanakua haraka, gharama kuwatunza, wakati mwingine wanachangamoto ya kuugua.

..Wanaofanya CROSS wanatarajia watapata mbuzi wenye SIFA NZURI za mbuzi wa asili na mbegu za nje.
 
Ki ukweli sijawahi kuita vet na huwa wakipata changamoto kuna daktari wa mifugo alikua ananielekeza dawa sahivi hayupo na nahisi madaktari wengi wa mifungo hawajui kuusiana na mbuzi ukilinganisha na ng'ombe, kuku na nguruwe.
Kaka nenda pale ubungo OIL COM Petrol station kwa madunga huwa wana ma vet pale watakusaidia ushauri mzuri please.
 
Back
Top Bottom