ni kweli angemPM lakini hata sisi tunahitaji kupata huo ujuzi kupitia kwenye hii sred. hivyo ni vema wakaendelea kuhojiana hapahapa ili tupateelimu nzuri. wakiingia kwenye issue za PM itakula kwetu.Malila nadhani ungem PM mkawasiliana na kumsaidia mkuu kwenye hio project yake. Najua wewe ni mtaalamu wa fani hiyo hivyo fanya kazi yako kwa kumsaidia vizuri na kumpa maelekezo yote juu ya ufugaji samaki wa aina mbali mbali na maeneo mbali mbali.
Wakuu natamani kufuga samaki lakini sijui wapi nitapata wajenzi wa bwawa, kuna mtu ana habari zozote kuhusu hili jambo??? msaada tafadhali
what is the comperative cost advantage?
hivi ukifuga samaki kwenye bwawa lako, je gharama za ufugaji mpaka kuuza zinaweza kuwa better than samaki wanaotoka kwnye maziwa kama victoria etc, bei zikoje, je ukiweza kufuga sato dar au karibu na dar unaweza kuuza kwa bei ya sato katika soko la kawaida na kupata faida? hivi samaki wa kufugwa mwenye wastani wa nusu kilo anaweza kutunzwa kwa muda gani mpaka kuwa tayari kuuzwa?
and what is yielding rate
is fish farming in Tz worth the value of investment and time?
just out of curiousity
someone should revert back to my queries please
Bwawa linahitaji inlet na outlet ili ufuge vizuri,lakini wakati mwingine static water ponds unaweza kutumia, hapa inabidi uangalie kama hilo bonde lako linaweza kukupa sifa hizo vinginevyo unaweza kupata shida kama ziwa likarudi na level ya maji ikazidi sana, samaki wote watasombwa, au ukitumia maji yaliyotuama kama ulivyosema, level ikipungua chini ya mita 1.2 samaki wanaweza wasifanye vizuri.
Hizi zote ni changamoto, lazima upambane nazo na uzishinde. Mimi nilianza pilot kwa kutumia static water, samaki wanakuwa vizuri, ila mimi maji yanatoka chini, kwa hiyo evaporation hainiathiri, kuna wakati dalili za kukosekana oxygen huwa naziona. Kama unaweza kupata mahali ambapo unaweza kuwa na mfereji wa kuingiza maji, ungefanikiwa sana.
ni kweli angemPM lakini hata sisi tunahitaji kupata huo ujuzi kupitia kwenye hii sred. hivyo ni vema wakaendelea kuhojiana hapahapa ili tupateelimu nzuri. wakiingia kwenye issue za PM itakula kwetu.
Niko hapa Mbezi kwa Msuguri DSM, nataka kuanza kufuga samaki, udongo ni wa mchanganyiko wa mfinyanzi na mchanga...naomba ushauri kama udongo huu utafaa kwenye kutengeneza bwawa na kama haufai mbadala wake ni nini, na ni aina gani ya samaki naweza kuwafuga kwa eneo hili?
How profitable is this business. Sijasikia yeyote akielezea. Baada ya miezi sita, samaki moja utamuuza kiasi gani.
Dah hiyo ya kenge imenishtua maana bwawa ninalotaka kufugia ni eneeo lenye kenge...dawa ya hawa kenge ni nini wakuu?
Dawa inayojulikana kule Uswahilini kwetu ni kuchemsha mayai mengi,halafu yachukue kayaweke pale kando ya bwawa lako. Kenge anakawaida ya kumeza yai na analivunjia shingoni kama halijachemshwa, sasa likichemshwa haliwezi kuvunjika,basi linamkaba na ndio kifo chake. Sasa kama ataweza kumeza, si ajabu akamaliza mayai yote na asife!!!!!!!!!!!!!