SoC04 Ufugaji wa samaki kwa mapinduzi ya kitaaluma na kiteknolojia katika shule za serikali nchini Tanzania

SoC04 Ufugaji wa samaki kwa mapinduzi ya kitaaluma na kiteknolojia katika shule za serikali nchini Tanzania

Tanzania Tuitakayo competition threads

Gentlemen_

JF-Expert Member
Joined
Nov 24, 2019
Posts
4,431
Reaction score
13,876
Adobe Stock.jpg

Chanzo: Adobe Stock
UTANGULIZI:

Maono yangu ni kuiona Tanzania katika nyanja ya elimu inapiga hatua kwa kutumia njia mbalimbali ikiwemo ufugaji. Napendekeza serikali ifatilie na kuchambua mawazo haya kwa mustakabali bora wa elimu yetu hapa nchini.

DHIMA KUU YA MRADI HUU:

Ufugaji wa samaki aina ya Sato katika shule za serikali nchini Tanzania ambapo ufugaji huo utaleta maendeleo kwa shule hizo, wanafunzi, waalimu wao pamoja na jamii kwa ujumla. Itapunguza gharama kwa serikali kwa 50% katika uendeshaji wa shule zitakazokuwa katika mradi huo, zitaongeza ufanisi kwa asilimia 70% ya uendeshaji wa shule hizo (shule zitatumia mapato ya ndani), mradi utawainua waalimu kwa asilimia 40% kiuchumi, mradi utaleta mapinduzi ya kiteknolojia kwa asilimia 80%, mradi utapunguza tatizo la ajira na utegemezi kwa asilimia 30%.
UFUGAJI WA SAMAKI AINA YA SATO (TILAPIA)

phys.org.jpg

Chanzo: Phys.org
SATO ama kwa jina lingine Tilapia ni aina gani ya samaki?..

ni swali jepesi sana ila linahitaji mpangilio maalumu kumwelewa samaki huyu kama ifuatavyo:-

Anatoka katika kabila la Tilapiine ambako kuna takribani aina 100 tofauti tofauti.
Aina.JPG

Sato hana mazoea kabisa ya kuishi katika mazingira ya baridi iliyopita kiasi,kwa kumuweka katika mazingira haya basi unahatarisha maisha yake kwa asilimia kubwa.

Sato akipewa matunzo vizuri anafikia urefu wa futi 2.0 au zaidi ya hapo kulingana na aina ya Sato na mazingira aliyotunzwa sambamba na chakula na ulinzi wa kutosha.

Sato anajulikana au anasifika kuwa na sifa inayotajwa kitaalamu kama Mouth brooding Specie ikiwa na maana kwamba, samaki huyu anatabia ya kubeba mayai yaliyorutubishwa au vifaranga kinywani mwake kwa muda wa siku kadhaa.

Ufugaji wa Samaki huyu unategemea pia na malengo ya mfugaji ni somo au maelezo marefu sana hasa katika mtindo bora wa uchaguzi wa ufugaji, ningependa kugusia aina moja ya kufuga kwa kuchagua jinsia.

Hapa mfugaji anaweza kuchagua jinsia ya madume tupu katika ufugaji wake ilia pate faida kwa haraka, kumpunguzia gharama za ufugaji na mambo mengine mengi ikiwemo pia kama mfugaji ana eneo dogo atachagua mtindo huu wa ufugaji. maelezo na uchambuzi juu ya mtindo ni marefu ya kitaalamu zaidi tusonge mbele.

pinterest.jpg

Chanzo: Pinterest
FAIDA ZA KUFUGA SAMAKI HAWA

1. Kujipatia fedha na kunyanyua kipato kwa kundi fulani au mtu mmoja mmoja:

Hapa Tanzania kwa wastani bei ya kilo moja ya Sato ni 10,000 hivyo ukiwa na kilo 100 una uhakika wa kuingiza milioni moja, jambo ambalo kwa wafugaji wa Sato ni kawaida sana kuvuna zaidi ya kg 100 na kuendelea kulingana na ukubwa wa bwawa na wingi wa samaki pamoja na lishe ya samaki hao.

2. Kitoweo kizuri na chenye virutubisho vingi.
Sato ana virutubisho vya kutosha ikiwemo wingi wa Vitamin B12, Protini za kutosha bila kusahau OMEGA – 3 na madini mengine mengi mno.

3. Kupunguza uhaba wa kitoweo katika jamii.
Ndio, ufugaji wa samaki hawa husaidia kujaza nafasi iliyoachwa wazi kwa kutegemea samaki wa kutoka ziwani au baharini moja kwa moja. Uwepo wa samaki hawa katika masoko yetu husaidia kupunguza gharama za maisha kwani upatikanaji ni wa uhakika na ambao hauathiri mazingira / mazalia hasa yale ya asili.

4. Silaha ya kibaiolojia ya kupambana na magonjwa hasa Malaria.
Baada ya kufanya utafiti wangu nchini Kenya niligundua kuwa nchini humo pia wanawatumia samaki hawa kama njia moja wapo kupambana na ugonjwa wa Malaria. Kivipi?.. samaki hawa wanatumia kama chakula mazalia mbali mbali ya wadudu ndani ya maji na kwenye udongo mazalia hayo huwenda yakaonekana kwa macho au kwa kutumia vifaa maalumu (Darubini) hasa kwa viumbe vidogo mno microscopic organisms, inafahamika Mbu hutaga mayai ndani ya maji ili kuzalisha mbu wengine kwa wingi mayai haya (larvae) huliwa na samaki hawa hivyo kupunguza hatari ya kuzaliwa Mbu wengine wanao sababisha ugonjwa wa Malaria hasa Mbu wa kike (Anopheles).
Faida ni nyingi sana ningependa kuwasilisha hizo chache na kugusia katika changamoto chache za ufugaji wa samaki hawa kama ifuatavyo:-

Kabla ya yote ikumbukwe samaki huyu anahitaji vitu vitano muhimu katika maisha yake.

a - Maji safi na salama;

b - Hewa safi ya oksijeni;

c - Chakula Bora na si bora chakula;

d - Mwanga na hali joto nzuri;

e - Nafasi ya kutosha.

fao.org.gif

Chanzo: Fao.org
Iwapo kimoja wapo kikienda ndivyo sivyo basi matokeo hasi lazima yaje, hivyo changamoto za ufugaji wa samaki hawa zinategemea mambo hayo niliyoyataja hapo juu, bila kusahau magonjwa hasa ugonjwa wa streptococcosis ambao kwa utafiti wa marekani umesababisha hasara zaidi ya dola bilioni 1 kwa mwaka.


WALENGWA WA MRADI HUU:
Walengwa wa mradi huu ni shule za serikali pekee ambazo zitakidhi vigezo vya awali, vigezo vya msingi ni ardhi ya kutosha na uwepo wa chanzo cha maji cha uhakika.

Mradi utatekelezwa kwa (PHASE) na kwa kanda mbalimbali kwa kuchagua shule baadhi za kuanza nazo mradi huu. Mafanikio ya shule A ndio mtaji kwa shule B. Mafanikio ya shule B ndio mtaji kwa shule C. hivyo ni mzunguko wa kuambukizana mitaji, ujuzi na mambo mengine mengi chanya ili kuinua shule zote za serikali nchini Tanzania kiuchumi na kijamii kwa ujumla.

TAKWIMU:

Idadi ya shule za serikali kwa ngazi ya Sekondari na Msingi kwa 11-Mei-2024
IDADI YA SHULE.JPG

Chanzo: Tovuti kuu ya Serikali

MIUNDOMBINU NA CHANGAMOTO ZA SHULE HIZI (picha):

mwangaza.jpg

Chanzo:
Tovuti ya Mwangaza
itv.jpg

Chanzo: ITV

moshi municipal.jpg

Chanzo: Manispaa ya Moshi

haki elimu.jpg

Chanzo: Haki Elimu


UFANYAJIKAZI (IMPLEMENTATION)

1. Uchambuzi wa Shule
Kamati maalumu itafanya uchambuzi wa shule kwa kuzingatia kanda na kupendekeza shule hizo ziwe za kwanza kufaidika na mradi huu kwa awamu ya kwanza (PHASE 1). Uchambuzi huo utajumuisha jopo la wataalamu mbalimbali.

2. Uchambuzi wa Kuandaa Mradi
Baada ya shule hizo kupendekezwa, hatua inayofuata ni kuchambua mradi utafanyaje kazi katika shule hizo, kuna (MANUAL) nimeandaa ambayo inaelezea hesabu, takwimu na muongozo wa hatua kwa hatua wa utekelezaji wa mradi pamoja na kuongoza mradi ili kuleta matokeo chanya.

3. Kufanya Utekelezaji
Nitaelezea kwa ufupi, Mradi wa msingi ni ufugaji wa samaki ambapo kwa kukadiria katika shule moja kutapandikizwa samaki zaidi ya eflu kumi (10,000) ambapo vifaranga hivyo vitafugwa kwa muda wa miaka miwili mpaka mitatu. Kwa makadirio ya awali ndani ya miaka hiyo mitatu mradi wa shule hiyo utakuwa na jumla ya samaki 50,000 kwa wastani na makadirio ya awali ambapo kizazi cha kwanza cha samaki hao kitakuwa tayari kwa mavuno yenye faida.

Kwa makadirio ya awali samaki 5000 wana uwezo wa kutoa tani 2.5 na zaidi, kwa hesabu yakinifu ni kwamba tani 2.5 ina faida ya shilingi za kitanzania milioni 25. (kwa mahesabu madogo ya awali) hivyo tunaona kwamba kwa faida ndogo/makadirio madogo shule itaweza ingiza milioni 25 huku mtaji wake ukiwa mkubwa kwa zaidi ya mara 5 huku ikifanya uvunaji endelevu kwa kuzingatia vizazi vya samaki hao (generation).

4. Matumizi Baada ya Kupatikana Faida
Matumizi ya awali ni kuimarisha shule hapa ndipo tunaingia (PHASE 2), faida itatumika kuimarisha miundombinu ya shule husika hasa katika nyanja ya teknolojia. Ikumbukwe katika mradi huu shabaha ya pili ni kukuza teknolojia katika elimu yetu hapa nchini. Shule nyingi hazina vitendea kazi vya kisasa mfano projector, computer/laptop, tablets na vingine vingi.
Fedha zitaelekezwa katika ujenzi wa maabara ya kompyuta (computer lab) na kuhakikisha wanafunzi na waalimu wananufaika na vifaa hivyo. Kamati maalumu itakuwa inafanya ziara za mara kwa mara kuhakikisha ubora wa matumizi ya vifaa hivyo pia kutoa msaada wa kiutaalamu na semina pamoja na programu mbalimbali za kukuza vipaji hasa katika nyanja ya usanifu wa kimtandao na uundaji wa program endeshi (Programming) hasa akili bandia (Artificial intelligence), usalama wa kimtandao (Cyber Security) na zaidi.

Shiksha Valley School.jpg

Chanzo: Shiksha Valley School
Baada ya kukamilika kwa (PHASE 2), faida inayozidi kwa kitaalamu kama (surplus) itatumika kama allowance kwa waalimu katika muda wa ziada wa kufundisha, itatumika kununua chakula hapo shuleni, itatumika kama motisha kwa wanafunzi watakaofanya vizuri katika masomo yao (Mitihani ya kitaifa) na mambo mengine mengi pindi itapoonekana kuna tija.

5. Kutumia Faida kutoka Shule A kuwa Mtaji kwa Shule B
Hapa inaingia (PHASE 3), ambapo faida inayopatikana kuna asilimia inatengwa ili kukuza mtaji ambao utanufaisha shule jirani. Serikali baada ya kutoa mtaji kwa shule A na huo mtaji kutoa matokeo chanya basi shule A haina budi kusaidia kutoa mtaji kwa shule B. ambapo itatoa mtaji wa kuanzia, pamoja na utaalamu wa kiufugaji wa samaki hao hivyo kama kuna changamoto za awali katika shule A basi katika shule B kutakuwa na ufumbuzi wa kukwepa changamoto hizo, hivyp mradi utazidi kukua na kushika kasi katika kanda husika, na utaratibu utakuwa endelevu.

MATOKEO CHANYA / NINI TUNATEGEMEA?

1. Shule za serikali kujiendesha kwa mapato ya ndani kwa asilimia kadhaa;

2. Afya bora kwa wanafunzi: mfano samaki aina ya sato ana virutubisho vingi, hivyo wanafunzi watakaopata mlo wenye mchananyiko wa samaki hawa basi utasaidia kusukuma uwezo wao wa akili kwa asilimia kubwa maana inatambulika kuwa kirutubisho kama vile OMEGA -3 ni kizuri sana katika sekta ya akili;

3. Elimu ya ufugaji wa samaki kwa wanafunzi;

4. Elimu itakua kwa kasi hasa sekta ya teknolojia;

5. Utunzaji wa mazingira ulio bora;

6. Kusaidia serikali katika gharama za uendeshaji wa shule hizi;

7. Kuinua kipato kwa waalimu na kuongeza morali na kuwajengea ujuzi zaidi wa ufugaji na teknolojia kwa ujumla;

8. Kuinua shule zingine.

NAWASILISHA
 
Upvote 19
Atleast walimu nao waanze kupata ela za mboga na kutoa vumbi
Ni kweli....

Waalimu watapata Posho/Allowance ya kutosha..

Watapata posho ya kitoweo kwa kila mavuno...

Pia watapata SEMINA, VIKAO, WARSHA za kutosha..

Pia katika Manual yangu inaelezea kuwajengea uwezo waalimu (baadhi yao) waende kusoma nje hasa mambo ya Tehama ili waulete huo ujuzi kwa watoto wetu hapa nchini..

Tukirejea mitaala mipya ya Serikali inasisitiza sana Tehama mashuleni pamoja na stadi za kimaisha kwa ujumla..

Wacha tuone...
 
Hili wazo ni zuri kbsa ufugaji wa samak na ungali wa muda mfupi basi na elimu ya ufugaji kilmo na ufundi inabid ianzie huko ngaz ya shule ya msing
Ni kweli..

Swala la UFUGAJI ni hao SATO.

Swala la Ufundi ni hiyo project ya maswala ya TEHAMA kwa kuwawekea mazingira bora watoto wetu na vifaa vya kisasa vya kujifunzia....

Hivyo, huu mradi unagonga pande zote za muhimu..

Ikiwa shabaha kuu ni KUJITEGEMEA na kuweka morali ya KUJIAJIRI.... kuwa wabunifu, kuwa washindani...
 
Mkuu mimi sijasoma bandiko nimepitia tu picha ila nimependa ulivyopangilia mawazo yako yaliyoambatana na picha
Na mimi kama mdau mkubwa wa samaki nimefurahi.
Karibu sana...

Pia kwa wale ambao ni watu binafsi naamini mmeokota mambo mawili matatu hasa hiyo section ya SAMAKI (PHASE 1).

Hapo unaweza pata ABC za ufugaji ingawa si kivile.. ila at least unapata mwanga wapi pa kuanzia... kama utataka kufuga binafsi.

Wanafaida sana endapo utafata MISINGI na KANUNI za kuwafuga.
 
Sawa. Najaribu kuelewa. SASA wanafunzi wadaslam wanaweza kufuga kweli??
Tukiangalia vizuri kuhusu uchambuzi wa huu mradi tunaweza kuona SHULE nyingi za DSM zitashindwa vigezo viwili vikuu.

1- Eneo
2-Maji

Ila kwa kutumia neno KANDA, DSM itakuwa ndani ya KANDA ya PWANI ambapo kuna shule nyingi zina maeneo na maji ya kutosha, mfano maeneo ya RUVU, KISARAWE, MLANDIZI , KIBAHA, BAGAMOYO kote huko kuna shule nyingi zina UHITAJI zaidi na zenye vigezo..

Katika PHASE 1 nimeelezea kuhusu JOPO la wataalam ambao watachambua ni SHULE zipi zipewe kipaumbele.. ikumbukwe huu MRADI ni wa KISAYANSI ambao umefanyiwa utafiti hivyo hatujaribu ni kufanya kwa UHAKIKA....

Karibu kwa maswali na maoni zaidi Mkuu..🙏
 
Hadi wafundishwe, wasimamiwe
Walimu wao wenyewe hawajui hata kufuga
Upo sahihi Dada yangu ephen_

Katika MANUAL inaelezea kila kitu kuhusu kuwaingiza Waalimu katk mfumo huo (Culture Change transformation)..

Pia, MANUAL hiyo ina SECTION ya TRAINING PROGRAM (TP) kwa Waalimu ni nini wanapaswa kujua katika MATABAKA yote mawili.

1 _ UFUGAJI
2 _ TEKNOLOJIA

Karibu kwa hoja, mawazo, michango zaidi...
 
Na bet andiko hili lina zaidi ya maneno 1000
Yes ni kweli..

Kwa Uzito wa hoja za Bandiko hili si rahisi kuandika kwa maneno mia mbili watu wakaelewa.

Na hapo nimebana sana.. sana..

Ndio maana nikatengeneza MANUAL inayojitegemea kuhusu huu MRADI.
 
Wanachukua muda kuwa tayari kwa kuliwa?
Analiwa kuanzia miezi 6 na kuendelea..

Ila kwa TARGET tutakazojiwekea hatutavuna ndani ya kipindi hicho na kukigeuza kuwa ni kipindi cha KUZALIANA (Reproduction Period).

Ili kupata SUPER PROFIT ni miaka miwili mpaka mitatu.. then ikiisha hiyo miaka basi ni kuvuna kila baada ya miezi 6..
 
Analiwa kuanzia miezi 6 na kuendelea..

Ila kwa TARGET tutakazojiwekea hatutavuna ndani ya kipindi hicho na kukigeuza kuwa ni kipindi cha KUZALIANA (Reproduction Period).

Ili kupata SUPER PROFIT ni miaka miwili mpaka mitatu.. then ikiisha hiyo miaka basi ni kuvuna kila baada ya miezi 6..
Mambo mazuri kumbe aisee
 
Na bet andiko hili lina zaidi ya maneno 1000
Reference only.JPG


Reference pekee ya picha nilizoambatanisha inabeba jumla ya MANENO 31.

Ukiangalia kiuhalisia maneno mengi imebidi kuyawekea Mabano ya ziada ili kuelezea jambo kwa ufasaha zaidi (UFAFANUZI) maneno haya yametokea zaidi ya mara 40

Sijagusia herufi zilizosimama pekea ake zilizotumika ili kujenga taswira na mifano bora A, B, C herufi hizi zinatambulika kama neno linalojitosheleza..

hivyo kwa haraka haraka maneno 100+ hayajatumika directly bali kama emphasizing technique.

MWISHO: Lugha ya kiswahili ina uchache wa misamiati ambayo hupelekea kutumika kwa maneno mengi ili ujumbe ufike sawia... bila hivyo ile Tanzania tunayoitaka hatutaipata kwa bandiko la maneno mawili matatu..
 
Back
Top Bottom