Ufugaji wa Nguruwe: Fahamu faida, hasara na mbinu bora za ufugaji

Kuna mbegu ya nguruwe warefu hawana mafuta mengi, wanazaa watoto wengi. Inapatikana wapi na kwa bei gani?
 
Wadau kuna threads nyingi humu kuhusu nguruwe zenye information za kutosha kujibu maswali ya kawaida.Pia internet imejaa mambo tele.Ukitaka kupata uhalisi tembelea wafugaji wanaofuga kibiashara.
 
Huu mradi huwa nafarijika sana nikisoma mada za humu ndani, Mimi ni mfugaji maarufu wa hawa viumbe(Avatar yangu inathibitisha) Tatizo langu kubwa ni namna ya kupunguza gharama za chakula kwani hivi viumbe vinakula sana. Na tatizo la pili ni vitoto kufa hasa wakiwa na miezi minne hadi tano.
 
Mkubwa naweza pata number yako ya simu na ww uko wapi maana mimi nataka kufuga kwa wingi
 
Naomba number yako ya kwangu ni 0767164257
Naweza pata number yako na unafugia wapi ya kwangu ni 0767164257, kwani nataka kuaanza kufuga maeneo ya Tanga nina ekari kama 50 hivi
 
Habari wapendwa

Samahan naomba kujua ufugaji wa nguruwe, malazi yao na matibabu yao.

Pia na ufugaji wa kuku wa kienyeji yaani jinsi ya kumnyang`anya vifaranga,na je nifanye hivo vikiwa vina umri gani?

Naitwa Moi Mwakye kutoka Mbeya.
 
nguruwe anachukua miezi mingapi toka kuzaliwa mpaka kufaa kuliwa au kufaa kuchinjwa nyama ?
Hakuna Nguruwe anaechinjwa.
Wakitaka kuua wanapiga Nyundo kichwani. Anamwaga uharo biashara imekwisha.
 
Nguruwe ni Chanzo cha SARATANI (CANCER) YA TUMBO.

Mtamaliza wananchi kwa hawa wanyama nyie watu.
 
..ufugaji wa nguruwe unalipa sana.
mimi nimeanza na watoto kumi mwaka huu,nimeiga huu ujasiriamali,mzee alikuwa anafuga tokea enzi ya ujana wake,katusomesha wote mpaka vyuo vikuu kwa huu ujasiriamali,asante sana mtoa uzi nazidi kujifunza mengi kwa huu uzi,ubarikiwe sana.
 
Hongera sana mkuu, sasa hakikisha kuwa haufugi kama alivyokuwa akifuga mzee wako. Wewe fuga kisasa mpaka mzee wako ajisikie raha kukupeleka shule. Unaweza kufunga drinkers za kisasa ili kurahisisha ufugaji wako wa nguruwe na kuwafanya wawe na afya bora, tunapatikana Dar lakini kama upo mkoani tutakuagizia kwa gharama zetu. Piga simu namba: 0625504952

KARIBU SASA NA UFURAHIE UFUGAJI WA KISASA
 
Habari wapendwa

Samahan naomba kujua ufugaji wa nguruwe, malazi yao na matibabu yao.

Pia na ufugaji wa kuku wa kienyeji yaani jinsi ya kumnyang`anya vifaranga,na je nifanye hivo vikiwa vina umri gani?

Naitwa Moi Mwakye kutoka Mbeya.


Utangulizi
Utunzaji wa nguruwe mara nyingi hutegemea aina ya nguruwe, njia na aina ya ufugaji. Kwa mfano nguruwe jike anayefugwa kwa ajili ya kuzaa anahitaji kutunzwa tofauti na wale wanaonenepeshwa kwa ajili ya nyama. Kadhalika nguruwe wanaweza kufugwa ndani ya banda au nje, kutegemea na ukubwa wa shamba, fedha zilizopo kwa shughuli za ufugaji na aina ya nguruwe.

Utunzaji wa Nguruwe Dume
Achaguliwe dume mwenye sifa bora ikiwa ni pamoja na kutokuwa na kilema au ugonjwa wowote. Dume aliyechaguliwa, atenganishwe na majike ili kuepusha kupanda wakati usiotakiwa. Inabidi nguruwe huyu asinenepeshwe, kwa hiyo alishwe chakula bora kiasi cha kilo mbili hadi tatu kwa siku. Vile vile apewe maji kila siku.

Kama anapanda chini ya mara tatu kwa wiki, alishwe kilo mbili na nusu na kama anapanda zaidi ya mara tatu, alishwe kilo tatu kwa siku. Ikiwa dume ni dhaifu, aongezewe nusu kilo ya chakula na kama amenenepa sana apunguziwe nusu kilo ya chakula kwa siku. Ni muhimu awe na eneo la mita mraba 9.3 ilikuwezakupata mazoezi ya mwili. Ikiwa sehemu ya kupanda imetenganishwa eneo livve la mita mraba saba.

Nguruwe dume anaweza kutumika kwa kupandajike akiwa na umri wa miezi minane hadi tisa. Kwa umri huu anaruhusiwa kupanda jike moja kwa juma. Afikiapo miezi 10 anaruhusiwa kupanda majike mawili hadi matatu kwa juma. Akiwa na umri wa mwaka mmoja au zaidi ana uwezo wa kupanda jike mmoja kila siku kwa majuma mawili hadi matatu, kisha apumzike kwa muda wa majuma mawili. Dume wakubwa wasitumike kupanda jike wadogo kwani wanaweza kuleta madhara kama vile kuwavunja mgongo.

Ni vizuri nguruwe dume mmoja apande jike 15 hadi 20 kwa mwaka. Dume akizeeka au kuwa na ubovu wa miguu, achinjwe mara moja. Ni muhimu dume aogeshwe kwa sabuni na dawa zinazoweza kuua wadudu na vijidudu vinavyoweza kusababisha magonjwa. Banda na vifaa vinavyotumika visafishwe kila siku.

Utunzaji Wa Nguruwe Jike
Ili mfugaji aweze kupata mazao mengi na bora hana budi kuchagua nguruwe jike mwenye sifa zinazotakiwa. Nguruwe huyu ni vizuri awe amezaliwa na mama anayezaa watoto wengi, mwenye kutoa maziwa mengi na mtunzaji mzuri wa watoto. Tabia hizi zinarithiwa hata navizazi vingine vijavyo. Vile vile awe na afyanzuri na chuchu nyingi zisizopungua 12.

Nguruwe jike anaweza kuzaa akiwa na umri wa miezi mitano hadi sita. Ili kumzuia asibebe mimba mapema, ni vizuri atenganishwe na dume afikiapo umri huo.

Afikiapo miezi nane hadi tisa au akiwa na uzito wa kilo 130 ahaweza kupandishwa. Kabla ya kupandishwa nguruwejike apewe kilo 2.5 hadi tatu za chakula kwa siku. Nguruwe asipelekwe kwa dume mpaka atakapoonyesha dalili zajoto.
Maelezo zaidi unaweza pata kupitia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…