Ufugaji wa Samaki: Pata ushauri, mawazo na michango kuhusu ufugaji samaki. Jifunze changamoto, utaalamu na masoko ya Samaki

Hahaaaaa. Tatizo lako nn? Acha ajibu hayo maswali ili sisi wakulima tunafaike na hiyo teknolojia. Nimeuliza hivyo ili teknolojia iwe wazi kwa wadau wote otherwise itakuwa uongo.

Kama ingekuwa tilapi na salmon wanajulikana tusingekuwa na uzi huu kuelimisha watu. Kama una hizo information toka fisheries ziweke hapa sio lazima kila mwana JF aende huko fisheries.
 
Aina za ufugaji
Zifuatazo ni aina/level za ufugaji ambazo mkulima anaweza kufanya kulingana na malengo na uwezo wake:

1. Huria (Extensive farming)
  • Idadi ya samaki wanaopandikizwa: samaki 2-3 kwa mita ya mraba
  • Samaki hutegemea chakula cha asili (mimea ya majini-phytoplankton, wadudu/viumbe vidogo vya majini-zooplankton)
  • Hauitaji ubadilishaji wa maji
  • Hauihitaji huduma ya ziada ya hewa
2. Kati ya huria na nusu shadidi (Modified extensive:
  • Samaki, 4-7 kwa mita ya mraba
  • Chakula cha asili na chakula cha ziada huitajika
  • Maji hubadilishwa sentimenta 10-20 kila baada ya 3-4weeks kulingana na hali ya samaki na maji yako
  • Huduma ya hewa ya ziada sio ya ulazima
3. Nusu shadidi (Semi-intensive)
  • Idadi ya samaki kwa mita ya mraba ni 10-25
  • Chakula cha asili na cha ziada
  • Huduma ya hewa ya ziada lazima
  • Maji hubadilishwa kila siku au kila baada ya siku kadhaa (15-25 cm)
4. Shadidi (Intensive)
  • Idadi ya samaki ni zaidi ya 25 kwa mita ya mraba
  • 100% chakula cha kutengenezwa
  • Maji ni kuingia na kutoka
  • Hewa ya ziada masaa yote
  • Eneo linalotumika ni dogo ukilinganisha na mifumo mingine
Miundombinu ya ufugaji
Samaki wanaweza kufugwa katika miundombinu mbalimbali kama ifuatayo

Bwawa
  • Kina 0.8-1.5m
  • Ukubwa 100 mita za mraba- 1ha
Matanki
  • Umbo-mstatili au mviringo nk
  • Kina 1-1.5m
  • Kipenyo kwa lile la mduara 3-10m
  • Ukubwa kwa la mstatili inategemea na uwezo lakini lisiwe kubwa ili kuhimili nguvu ya maji
Materials: Plastic, cement, chuma nk

NB: Simtank linafaa( Faida inapatikana kama utalitumia kwa intensive system)

Vizimba (Fish cages)
  • Huwekwa katika maji ya asili kama vile ziwani, baharini au katika bwawa. Vipo vinavyoundwa kwa local materials kama mianzi na vipo vya aluminium.
Eneo linalofaa kwa ufugaji
Baadhi ya maeneo yanayofaa ni yale mashamba ya mpunga, na maeneo yaliyo karibu na vyanzo vya maji. Zifuatazo ni sifa za maeneo yanayofaa:
  1. Udongo: Mfinyanzi husaidia kupunguza gharama za ujenzi wa bwawa na maji kwakuwa linaweza kutuamisha maji na kuruhusu maji yasipotee. Likiwa la kichanga bwawa ni lazima lijengewe au kuwekwa nylon sheet ili kuzuia upotevu wa maji. Unaweza ukahamisha udongo wa mfinyanzi kutoka sehemu moja hadi nyingine ili kuzuia upotevu wa maji (muone mtaalamu kwa ushauri zaidi juu ya mbinu ya kuhamisha udongo).
  2. Chanzo cha maji ya uhakikaEneo liwe na maji ya uhakika. Vyanzo vya maji ni kama vile mito, bahai, maziwa, chem chem., kisima, maji ya dawasco na mvua. Maji yasiwe na kemikali hatarishi kwa viumbe.
  3. Miundombinu ya barabara: Inasaidia kwa ajili ya usafirishaji wa bidhaa na samaki wakati wa kuvuna.
  4. Eneo lisiwe na historia ya mafuriko ili kuzuia athari za mafuriko kwa miundombinu yako. Utatumia gharama nyingi katika kuimarisha miundombinu yako.Jamii/aina ya samaki
  5. Eneo lenye mwinuko wa wastani husaidia katika ujenzi wa bwawa.
  6. Miundombinu ya umeme ni sifa ya ziada hususan kwa mkulima wa kati na wajuu kwa ajili ya kutumika katika kuendesha visambaza hewa.
  7. Ulinzi ni muhimu
Angalizo: Aina ya eneo lako ndilo linaweza kukufanya uchague muundombinu gani wa kufugia utumie

Aina ya samaki unaoweza kufuga Tanzania kwa sasa

Maji baridi
Sato/Perege, Kambale, Kambamiti wa maji baridi na Trout

maeneo ya baridi kama vile
  • Iringa
  • Kilimanjaro
  • Arusha
  • Mbeya
Maji bahari

Kambamiti wa maji bahari, mwatiko, chewa, kaa, chaza wa lulu

Upatikanaji wa Vifaranga vya samaki husika
Vyanzo vya vifaranga ni kutoka katika mito, bahari, maziwa na wale wa kuzalishwa katika vituo vya kuzalishia vifaranga.

Sato na Kambale. Kifaranga huuzwa Tsh. 50-100 kwa kifaranga.

Vituo vya serikali Utapata sato wa kike na kiume mixed sex).
  • Kingolwira - Morogoro
  • LuhiraSongea
  • Mbegani-Bagamoyo .
Vituo binafsi kama vile Faith aquaculture-Kibamba (DSM) (utapata monosex sato), PeramihoSongea (mixed sex). Monosex huuzwa kuanzia Tsh. 200 kwa kifaranga, na mixed ni100 kwa kifaranga.

Trout
Mayai huagizwa toka Marekani, Israel

Kambamiti wa baharini Alphakrust “Mafia.

Chakula cha samaki, uvunaji, ujenzi na gharama zake na mchanganuo mzima unaweza kuupata kupitia
Mengine yanayofanana waweza yapata kupitia
 
mmmmh,mimi pia nimesoma lyamungo advance.,mbona vile visamaki ni vidogo tena kwa ajili ya prac
 
Reactions: SDG
Habari Wakuu. .kwa wale wanaouza samaki sokoni reja reja au wanaohitaji samaki maotelini ntaanza kuuza samaki mwezi wa Tano kwa bei nafuu sana na kwa mda wowote ule ..samaki wenye afya wanafika kwako bado wazima kabisa wanafia kwako.. mume wangu na mabwawa wa samaki ila sijui mengi kuhusu ufugaji ningeshauri..namba Yangu ya simu 0652856708
 
ahsante. wanafikia uzito gani kwa mmoja?
 
Habari wadau. Naomba niongee kidogo kuhusu masoko ya samaki. Kwanza kuna masoko ya reja reja (tsh7000-9000) ambapo unawatangazia majirani zako kuja shambani kununua, unavua na kuhifadhi kwa barafu na kuwapelekea marafiki au office mate wako wakuchangie.

Unaweza kuwa na gari ile ndogo refrigerated na kusambaza sehemu mbalimbali za mji uliopo. mfano wazoeshe watu kuwa kila siku fulani unauzia mahala fulan, peleka feri soko la samaki, Pili, Uza kwa jumla katika viwanda vya samaki ( bei yao ni 5000-6000 kwa kilo)hawa hata ukiwa tani 1000 wanachukua kwa maramoja, uza ktk maduka ya jumla.

Tatu, uza kwa mama nitilie, hotelin. Nne, ongeza thamani samaki wako nfano tengeneza sausage za samaki, kausha kwa moshi nk.
 
kwa uchache nafikiri itasaidia kuhusu masoko. Mods tafadhali weka juu pale hiyo ya masoko
 
Nina maswali juu ya ufugaji wa samaki
1. Bwawa Kama hilo lililopamba huu Uzi unalisafisheje?
2. Je Bwawa la samaki linahitaji kusafishwa?
je nisafisheje bila kuharibu mazalia ya samaki?
3. Je ni lazima kutenganisha samaki watoto na wakubwa?
Bwawa standard linatakiwa kuwa na mlango wa kutolea maji ambao unaweza kuwa wa mbao, pvc pipe au zege.

Bwawa husafishwa kwa kubadilisha kiasi cha maji kama vile 10-15cm kwa siku/wiki/mwezi kulingana na uwingi wa samaki na upatikanaji wa maji.

Kuhusu samaki watoto na wakubwa:ukiwa na size tofauti ktk bwawa utasumbuka ktk kukadiria chakula, ukubwa na muda wa kuvuna tena kwa sato kama wanazaliana utasababisha samaki kuwa wengi kuliko uwezo wa bwawa hivyo kusababisha kudumaa.
 
Wapebdwa habari. Ni wapi ninaweza kupata liner za kuweka kwenye bwawa la samaki.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…