Ufugaji wa mbuzi wa nyama kibiashara unalipa?

Changamoto katika ufugaji wa mbuzi ni hii

Mbuzi wa kisasa ni rahisi kuwafuga hata kwenye eneo dogo na wanakua haraka sana ukizingatia kanuni zake
Changamoto ni soko, watu wengi hawapendi mbuzi wa kisasa

Mbuzi wa kienyeji wana soko kubwa sana
Changamoto yao ni kwamba wanakua taratibu sana, wanahitaji eneo kubwa la malisho na hawafanyi vizuri ukiwafungia eneo dogo,
Ni wasumbufu sana
 
Eka 20 ni nyingi sana Kwa mbuzi 200, ila hakikisha una kisima/maji ya kumwagilia majani ya kuwalisha
 
Eka 20 ni nyingi sana Kwa mbuzi 200, ila hakikisha una kisima/maji ya kumwagilia majani ya kuwalisha
Kweli kuna video ya jamaa wa Uganda anafuga wa kisasa, kwenye heka moja ana mbuzi 50, amepanda majani, ipo you tube nashindwa kuweka link yake hapa, kwa heka 20 hizo nyingi sana hata mbuzi 1000 anaweka kwa ufugaji wa kisasa.. kupanda majani,kisima cha maji na kulisha kwa vizimba
 
Weka ata jina la video tuka angalie
 
Kwanini kondoo mkuu? Fafanua na soko
1. Kondoo ana soko kubwa kuliko mbuzi, nyama ya kondoo haileti gauti
2. Kondoo ni watulivu kuliko mbuzi
3.Ulaji wa kondoo unahimilika
4. Kondoo anazaliana kwa kasi ana uwezo wa kuzaa mara 3 kwa mwaka

Kondoo ni mfugo wa nyama ya binadamu, mbuzi ni mfugo kwa ajili ya maziwa na nyama za mifugo wakali walao nyama.
 
Aisee nimepata kitu kipya! Maana na deal na mbuzi, sikuwa najua kuhusu kondoo kuzaa mara 3 ni bingo hapo mzee. Kuna mfugaji hapa jirani inabidi nikamtembelee anafuga kondoo tu, sikuwa najua hii siri
 
Ktk ufugaji tunapashwa kutafuta Mbegu zilizo bora, majike walio bora na maumbo makubwa ili waweze kukuletea uzao ulio bora ndani ya miezi 6 aweze kutoa aidha kama mbegu au wa supu.
 
Samahani naomba ufafanuzi hapo kwenye Kondoo kuzaa mara 3 kwa mwaka, ninavyo fahamu kondoo ukuwaji wake ndio wakasi tofauti na Mbuzi.
 
Kikubwa nacho shauri usinunue Mbugu kuanzisha ufugaji kabla huja tembelea wafugaji wenzako ili uweze kujua mahitaji, matunzo ,usimamizi,matibabu na jinsi ya kuchagua mbegu zilizo bora ktk ufugaji. Nasisitiza sana tembelea wafugaji waliopo karibu yako na kama ofisi za Taliri uko nazo karibu pitia huko huwa wana toa elimu nzuri sana ktk ufugaji.
 
Hii ni Isiolo/Galla kwaajili ya kuzalisha, hii sasa inabidi umtafutie majike walio wa kubwa kwaajili ya kuweza kukuletea mazao yaloyo bora shambani kwako
 

Attachments

  • 20240926_063100.jpg
    1.3 MB · Views: 29
Aisee nimepata kitu kipya! Maana na deal na mbuzi, sikuwa najua kuhusu kondoo kuzaa mara 3 ni bingo hapo mzee. Kuna mfugaji hapa jirani inabidi nikamtembelee anafuga kondoo tu, sikuwa najua hii siri
Jaribu kufuatilia utakuja kusema mwenyewe hapa Mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…