Ufugaji wa Samaki Wenye Tija: Fahamu Kuhusu Ufugaji wa Samaki Jinsia Moja

BwanaSamaki012

JF-Expert Member
Joined
Jan 13, 2023
Posts
212
Reaction score
250
Watu wengi wanatamani kufuga samaki lakini wanakosa taarifa sahihi juu ya namna bora ya kufuga samaki, moja kati ya vitu muhimu kwenye ufugaji wa samaki ni kuwa na mbegu bora ya samaki, nikisema mbegu bora ya samaki wa kufugwa nina maanisha samaki anayekuwa haraka ndani ya muda mfupi na mwenye uwezo wa kustahimili kuishi kwenye mazingira yasiokuwa ya asili.

Naomba nijikite zaidi kuelezea samaki aina ya sato, kuna aina nyingi sana za samaki aina ya sato (Tilapia species) lakini sio aina zote zinafaa kwa ufugaji

Hivyo ni muhimu kuhakikisha unapandikiza mbegu (vifaranga) bora kwa kununua mbegu kutoka kwa wazalishaji wanaotambulika na kuaminika badala ya kuchukua vifaranga kutoka kwenye vyanzo asili vya maji mfano ziwani, mabwani au mitoni ili kuepuka kuchukua mbegu isiyofaa kwa ufugaji wa kibiashara (samaki ambao kiasili hawakui sana kuwa na maumbo makubwa)

Vifaranga/Mbegu inayofaa ni ipi?

Katika ufugaji wa samaki aina ya sato (Tilapia species), species ambazo zinashauriwa na zimeonekana kuleta matokeo mazuri kwa wafugaji wengi ni hizi mbili, species ya kwanza kabisa ni Nile tilapia (Oreochromis niloticus) ikifatiwa na Wami/Mozambique tilapia.

Faida za kufuga samaki jinsia moja pekee (madume tu) ni zipi?

Katika ufugaji wa samaki kibiashara ni muhimu na vizuri zaidi ukifuga samaki madume pekee badala ya kufuga jinsia mchanganyiko madume na majike kwa sababu zifuatazo:

1. Ukuaji wa Haraka: Samaki madume hukua haraka zaidi kuliko majike. Kwa hivyo, ukifuga samaki madume pekee, watafika ukubwa unaohitajika kwa biashara mapema zaidi kuliko mchanganyiko wa madume na majike.

2. Kupunguza Uzalianaji: Samaki majike uzaliana kwa wingi sana jambo linalosababisha idadi ya samaki kuzidi uwezo wa bwawa (carrying capacity). Hii husababisha ukosefu wa oksijeni ya kutosha kwa samaki, hivyo kuathiri afya yao na ukuaji wao.

3. Uchafuzi wa Maji wa Mapema: Samaki wanapozaliana, idadi yao inakuwa kubwa, na kusababisha uchafuzi wa maji kwa haraka. Uchafuzi huu unatokana na kiwango kikubwa cha amonia inayozalishwa na kinyesi cha samaki, jambo linaloharibu ubora wa maji na hatimaye kuathiri ukuaji wa samaki.

Mbinu za Kuzalisha Samaki Madume Pekee ni zipi?

Baada ya kuona changamoto za kufuga samaki mchanganyingo kwa ufugaji wa samaki kibishara wataalamu walikuja na njia nne ili kuhakikisha uzalishaji na ufugaji wa samaki unafanikiwa, njia hizo ni kama zifuatazo:

1. Utenganishaji wa Kawaida (Manual sex separation): Hii ni mbinu ya kuchagua na kuwatenganisha samaki madume na majike kwa kwa kutumia mikono na kuwafuga katika sehemu tofauti tofauti mfano bwawa A majike pekee bwawa B madume pekee.

Mbinu hii ni ya kizamani na ningumu lakini pia ni rahisi kutokea makosa ya kibinadamu (human errors), pamoja na changamoto zake bado inatumiwa katika uzalishaji mdogo wa samaki.

2. Kubadilisha Jinsia (Sex Reversal): Mbinu hii inahusisha matumizi ya kemikali au hormone ili kubadilisha jinsia ya samaki na kuwa madume. Kwa mfano, matumizi ya 17-Alpha Methyltestosterone (MT) kwenye chakula cha mwanzo cha samaki (starter feed) ambacho upewa vifaranga kwa muda wa siku 21 - 28 za kwanza baada ya kifaranga kutotolewa.

Kwa lugha rahisi chakula hicho wanachopewa samaki kinakuwa na kiwango kikubwa cha hormone ya testosterone inayochochea mabadiliko ya samaki majike kuwa na madume. Mbinu hii ni maarufu katika ufugaji wa samaki kwa sababu ndio hutumiwa na wafugaji wengi, inauhakika kwa asilimia 90%+.

3. Mchanganyiko wa Spishi (Hybridization):
Kwenye njia hii mfugaji anacrossbreed two different tilapia species that have distinct sex-determining mechanisms. Baads ya kucrossbreed na samaji jike kutotoa mayai vifaranga vitakavyototolewa vyote uwa vya kiume; For example when you crossing Nile Tilapia (XX/XY system) with Blue Tilapia (ZZ/ZW system) kizazi mseto (hybrid) kwa kiasi kikubwa huwa madume pekee.

4. Mabadiliko ya Kijenetiki (Genetic Manipulation): Hii ni njia ya kitaalamu na yenye ufanisi zaidi inayoruhusu mabadiliko ya moja kwa moja ya vinasaba vya samaki ili kuhakikisha uzalishaji wa samaki madume pekee. Mfano mzuri ni matumizi YY male fish, YY male can only produce genetically male offspring when crossed with normal females.

Njia gani ni rahisi kutumia?

Kati ya njia zote tajwa hapo juu njia rahisi zaidi ni ambayo inaweza kutumiwa na mtu ambaye hana uelewa mpana juu ya ufugaji samaki ni manual sex separation na sex revesal method

Kwa kutumia moja kati ya mbinu hizi, wafugaji wa samaki wanaweza kuzaliza samaki wa jinsia moja madume pekee na kupunguza msongamano, kuhakikisha ukuaji wa haraka, na kuthibiti ubora bora wa maji, hatimaye kuleta faida na uendelevu katika sekta ya ufugaji wa samaki.

Ilikuwa na mradi endelevu ni vyema kuyatenga mabwawa yako kwa matumizi tofauti tofauti;
Bwawa A kwa ajili ya kuzalisha vifaranga, ambalo litakuwa na samaki mchanganyiko majike na madume na mabwawa.
Bwawa B kwa ajili ya kufugia samaki wa jinsia moja (madume pekee) ambalo hili ndio utakuwa ukiwauza kibiashara.

Kwa maelezo zaidi, ushauri au jambo lolote linaloruhusu ufugaji samaki unaweza nicheck directly
Call/WhatsApp: 0758779170


Unaweza kujiunga kwenye group letu upate dondoo za kila siku kuhusu ufugaji samaki
 


Mkuu toa mwongozo wa gharama.
1 gharama zaVibali vya kufugia kwenye vyanzo vya maji i.e ziwani
2 bei ya vifaranga
3 gharama za malisho
4 utunzaji na material . Pia project cost ina gharimu kiasi gani
 
Mkuu toa mwongozo wa gharama.
1 gharama zaVibali vya kufugia kwenye vyanzo vya maji i.e ziwani
2 bei ya vifaranga
3 gharama za malisho
4 utunzaji na material . Pia project cost ina gharimu kiasi gani
1. Gharama za vibali vya kufugia samaki ndani ya chazo cha maji (cage culture): Gharama ni kati ya milioni 10 hadi milioni 15 inategemea na ukubwa wa eneo unalohitaji na umbali uliopo toka ofisi za mamlaka husika na sehemu unayohitaji kuanzisha mradi wako,

Mchanganuo wa gharama pamoja na utaratibu wa kupata vibali vya kufanya shughuli za ufugaji samaki ndani ya ziwa Victoria:

I)Mhutasari wa kikao cha serikali ya kijiji au mtaa ambapo mradi utafanyika, utatakiwa kuitisha kikao na kuomba hidhini kwa wananchi wa eneo husika kutumia eneo lao kwa shughuli zako za ufugaji samaki (Gharama za kuitisha kikao sio constant ila andaa milioni 1).

II)TAFIRI (Tanzania Fisheries Research Institute) - Taasisi hii iliyopo chini ya wizara ya mifugo na uvuvi, inahusika kwenye hatua za mwanzo kabisa za kufanya survey kwenye eneo ambapo vizimba vitawekwa, kupima kina cha maji, ubora wa maji, mkondo wa maji, ukubwa mawimbi n.k. (Gharama ni Tsh. 3,000,000)

III)NEMC (National Environment Management Council) - Hii mamlaka itafanya tathimini za kimazingira (environmental impact assessment) Kisha utapewa report na utaratibu wa namna gani yankuendesha shughuli zako bila kusababisha matoa hasi kwenye mazingira ya asili. (Gharama yao n 5,000,000)

IV)Bonde la Ziwa Victoria - Hii mamlaka inatoa kibali cha matumizi ya maji (gharama ni chini ya milioni moja kwa mwaka)

V)Barua ya Afsa uvuvi wa eneo husika (Bure)

VI) Kibali kutoka Wizara ya mifugo na uvuvi idara ya ukuzaji viumbe hai majini.

Lakini pia sasa hivi kuna maeneo tengefu yaliyotengwa ndani ya ziwa Victoria kwa ajili ya shughuli za ufugaji samaki, yanakodishwa na halmashauri ili kuwapa unafuu wawekezaji wenye mitaji midogo.

Unachotakiwa kufanya ni kuandika barua kwa wilaya husika kupitia kwa mkurugezi wa wizara ya uvuvi, kuomba eneo la kukodi kwa ajili ya kuendesha shughuli zako za uvuvi ndani ya ziwa Victoria
 
Mkuu toa mwongozo wa gharama.
1 gharama zaVibali vya kufugia kwenye vyanzo vya maji i.e ziwani
2 bei ya vifaranga
3 gharama za malisho
4 utunzaji na material . Pia project cost ina gharimu kiasi gani
2. Bei za vifaranga inategemea na ukubwa wa kifaranga bei ni kati ya shilingi 200 hadi shilingi 300.

3. Gharama za wastani za chakula cha samaki kwa kilo moja ya chakula ni 3,500 Tsh. Hiki ni chakula kinachotoka nje ya nchi kwa wazalishaji wa ndani gharama zinakuwa nafuu zaidi

4. Project cost inategea unataka kuvuna tani ngapi kwa kila production cycle, mfano ujenzi wa cage moja yenye uwezo wa kuchukua samaki 12,000 inacost 3M.
 
Tunaotaka kufuga nyumbani bwawa dogo liwe na ukubwa gani!? Na gharama ni makadirio kiasi gAni
 
Tunaotaka kufuga nyumbani bwawa dogo liwe na ukubwa gani!? Na gharama ni makadirio kiasi gAni
Yapo mabwawa ya kuamishika (Mobile pond) yenye uwezo wa kuchukua samaki 500 - 2,000 ambayo yanafaa sana kwa mazingira mijini, unafuga samaki bila kuchimba bwawa na unaweza kutumia hata maji ya bomba

Makadilio ya manunuzi na Uendeshaji wa mradi (vifaranga, chakula na umeme) ni kati ya milioni 2 hadi milioni 5
 
Kumbe kuna kubadili jinsia ya Samaki?
Mhizi kemikali zikiingia kwa mwanadamu ndio zinasababisha shida kwa watoto wetu,hapo mnatenegeza mashoga transgenders
 
Kumbe kuna kubadili jinsia ya Samaki?
Mhizi kemikali zikiingia kwa mwanadamu ndio zinasababisha shida kwa watoto wetu,hapo mnatenegeza mashoga transgenders
Hapana sio kweli, Matumizi ya methyltestosterone kwa ajili ya kubadilisha jinsia ya samaki hazina athari kwa watumiaji wa mwisho kwa sababu hormone hii haibaki katika tishu za samaki baada ya kuchakatwa. By the time the fish reaches the consumer, the substance is either metabolized or removed completely.

Lakini pia homoni hii inatumika kwenye uzalishaji wa samaki madume udhibitiwa isiingie moja kwa moja kwenye mazingira ya asili ili kuepuka environmental pollution.

Tafiti zimethibitisha kuwa hakuna athari zozote za kiafya kwa mlaji na kwa mazingira
 
Mkuu tunaweza kupata connection ya hayo maeneo tengefu ya ziwa victoria ya ufugaji wa samaki kama hutajali unaweza kutueleza gharama za ukodishaji zikoje
 
Mkuu tunaweza kupata connection ya hayo maeneo tengefu ya ziwa victoria ya ufugaji wa samaki kama hutajali unaweza kutueleza gharama za ukodishaji zikoje
Ndio Mkuu inawezekana, gharama inategemea na idadi ya vizimba inavyotaka kuweka kwa wastani ni kuanzia 250,000.

Mimi nipo Mwanza sasa hivi naomba tuwasiliane nikupe muongozo.
 
Mkuu nahitaji hii, naweza kupata wapi
Dar es salaam Mkuu, pia naweza kukutengenezea sehemu yoyote ulipo kama uko nje ya Dar ili kuepuku usumbufu na gharama za usafirishaji

Niambie uko wapi na unahitaji la size gani?
 
Kwa wale wanaotaka kupunguza gharama za ujenzi wa mabwawa wanaweza tumia pond liner (nylon sheet) kutengeneza mabwawa ya aina hii
 

Attachments

  • 28896dc18fb0434086140a9bc213781c.mp4
    1.1 MB
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…