Ufugaji wa Nguruwe: Fahamu faida, hasara na mbinu bora za ufugaji

Nenda Vikindu kupita geti la maliasili toka hapo ni kama km 1 mkono wa kulia kuna Jamaa wanao wengi sana.
 
Mwenye uzoefu wa kufuga nguruwe tunaomba changamoto zakee maana nimejitosaa kufuga hawa jamaa
 
Nawakubali sana hao wadudu..... Tulikua tunafuga kwetu

Kikubwa ni chakula, pumba na mara nyingi ujitahidi kupita kwenye mabaa kukusanya maganda ya viazi, unayachemsha na chumvi, wanayakubali sana na yanawastawisha ile mbaya


Kingine ni usafi kwenye mabanda yao daily!
 
Thread nzuri,ila tupo kwenye mfungo.
 
Mkuu mm nataka kuanza kufaga ni 4,000,000/= natak nianze na 40 nipo moshi ila nitafugia kibosho je garam zao zitazd huo mtaji niliona mpk kufikia hatua ya kuwauza.
 
Mkuu mm nataka kuanza kufaga ni 4,000,000/= natak nianze na 40 nipo moshi ila nitafugia kibosho je garam zao zitazd huo mtaji niliona mpk kufikia hatua ya kuwauza.

Kama utawalisha inavyotakiwa,hiyo ni pesa ya kutunza nguruwe 20 kwa muda wa mwaka mmoja na nusu toka wazaliwe na wao kuanza kuzaa
 
Ivi ufugaji wa nguruwe na ng'ombe upi wenye faida nzuri. Msaada apo ktk ufugaji
 
Ivi ufugaji wa nguruwe na ng'ombe upi wenye faida nzuri. Msaada apo ktk ufugaji
Ng'ombe anaweza kuwa analipa kwenye maziwa,kwa vile utamkamua muda mrefu na faida nyingine ni kukuletea ndama,lakini kasoro yake hadi kufikia hatua hizo inachukua muda mrefu sana.
Nguruwe unamfuga muda mfupi nikiwa na maana ndani ya miezi sita unaweza muuza au kumzalisha.Na watakulipa zaidi kama utawafuga na kuwauza kwa wingi,kama tunavyofanya kwenye Kuku wa kisasa.Na ukiweza kuwa na Shamba lako ambalo utaweza kuwalimia nafaka,maboga au matikiti,itakulipa zaidi.Na ikatokea ukawa na mashine yako ya kukoboa nafaka kama mahindi,maana yake utakuwa unapata pumba kirahisi na bado kwenye mashine ukafungua mradi mwingine wa kuuza unga.Nahitimisha kwa kusema nguruwe ni zaidi ya mifugo yote.Huo ni mtazamo wangu
 
Mkuu nimependa sana hilo banda, ila niulize huwa hakifanyiwi usafi kwa kuosha na maji sababu umesema hapo kati zinawekwa pumba au nyasi...
 


kaka mm sina mtaji mkubwa nilitaka kufuga nguruwe na kuku.

vipi uko maeneo ya morogoro naweza pata maeneo kwa bei nafuu hasa rafiki kwa ufugaji huo nilioutaja na ambapo naweza pata mashamba ya kukodi kwa ajili ya kuwalimia chakula. ili kunipunguzie gharama.

je naweza pata shingapi kwa heka.
 
Kama utawalisha inavyotakiwa,hiyo ni pesa ya kutunza nguruwe 20 kwa muda wa mwaka mmoja na nusu toka wazaliwe na wao kuanza kuzaa
Nguruwe wangu mdogo miguu ya mbele haina nguvu hawezi kusimama atakua amepata ugonjwa gani au shida nini mkuu..
 
Mkuu huo ni ukosefu wa madini chuma. Changanya chakula chao na pig mix, inapatikana maduka ya mifugo, kipakti 4500,muangalie kama wiki akiendelea nunua sindano ya Iron mchome,kama ni mdogo mls 1.5,mkubwa 3mls
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…