Mama timmy labda tu nikueleze kwa ufupi
Kuhusu utunzaji wa watoto hiyo inategemea na aina ya Sungura.. sungura wa kienyeji (mara nyingi huwa wana mabaka) ni wavumilivu sana, huwa wanazaa watoto wengi na kuwatunza vizuri i.e anaweza asiue mtoto hata mmoja lakini hawa wakisasa kama wale weupe wenye macho mekundu (tuwaaita mchina) ni wasumbufu na wakizaa huwa hawawajali watoto wao .. anaweza kuzaa watoto 7 watano wakafa ndani ya wiki 1..
sungura anapenda sana kuishi sehemu isiyo na sakafu na yenye giza giza.. huwa wanachimba mashimo marefu sana na kuzaa humo humo.. watoto wakishaota manyoya anawatoa nje (njia hii ni hatari sana c'se wanaweza kuangusha nyumba)... kama una ardhi ndogo unawaweza kuwajengea mabanda ya mbao ya ghorofa yenye cuts nyingi halafu chini ukawekea udongo/maranda/pumba za mpunga iliwapate mazingira yao ya asili na joto vinginevyo wakizalia juu ya mbao au sakafu watoto ni lazima wafe
magonjwa: sijawahi kumuona sungura wangu aumwe lakini papasi huwa wanawapenda sana kwahiyo inakubidi uwe unapulizia dawa kwenye banda lao mara kwa mara au uwe unawapaka dawa ya unga (nzuri zaidi).. bila kusahau kuchoma moto yale madongo/pumba wanazolalilia baada ya wiki kadhaa