Ufugaji wa Samaki Wenye Tija: Fahamu Kuhusu Ufugaji wa Samaki Jinsia Moja

Samaki 12,000 gharama ya bwawa na nylon 0.75mm
Otherwise, kama eneo lako lina umeme nitabidi ununue machine ya kuongeza hewa kwenye maji (earator) then udouble idadi ya samaki uwepandikize wastani wa samaki 20 kwa mita ya mraba (20/m²) ili uwe na bwawa moja tu la 600m² (urefu 30m × upana 20m) badala ya mabwawa mawili

Hapa Utahitaji pond liner zenye ukubwa wa mita za mraba 704 (704m²) ambayo ni sawa na Tsh 5,280,000.

Hizi pond liner zinakatwa na kuunganishwa kiwandani kulingana na ukubwa wa bwawa lako, likikufikia unatandika kama shuka kucover bwawa lako ili kuzuia maji yasipotee
 

Mtalaam naomba umjibu huyu mtu.
 
Kwa wale wanaotaka kupunguza gharama za ujenzi wa mabwawa wanaweza tumia pond liner (nylon sheet) kutengeneza mabwawa ya aina hii
Hio pond liner ( nylon sheet) kuna kua na sehemu ya kuruhusu maji kutoka ( oulet) ikitokea maji yamechafuka?

Je maji utakayo yaingiza kwenye hio pond ndo mpaka kipindi utakacho vuna ndounayotoa?
 
Hio pond liner ( nylon sheet) kuna kua na sehemu ya kuruhusu maji kutoka ( oulet) ikitokea maji yamechafuka?

Je maji utakayo yaingiza kwenye hio pond ndo mpaka kipindi utakacho vuna ndounayotoa?
Ndio kunakuwa na outlet system zinazotoa maji kupitia PVC pipe

Hapana yanatakiwa kubadilishwa at least mara moja kwa mwezi
 

Mawazo 114 ya Biashara na Mitaji yake: Hatua kwa Hatua Jinsi ya Kuanzisha Biashara 114.
Whatsapp: 0687746471
 
Mtaalam,
Kuna mmoja alinieleza hivi kwa maeneo ya joto kama Dar Es Salaam samaki aina ya Tilapia(Sato) wanaweza kukua kwa miezi sita kufikia ukubwa wa kutosha tofauti na sehemu za joto pia kuna suala lingine pia alinieleza kuwa kufanya tathimini ni kama ifuatavyo kuwa samaki mchanga ananunuliwa kwa 3,00 na mpaka anafaa kuuzwa anakuwa amekula 1,500 na anakuwa na uzito wa gramu250 yaani kuipata kilo ni samaki wanne wenye wamegharamiwa kwa 9,400 na bei ya kilo ni 10,000 faida ni 6,00. Kuna ukweli wowote juu ya hilo? Na pia kama hakuna ukweli hesabu iliyopo ni ipi na hapo nimeweka nje gharama za uendeshaji na gharama za awali za uwekezaji kama kuchimba bwawa au kutengeneza bwawa.
 
Ni sahihi, samaki (Sato) wanakuwa vizuri zaidi kwenye maeneo ya joto kuliko kwenye maeneo ya baridi, mfano Njombe.

Bei ya kifaranga ni 300 hadi 200, kwa wastani inachukua miezi 6 kufikia mavuno ambapo kwenye kilo moja wanaingia idadi ya samaki samaki 4 hadi 3, wenye uzito wa 250g - 350g kwa samaki mmoja.

Kitaalamu ili kuzalisha kilo moja ya samaki samaki wako wanatakiwa wale kati ya 1.2kg - 1.5kg kwa kipindi chote cha ufugaji hadi kufikia mavuno, ukilisha chakula zaidi ya hapo uwezi kuona faida ya ufugaji samaki.

Gharama za kuzalisha kilo moja ya samaki ni kati wa Tsh 3,000 - 4,000. Hapa inategemea na ubora wa chakula na namna ya ulishaji.

Hapa ni muhimu kuzingatia kanuni za ulishaji kwa kulisha samaki wako kiwango sahihi cha chakula kulingana na uzito wao bila kuzidisha wala kupunguza, hakikishe kila chakula unachowapa samaki wanakula response ikionekana kuwa mbaya usilishe ili kuepusha upotevu wa chakula

Bei ya samaki kwa sasa ni Tsh 10,000 hadi 12,000 kulingana na ukubwa wa samaki wako wanapokuwa wakubwa zaidi ndio bei uongezeka.

Gharama za ujenzi wa bwawa inategemea na idadi ya samaki unaotaka kuvuna/kufuga, pia gharama inategemea ya mabwawa unayotaka kutumia mfano mabwawa ya kujengea, mabwawa ya kuamishika au mabwawa ya udogo.

Hii ndio itatoa picha kamili ya gharama za ujenzi na uendeshaji wa mradi wako
 
Kilo moja ya samaki, idadi ya samaki ni watatu na wastani wa uzito wa samaki ni 350g
 
Kilo moja ya samaki, idadi ya samaki ni watatu na wastani wa uzito wa samaki ni 350g
View attachment 3224994
Ok,
Kwa kiwango cha chini kwa kuzingatia maelekezo yako mtaalam ni kwamba
Bwawa lipo kwa mfano;-
Samaki mchanga 300×4
Chakula 1,000×4
Jumla 5,200
Gharama za uendeshaji 70%
Jumla Kuu 8,840 kwa kilo.
Mtaalam hivi ya Nylon ya 1mm ya samaki 5,00 au 1,000 movable inaweza cost kiasi gani?
 
Unanikumbusha mambo ya aquaculture systems.
Extensive, Semi-intensive and intensive culture.

Very Interesting
 
Ufugaji wa samaki 1,000
Utatakiwa kuwa na bwawa lenye ukubwa wa 100m². Nylon sheet yenye ukubwa wa 170m²
Bei ya nylon sheet 1m² ni Tsh 9,000
173m × 9,000= 1,557,000

Ufugaji wa samaki 500
Utatakiwa kuwa na bwawa lenye ukubwa wa 50m², nylon sheet itakayoitajika kucover bwawa lenye size hii ni 104m²
Bei ya nylon liner ni Tsh 9,000
104m² × 9,000m²= 936,000

60% ya Gharama za uendeshaji wa mradi wa samaki zinaenda kwenye chakula
 
Kwa maelezo haya, wewe ni mtaalamu, nimekukubali.

Nimeikopi namba yako kwa msaada zaidi.
 
nipe mwongozo kwa mfugaji anayetarajia kuanza kuchimba mabwawa yake binafsi shambani mwake. Pia unapatikana wapi?
 
nipe mwongozo kwa mfugaji anayetarajia kuanza kuchimba mabwawa yake binafsi shambani mwake. Pia unapatikana wapi?


Upatikanaji wa maji: Ni muhimu kuhakikisha kwenye eneo unalotaka kuchimba mabwawa kuna chanzo cha maji cha uhakika, chenye uwezo wa kusupply maji kipindi chote cha mwaka January - December

Mbegu bora/nzuri: sio kila samaki wanafaa kufugwa baadhi ya samaki (species) hazifai kufugwa kwa sababu wanachukua muda mrefu kukua hadi kufikia marketable size (250g). Muhimu kununua vifaranga/mbegu toka kwa mzalishaji anayeaminika badala ya kukusanya vifaranga toka ziwani au mtoni

Chakula: Lisha samaki wako chakula chenye ubora, chakula chenye virutubisho vyote muhimu (balance diet). Epuka kulisha samaki wako ugali au pumba pekee, wapo supplier wengi wanaouza chakula bora unaweza kununua toka kwao au ukatengeneza mwenyewe

Usimamizi: Ni muhimu kuwa na usimamizi mzuri kwa kuzingatia muda sahihi wa kulisha, kiwango sahihi cha chakula unachopaswa kulisha samaki, wakati sahihi wa kubadilisha maji n.k

Mimi kwa sasa nipo Moshi ila naweza fika sehemu yoyote kama utahitaji huduma yangu
 
Uzi mzuri sana...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…