UTANGULIZI
Kabla hujaamua kufuga
sungura hakikisha ya
kwamba umejitoa na una
muda wa kuwahudumia
wanyama waha, ufugaji wao si rahisi kama vile ukifuga paka au mbwa, sungura Wanahitaji uangalizi na hasa kwenye usafi kwa sababu ni rahisi kwao kupata maradhi yatokanayo na mazingira
mabaya na machafu
AINA ZA SUNGURA
Kuna aina mbali mbali wa
sungura lakini
wanagawanywa mara mbili
kwa matumizi. Moja ni kwa
matumizi ya ngozi yake kwa
kutengeza kofia, mifuko, na mishipi na pili kuna aina ya
sungura ambao hufugwa kwa
kuzalisha nyama. Mfano wa
aina ya sungura wa ngozi ni
"Angora" ambaye manyoa
yake ni marefu. Na kwa sungura wanaofugwa kwa
nyama ni aina ya sungura
ambao hukua haraka, uzito wa
sungura wa nyama ni kutoka
kilo mbili hadi kilo tano. Bw.
Wachira anafuga sungura anina ya Califonia White na
Newzealand White, Chinchila
Flemish Giant ambaye ni
mkubwa, an pia hufuga
sungura aina ya Flemish
Fender
MABANDA
Kuna aina mbili za mabanda ya kufugia kwanza ni yale yakuwafungia ndani muda
wote bila kutoka nje na ya
pili ni ile ya pili ni nusu nusu
yaani wanakuwa na mabanda na wanaweza
kutoka nje kwenye ua
maalum, katika aina zote
mbili ni muhimu kuhakikisha
hakuna upenyo wa kuruhusu
panya kupita kwa sababu huwa wanakula watoto wa
sungura.
UFUGAJI WA NDANI
1 - Usitumie banda la kioo (aquarium) kwa sababu
halina hewa ya kutosha na ni vigumu kusafisha
2 - Sakafu ya nyavu za waya ni nzuri zaidi ila hakikisha
hakuna sehemu zenye ncha
kali inayoweza kuwaumiza
sungura, kwani wakumia ni
mpaka wapone wenyewe au
umchinje kwa sababu ukitumia dawa za antibiotic
sungura hana uwezo wa
kuzimeng'enya na kuisha
mwilini mwake, siku
ukimchinja atabakia na dawa na hata ukinusa nyama yake utahisi harufu ya dawa
3 - Ukubwa wa banda usipungue mita 4 * 2 kwa kila sungura mmoja, likiwa
kubwa zaidi ni vizuri
4 - Chini kuwekewe matandazio kama nyasi kavu au maranda ya mbao, lakini maranda yatokanbayo na miti yenye mafuta kama mi-pine na mikaratusi hayafai,
wawekee kipande cha blanket au taulokwa ajili ya kulalia na kujifungulia hasa kwa wazazi
5 - Ni muhimu kuwawekea sehemu ya kujificha mara
wanapohisi hatari, unaweza
kutumia mbao, box gumu au
plastiki
UFUGAJI WA NJE
1 - Sehemu yote izungushiwe wavu wa kuku kuzuia panya kuingia na wanyama wengine kama paka, mbwa, mwewe nk
2 - Upande mmoja uwe na mabanda, sehemu ya chakula na maji pamoja na kivuli kwa ajili ya sungura kupumzika
3 - Futi moja chini ya udongo kuwe na zege kuzuia sungura kuchimba na kwenda mbali
4 - Eneo la wazi liwe huru na hatari zote za sumu kama dawa za kuulia wadudu au mbolea, pia majani yaliyoota yasiwe ni yale yenye sumu
(waone wataalamu
wakushauri au ng'oa yote)
MAJI
Tumia mabakuli ya kigae,
plastiki au jengea kwa saruji, maji yabadilishwe kila siku na vyombo visafishwe kila siku
CHAKULA
Wapewe majani, mabaki ya
mboga za jikoni baada ya
kuchambuliwa, pia unaweza
kuwawekea pumba au chakula cha kuku (growers
mash) kwenye vyombo maalum kama chakula chenye virutubisho (concentrates)
USAFI
Kila siku jaribu kuondoa
uchafu kama vyakula vilivyo
mwagika, na kinyesi
kilichoganda kwenya
matandazio, fagia na kubadili matandazio angalau mara moja kwa wiki, manyoya ya
sungura mzazi yasiondolewe
hii huonyesha kwamba
anakaribia kujifungua watoto
MENO
Wakati mwingine meno ya
mbele hukua sana na
kumsababishia usumbufu
wakati wa kula, waone
wataalam ukiona ni marefu
zaidi na yanahitaji kupunguzwa, dalili kuu ni
sungura kushindwa kula kwa zaidi ya masaa 12
MIGUU
Miguu ya sungura si kama ya
wanyama wengine, nyayo
zake zimefunikwa kwa
manyoya, angalia ukiona
yananyonyoka kuna tatizo
chunguza, kucha zake nazi huhitaji kupunguzwa zikikua sana
UBEBAJI
Usimbebe kwa kutumia
masiki yake huwa wanaumia
sana, shika ngozi nyuma ya
shingo kama paka ukitaka
kumbeba
DAWA
Wapewe dawa ya minyoo
kama piperazine kila baada
ya miezi mitatu, dawa za
wadudu kama akheri
powdeer zinyunyuziwe
kwenya mabanda yao kuzuia viroboto, usiwape dawa nyingine bila ushauri wa kitaalamu, antibiotics ndio usijaribu kabisa kama
nilivyosema mwanzo
NB:Epuka kuzaana ndugu kwa ndugu (inbreeding) kwani pia hujenga tabia hii kwa majike, itabidi ubadili majike na baada ya vizazi kadhaa utabadili pia madume ili yasizae na watoto wao
Aksante