Nimeisoma ilani ya Chadema na mwanzoni kabisa nimeanza kuona tatizo lile lile ambalo Chadema wanasema wanapingana nalo.Longolongo na kutoweka jambo wazi kwa mapana yake.Sehemu iliyoanza kunipa mashaka kabla hata sijafika mbali ni hii:

Ufisadi ni nini?

Tunapozungumzia Ufisadi tunazungumzia mfumo na muundo wa utawala ambao umetengeneza utamaduni wa kuishi kiujanja ujanja, matumizi mabaya ya madaraka na vyeo, ufujaji wa mali ya umma, wizi wa fedha za umma, utaratibu wa kubebana na ajira zinazotegemea kujuana, na mahusiano ya watawala na watawaliwa ambayo msingi wake ni woga, vitisho, na kujiona watu wanastahili zaidi kuliko wengine. Ni mfumo uliodidimiza tawala mbalimbali duniani na ambao pasipo kuushughulikia kwa makusudi unasimama kama tishio lilopo na la hatari kwa Tanzania kuliko vita. Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere alisema kuwa "ufisadi na rushwa ni adui mkubwa zaidi wa maslahi ya wananchi wakati wa amani kuliko vita" (Bungeni, Mei 17, 1960, kikao cha 35 cha bajeti).

Ufisadi ndio kizuizi kikubwa cha kuboresha maisha ya watu wetu; ni kikwazo kikubwa katika kujenga na kuimarisha utawala bora, utawala wa sheria na haki za raia. Ufisadi ndio kikwazo kikubwa kabisa cha maendeleo ya nchi. Ndio kusema, juhudi zetu za kujiletea maendeleo kama nchi haziwezi kufanikiwa bila kwanza kukomesha ufisadi.

Tumekuwa na miaka takribani 50 ya CCM. Wameahidi kila aina ya ahadi na wamefanya kila makosa, lakini tukawavumilia na tukawapa nafasi nyingine tukiamini kwamba mambo yatabadilika. Kila tulipowapa nafasi, hali ilizidi kuwa mbaya, tukasogea kutoka kubaya kwenda kubaya zaidi. Lengo lao kubwa limekuwa ni kushinda uchaguzi, ili waendelee kutumia madaraka tunayowapa kwa ajili ya kujinufaisha kwa njia ya ufisadi.

Ni wakati wa mabadiliko, na fursa ya kufanya mabadiliko ni huu uchaguzi wa 2010 na siyo 2015. Tukisubiri wakati mwingine tutakuwa tumechelewa sana. Na tukiwapa nafasi nyingine moja CCM ya kututawala tena tutakuwa tumewapa leseni ya kuendelea kutawala wapendavyo na tutakuwa tumejihukumu sisi wenyewe na uzao wetu katika maisha ya umaskini wa kudumu.

Katika sehemu hiyo ni wazi kuwa Chadema wanataka umma uamini kwamba matatizo yote tuliyo nayo yanatoka na utawala!

Wanataka tuamini hata wale watu wanaotumia vyandarua kufugia kuku badala ya kujikinga na malaria kuwa ni tatizo la watawala.

Wanataka tuamini kuwa serikali inawafuatilia wakwepa kodi sugu kuwa ni unyanyasaji simply kwa sababu JK kapita mahali basi hata kama TRA walitaka kudai kodi basi wasidai tena.

Wanataka tuamini hata kushindwa kwetu kuweka akiba na kujaa kwenye sehemu za starehe siku za kazi,kuchangia mambo ya burudani zaidi kuliko elimu na maendeleo yote hayo kuwa ni tatizo la serikali!!!!!

Ilani haisemi kwamba hakuna chama kinachoweza kuwaondolea watu umasikini kwa asilimia mia. Natumaini Chadema watajipanga zaidi miaka ijayo kuelezea wananchi kwamba elimu ya kujitambua binafsi ni muhimu sana kabla ya lolote.On top of that Chadema inasema kwamba 2010 ndo wakati muafaka!!!

What are the justifications kwa hili??U mean 2010 ndo Chadema imeona nchi inaporomoka au ni ile "I wana be the boss too"!!!

MUNGU IBARIKI TANZANIA.