Elections 2010 Ufunguzi wa Kampeni ya Chadema Jangwani 2010



Tuko pamoja Mkuu. asanteni wote.

Regia pia ameonyesha ushirikiano mkubwa sana. Anastahili pongezi.

Mkuu Invisible, in case kutahitajika Video Camera aanytime, na mimi pia naungana na Indume, naweza kutoa yangu pia.

Naamini sana JF inafanya kazi yake vema kipindi hiki.
 
Kweli siasa ina mambo hasa. Mnajenga hoja ya nchi kuja kuongozwa na mambumbu?!! Darasa la saba! Haipo hiyo.
 

kwa kauli zako mbovu we ni m.s.e.n.g.e. Tumekuwa jangwani watu wa kada zote. Unaposema wahudumu wa baa unachefua wengi. Wasomi unaowajua wewe wameiletea nini nchi? Huyo 'dk' kikwete kafanya nini? Wasomi akina lowasa, rostam, ridhiwan, karamagi et al walioko ccm wamefanya nini? Watch out, boy
 
chadema ilimchagua vipi mgombea wake wa nafasi ya makamo wa raisi ikiwa hana uzoefu wowote wa kazi na ana elimu ya msingi tu? walitumia vigezo gani kuona huyu anafaa kuwa makamo wa rais na wakati wa dharura kuwa rais wa nchi?

au randomly selected kwa kuwa 'mtu yoyote anaweza kuwa mbunge'?

inashangaza kuona chama mbadala kina justfy matendo yake kwa kujifafanisha na ccm!

:confused2:
 
A vice president is a heartbeat away from being president......question is...can he president?

Let me keep quite lest I be excoriated for talking about 'irrelevant foreign issues'.
 

Kanyafu, achana na hesabu za kufikirika. Kwako 1=1=3, makubwa!!!! Una maana gani unaposema Slaa ameingia choo cha kike, unataka kudharirilisha akina mama, dada zako, mama zako nk !!! Ushindwe na ulegee!!!
 
Ilikuwa lazima CHADEMA kufungulia kampeni sehemu hiyo hiyo kama ratiba ya C.M.M? Jamani CHADEMA, tuonyeshe creactivity
 
</H2>Nostradamus:Tatizo si uongozi pekee,tuwe wazi,kubadili utawala bila kubadili fikra bado kunaturudisha pale pale!We have a problem within our own heads kama raia.Si kila lawama kwa serikali!

Nostradamus nakubaliana na wewe kuwa matatizo yetu sio serikali peke yake, lakini nafikiri UONGOZI/LEADERSHIP huuelewe vizuri. Kiongozi ndiye anayeweka vision yake kwa wananchi, ndiye anayewapa direction wamfuate, ndiye anayewapa energy ya kuweza kwenda safari ya mbali japokuwa resources zipo kidogo. Ukiona nchi haiendelei ujue haina vision, haina mtu wa kuipa direction. Ukiona rushwa na ufisadi vinapamba moto ujue hiyo ndiyo vision ya viongozi. Ukiona wananchi wengi hawana elimu ujue Viongozi wameshindwa kuwafanya wananchi waone umuhimu wa elimu. Ukiona wananchi wanawachoma vibaka ujue Viongozi wameshindwa kuwafanya wananchi wawe na imani na mfumo wa sheria. Leta hoja nakusubiria, nataka unishawish kuwa matatizo yetu hayatokani na UONGOZI mbovu
 
A vice president is a heartbeat away from being president......question is...can he president?
I agree, to the extent that the V.P. is that close to presidency. But beyond that I must add that your appreciation of election year politics in Tanzania is oft-times a bit off-key. Traditionally, the profile of prospective VP is a total non-factor.

Rashidi Mfaume, Idris Wakil, Ally Mwinyi, Othman Juma, Shehe Mwinyi Jumbe, and this Alli Shein guy, were all political goofs and goons whom nobody thought of for more than three seconds when they were elected V.P's.

When Rashidi Mfaume abruptly took over the reins from Nyerere in 1962 the sky didn't fall on our heads, and when a Hassan Mwinyi ascended to presidency from total Michenzani obscurity the country arguably prospered, with a near unanimous consensus among many presidential observers that Shehe Mwinyi "freed" the nation. So, we have never worried about the eventuality of an eerie V.P. landing at Ikulu.

Indeed this general apathy over the VP may not portend a healthy scenario for our country, after all we're living in such uncertain times when the incumbent president is dogged by nasty black-out drop-down seizures which no doctor in the country can explain. But suffice is to say, we just don't give a hoot about the second fiddle at Ikulu. I wouldn't mix up local politics with electioneering concepts from a different universe.
 
WanaJamii tujaribu kuwa serious na wahalisia....ni bora ku accept ukweli kwa sababu ukweli unakupa uhuru wa mawazo.
Jamaa ni standard 7 period....huwezi ukafananisha enzi hizi na za mwalimu ambapo Kawawa alikuwa VP,hata hivyo angalia Mwl.Nyerere alivyokuwa anamburuza...hata story za Kawawa kuambiwa afunike kikombe ili wahudumu wasiendelee kuleta chai zinaweza ashiria sthng relating to his education level.

Unacceptable kuwa na VP std 7..hapa jamaa walichemsha......form IV tu ni mashaka kupata even ukarani in this era..iwe std 7 na u VP!!!

Ni mtizamo tu~~~~
 

Asante umeniwakilisha
 

Hivi kipi bora kati ya kuchagua kati ya Rais darasa la saba au Rais mgonjwa, tuseme umelazimishwa upate mmoja kati ya hao
 
Wafundishe wanao hesabu nyumbani,don't send them to school and when they are 23 send them to look for a job bila vyeti.Ni system ya ulimwengu!!!
 
Hivi kipi bora kati ya kuchagua kati ya Rais darasa la saba au Rais mgonjwa, tuseme umelazimishwa upate mmoja kati ya hao

Sitaki kuamini kama tunaweza kufikiria hadi hapa tu.

Neither of the two Mheshimiwa
 
Kumbe unazungumzia utafiti wa shuleni?nilikuwa sijakupata.Come on hivi unaamini katika hili?madesa na simbi kwa sana..

Dada regina Elimu haina mbadala.Tizama Video ya Mkutano wa jana.Jangwani kukiri kwa Slaa na Mbowe kuwa elimu haina maana yeyote ni kuonesha kuwa Chadema hawako serious kwenye elimu.karne hii Graduate wako wengi sana kule Zanzibar kuna Digrii Nyingi tu.jiulize Dr.Bilal Gharib amefanya kazi Marekani na ana elimu kubwa sana kwenye Nyuklia.ameshiriki kuasisi Udom na anajitolea kufundisha.
huyo ni mgombea mwenza wa CCM.

Mkuchukue Juma Duni ana masters na uzoefu mkubwa ana uwezo mkubwa wa kujenga Hoja. sasa watu hawa wawili walinganishe na Mgombea Mwenza wenu.inaonekana hamko Serious.

Dr.Shein kuwa na PhD lazima kuna mambo mengi amefanya kwenye tafiti zake kama hilo linamzidishia umakini na uwezo wa kazi.Elimu ni suala nyeti sana kwenye uongozi.kubalini kosa.
 
Alnadaby sio kuwa kama Mwalimu angekuwa hai, alishawahi kutamka katika moja ya hotuba zake kuwa CHADEMA ni chama makini. Nafikiri wengine Mwalimu Nyerere mnamsikia tu. Hivyo msimdandie tu.
Wengine tulikuwepo hata wakati anahutubia kuwa "Ukifuga kuku, baada ya kutoa gharama unatakiwa kugawana sawa kwa sawa na mfanyakazi wako"
 
PAx nani amesema Tanzania haiendelei. Inategemea ni maendeleo yapi unayoyataja. Tanzania tumeemndelea sana katika Ufisadi na Rushwa na hiyo ndio vision ya current CCM. Hata donors wananwashindwa strategy CCM walizonazo kufanikisha wizi wa rasli mali za taifa na donor resources. Hivyo kazi ya kwanza ni kurejesha Peoples Power aliyoua Nyerere
 
Katika uzinduzi wa kampeni za chadema jana nilishangazwa na tukio la mgombea urais wa chadema kusahau kuzungumzia uchumi wa taifa. Ambapo ndio kitu muhimu sana. Yeye alijikita na habari za ruge na house of talent, badala ya kujadili issue za kitaifa. Wao ugomvi wa watu wawili wameufanya ndio sera za chama. Akajikita na uendeshaji wa kesi mahakama ya kisutu.

Kama chama chadema kingezungumzia suala za uendeshaji kesi zote yaani mfumo wa sheria nchini, sio kujadili kesi moja au mbili za mahakama ya Kisutu.

Slaa ameshindwa kusema kuwa JK amechagua majaji wangapi kurahisisha mfumo wa sheria.

Nilivunjwa mbavu pale John Shibuda alipompelekea desa bwana slaa kuwa mzee umesahau kuzungumzia uchumi. Slaa kwa ufahamu wake mdogo akatamka hadharani akisema 'nakushukuru ndugu yangu Shibuda kwa kuniletea karatasi kunikumbusha nizungumzie uchumi"

Chama makini kingezungumzia uchumi kutokana na mambo kadhaa yaliyojiri hivi karibuni dunian na hapa nchini mambo kama credit crunch na mengi ya mfano huo. Riba na uchumi wa nchi. Yeye alikuwa busy kuzungumzia neno moja tu ufisadi.

Sasa kama shibuda angekuwa hayupo jana ingekuwaje? Hilo ndio tatizo la chama kuwa na watu wenye elimu ya darasa la saba na kidato cha nne kama mbowe na mgombea mwenza wa Slaa.

Mgombea mwenza angekuwa msomi au mwenye uelewa angemsaidia Slaa.

Chadema mshukuruni sana Shibuda kafanya kazi nzuri ingawa hamkumpa nafasi ya kuzungumza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…