Ufumbuzi wa Kudumu wa Mgogoro wa Israel na Palestina

Ufumbuzi wa Kudumu wa Mgogoro wa Israel na Palestina

Filosofia ya Rorya

JF-Expert Member
Joined
Sep 20, 2021
Posts
3,211
Reaction score
3,611
Kufuatia dunia kukata tamaa kwamba mgogoro wa Israel na Palestina hauwezikuisha asilani na kwamba dunia imegawanyika katika mgogoro huu kwa kuchukuwa pande mbili ambapo upande mmoja wa dola za Magharibi kushikilia kuiunga mkono Israel (kisirisiri) na upande wa dunia ya Waarabu na Waafrika wakiungana kutengeneza upande kinzani kwa kuiunga mkono Palestina katika mgogoro huo kwa kuilaumu Israel kwa uvamizi wa ardhi ya Wapalestina kinyume na haki, nadhani hatujafikia ukingo wa kutafuta suluhu ya kudumu.

Mapendekezo yangu:

1. Ninapendekeza kwamba ili kumaliza tatizo hili, Afrika iamue kutoa eneo kwa ajili ya hasimu mmoja kuanzisha utaifa wake ili hasimu mwingine ndiyo abakie Mashariki ya Kati kumiliki maeneo mawili ya Israel na Palestina kwa pamoja kutengeneza utaifa wake.

2. Mbadala na hilo, ama Wapalestina au Waisraeli, mmoja ahamishiwe katika moja ya nchi za Afrika badala ya kutengeneza taifa jipya.

Angalizo:

Afrika Kusini
weupe na weusi wanaishi taifa moja (kwanini Israel na Palestina zisiunganishwe kuwa taifa moja?).

Amerika weupe na weusi wanaishi taifa moja (kwanini Israel na Palestina zisiunganishwe kuwa taifa moja?).

Sudan ya zamani Waarabu na weusi waliishi taifa moja kabla ya Sudan Kusini kuanzishwa (kwanini Israel na Palestina zisiunganishwe kuwa taifa moja?).

Canada ni mchanganyiko wa races wanaoishi taifa moja (kwanini Israel na Palestina zisiunganishwe kuwa taifa moja?).

Australia weupe (Waingereza) na weusi (Aborigines) wanaishi taifa moja (kwanini Israel na Palestina zisiunganishwe kuwa taifa moja?).

Mauritius weusi na machotara wa Kihindi wanaishi taifa moja (kwanini Israel na Palestina zisiunganishwe kuwa taifa moja?).

Haiti weusi na machotara wanaishi taifa moja (kwanini Israel na Palestina zisiunganishwe kuwa taifa moja?).

Liberia weusi (Afro-Liberians) na weupe (Americo-Liberians) wanaishi taifa moja (kwanini Israel na Palestina zisiunganishwe kuwa taifa moja?).

Afrika pekee yenye nusu ya rasilimali zote za sayari sehemu yake inayokaliwa na binadamu ni takriban 50% sawa na maili za mraba 5.85ml, sehemu iliyosalia ya ukubwa huo haikaliwi na binadamu (Afrika ina ukubwa wa maili za mraba 11.7ml). Israel ina idadi ya watu 9.3ml 2020 UN, Palestina ina idadi ya watu wapatao 5.2ml 2020 UN. Ukubwa wa Israel unaingia kwa Tz mara 45.4 (ukubwa wa Tz ni 945,203 km2, ukubwa wa Israel ni 20,770 km2).

Kama wazo hili lingetekelezwa unadhani kati ya Wapalestina na Waisraeli wepi ungependa waletwe Afrika au katika nchi yako? Sababu zako ni zipi?

1637916832296.png

1637916865579.png

Taswira zote kwa hisani ya google.
 
Pamoja na maelezo yako lakini hujui wanagombania Nini wale
 
Yaani unataka kuwaunganisha Tom and Jerry! Kweli! Utamu wa series utaisha sukari mapema sana na show haitakuwa ikibamba tena..
 
huo mgogoro NI kipimo cha mwisho wa dunia.
Dalili kubwa Moja wapo za dalili za mwisho wa dunia.
NI PARESTINA KUMSHINDA ISRAEL.
 
Kwamba hujawahi sikia kuwa waisrael walipewa eneo Uganda baada ya vita ya pili ya Dunia kuisha .
 
Sisi waafrika wenyewe tuna mamigogoro yasiyoisha tena ya kijinga tu.ndio tukaribishe matatizo mengine kweli?
 
Kwamba hujawahi sikia kuwa waisrael walipewa eneo Uganda baada ya vita ya pili ya Dunia kuisha .
Naelewa mkuu, kwa muhtasari iko hivi:

Baada ya vita kuu ya pili ya dunia WWII, UN iliazimia kuwahamishia Waisraeli wote nchini Uganda kupisha Wapalestina, Mhe. Waziri
Mkuu wa Israel Ben Gurion alipopata habari hizo aliona waziwazi kupoteza dola (siyo taifa) la Israel, alichofanya Mhe. Waziri Mkuu ni kujiwahi kwenda moja kwa moja kwa Rais wa US Mhe. Harry Truman na kumwomba kwamba kwa influence ya nafasi yake na ya nchi yake atangaze kinyume na UN kwamba US inatambua rasmi uwepo wa dola la Israel kwenye ramani ya dunia. Baada ya tangazo hilo la US kila kitu kikabadilika UN kuhusu Israel na mchakato wa kuipa uhuru ukaanza na ilipotimu 1948 kwa tangazo la UN Israel ikatangazwa kuwa taifa huru. Kumbe inawezekana kuhamishwa taifa (taifa ni watu) kwenda sehemu nyingine. Dunia ihamishie Afrika taifa moja kati ya Israel na Palestina.

Australia kwa asili haikuwa ya weupe (Waingereza) bali ya Aborigines. Baada ya mapinduzi ya kwanza ya viwanda katika karne ya 17 yaliyoasisiwa na Malkia Victoria matumizi ya mitulinga katika uzalishaji mali na utoaji huduma yalipungua baada ya kupatikana mashine za kurahisisha kazi, ndipo wafanyakazi wengi wa viwandani wakapunguzwa na kuibua tatizo lingine la wahuni na wazururaji (uhalifu wa kuhujumu hata na viwanda vyenyewe) ambao waliisumbua sana Uingereza, ndipo Bunge likaamua kwamba wachukuliwe wazururaji wote na wahalifu wote wapakiwe kwenye meli kubwa wakatupwe kwenye kisiwa cha mbali huko ambako hawataweza kurudi Uingereza. Walipotupwa kwenye kisiwa cha Australia ndipo wakajifua na kujipanga kumiliki kisiwa kile na kuanza kuzaana na kujitengenezea ustaarabu mpya uliowafikisha leo hapo walipo. Walipohamishiwa Australia walikuta Aborigines (kama vile) bado wako kwenye stage ya Homo Erectus ya Evolution ya binadamu (macho yako kwenye paji la uso).
Kumbe inawezekana kuhamishwa taifa (taifa ni watu) kwenda sehemu nyingine. Dunia ihamishie Afrika taifa moja kati ya Israel na Palestina.
 
haiwezekani hao watu kuunganishwa kuwa taifa moja, maana waisrael ni wabaguzi na roho mbaya hawawez kuish na watu wasio wa damu zao maana hujiona wao watu special sana dunian,

vile vile ni ngumu kuwaondoa wapalestina katk ardhi yao, wao wanaona bora wapambane mpka kufa, ila si kumuachia ardhi mtu wakuja,

kuhusiana na kupewa ardhi kwa hao watu tokea afrika, hiyo haiwezekan maana afrika ishamegwa sana, na hata iyo ardhi wanayogombania imemegwa kutoka ktk afrika ambayo ilikaliwa na watu weusi hapo kabla ushahid upo, na ndyo hao hao watu weusi ambao walitambulika kama israel ya kale kabla ya ujio wa hao watu weupe na kubadiri historia.

wapalestina si wakulaumiw, bali wakulaumiwa ni hao israel waliovamia hilo eneo na kujimilikisha kibabe.

waisrael hawana ushahidi wa umilik wa iyo ardhi zaid watasingizia Ni agano la Mungu wao na mahali alipoishi ibrahimu,

cha ajabu ukija ktk historia ya kisayansi na shahid za kwel, hutowai kuona kuwa kuliwai kuwa na taifa lolote la mtu mweupe eneo hilo ktk kipind wanachokisema wao waisrael kuwa waliishi wakina ibrahim,
pia hakuna ushahid wa uwepo wa jamii za hao watu wanaotajwa na maandiko kuishi eneo hilo, hawapo na hawakuwai kuwepo,

jiulize kama historia inaproof uwepo wa mafarao walioishi zaidi ya miaka3000bc sasa why hakuna ushahid wa uwepo wa waisrael ama wahusika wa uyahudi eneo hilo la sasa wanalogombea? jibu unapata nikuwa hao waisrael wa sasa ni watu wa ujanja yaan walipindua meza kwa kuiba historia isyo yao, na kuitumia kumikil eneo la middle east kwa manufaa yao wao na manufaa ya wamagharibi na ulaya.

popote palipo na huyo muisrael kuna mikono ya wamagharib na USA, na amani ya mahala hapo haiwez kuisha mpka haki ya kwel itakapopatikana.

haki ya kwel haipo kwa hao wapalestina wala kwa hao waisrael feki, bali haki ya kwel ipo kwa mtu mweusi alieibiwa ardhi, akuwawa, akanyanyaswa na kupora historia yake, na ukweli huu hautowai kuupata toka kwa watetezi wa dini&diplomasia zenye malengo ya utetezi wa hawa mabwana wawili yaan USA(wazungu)&waarabu.

Siku inakuja ambapo ukwel utajulkna
 
Naelewa mkuu, kwa muhtasari iko hivi:

Baada ya vita kuu ya pili ya dunia WWII, UN iliazimia kuwahamishia Waisraeli wote nchini Uganda kupisha Wapalestina, Mhe. Waziri
Mkuu wa Israel Ben Gurion alipopata habari hizo aliona waziwazi kupoteza dola (siyo taifa) la Israel, alichofanya Mhe. Waziri Mkuu ni kujiwahi kwenda moja kwa moja kwa Rais wa US Mhe. Harry Truman na kumwomba kwamba kwa influence ya nafasi yake na ya nchi yake atangaze kinyume na UN kwamba US inatambua rasmi uwepo wa dola la Israel kwenye ramani ya dunia. Baada ya tangazo hilo la US kila kitu kikabadilika UN kuhusu Israel na mchakato wa kuipa uhuru ukaanza na ilipotimu 1948 kwa tangazo la UN Israel ikatangazwa kuwa taifa huru. Kumbe inawezekana kuhamishwa taifa (taifa ni watu) kwenda sehemu nyingine. Dunia ihamishie Afrika taifa moja kati ya Israel na Palestina.

Australia kwa asili haikuwa ya weupe (Waingereza) bali ya Aborigines. Baada ya mapinduzi ya kwanza ya viwanda katika karne ya 17 yaliyoasisiwa na Malkia Victoria matumizi ya mitulinga katika uzalishaji mali na utoaji huduma yalipungua baada ya kupatikana mashine za kurahisisha kazi, ndipo wafanyakazi wengi wa viwandani wakapunguzwa na kuibua tatizo lingine la wahuni na wazururaji (uhalifu wa kuhujumu hata na viwanda vyenyewe) ambao waliisumbua sana Uingereza, ndipo Bunge likaamua kwamba wachukuliwe wazururaji wote na wahalifu wote wapakiwe kwenye meli kubwa wakatupwe kwenye kisiwa cha mbali huko ambako hawataweza kurudi Uingereza. Walipotupwa kwenye kisiwa cha Australia ndipo wakajifua na kujipanga kumiliki kisiwa kile na kuanza kuzaana na kujitengenezea ustaarabu mpya uliowafikisha leo hapo walipo. Walipohamishiwa Australia walikuta Aborigines (kama vile) bado wako kwenye stage ya Homo Erectus ya Evolution ya binadamu (macho yako kwenye paji la uso).
Kumbe inawezekana kuhamishwa taifa (taifa ni watu) kwenda sehemu nyingine. Dunia ihamishie Afrika taifa moja kati ya Israel na Palestina.
Kama Israel ingehamishiwa Uganda, leo Uganda ingekuwa taifa kubwa sana duniani, kiuchumi, kiulinzi, kisiasa nk, na Afrika ingekuwa na Ma-Super power wawili (South Africa na Uganda). Angalia Australia leo ilivyo na nguvu kubwa almost kuizidi au kuikaba koo UK.
 
haki ya kwel haipo kwa hao wapalestina wala kwa hao waisrael feki, bali haki ya kwel ipo kwa mtu mweusi alieibiwa ardhi, akuwawa, akanyanyaswa na kupora historia yake, na ukweli huu hautowai kuupata toka kwa watetezi wa dini&diplomasia zenye malengo ya utetezi wa hawa mabwana wawili yaan USA(wazungu)&waarabu.
Nimependa aya hiyo hapo juu mkuu. Inafikirisha upya!
 
Back
Top Bottom