Ufunguzi wa Mkutano wa Mwaka wa Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi

Ufunguzi wa Mkutano wa Mwaka wa Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Wakuu tufuatilie hii live inaendelea sasa Mgeni Rasmi akiwa Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango


View: https://www.youtube.com/live/Gt5cxeNI90U?si=IYfVYZ27diQ2bosr

Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania IGP Camillus Wambura:

Mkuu wa jeshi la polisi nchini Camillus Wambura amesema jeshi hilo halitovumilia mtu au kikundi cha watu watakaojaribu kuvunja amani ya nchi kwa namna yoyote ile.

“Jeshi la Polisi liko imara na litaendelea kuhakikisha kuwa nchi yetu inakuwa shwari wakati wote na halitomvumilia mtu au kikundi cha watu watakaojaribu kuvuruga amani ya nchi yetu kwa namna yoyote ile.” Amesema Camillus Wambura.

Aidha amesema hivi karibuni vilijitokeza vikundi vya baadhi ya watu kwa mwamvuli wa siasa, demokrasia na uanaharakati na kuanza kuleta taharuki na kufanya vitendo vya uvunjifu wa amani kwa kutoa maneno ya uchochezi katika majukwaa mbalimbali yakiwa na uelekeo wa kuvuruga amani ya nchi na tayari jeshi la polisi limechukua hatua stahiki za kisheria kudhibiti vitendo hivyo vya kihalifu na sasa hali ni shwari.

"Nchi yetu ipo salama hali ya utulivu ni mkubwa, leo hii tumeamkaa salama na tuna uhakika kwa jinsi tulivyojipanga na mikakati yetu nchi hii itaendelea kuwa salama. Aidha hivi karibuni vilijitokeza vikundi vya watu kwa mwamvuli wa siasa demokrasia na uanaharakati kuanza kuleta taharuki ya kufanya vitendo vya uvunjifu wa amani kwa kutoa maneno ya kichochezi katika majukwaa mbalimabali yakiwa na mwelekeo wa kuvuruga amani ya nchi yetu. Tayari Jeshi la Polisi limeshachukua hatua stahiki za kisheria katika kudhibiti vitendo hivi vya uhalifu na sasa hali ni shwari na inaendelea kuwa shwari"

Jeshi la Polisi limejipanga vyema katika kuhakikisha uchaguzi mkuu ujao unafanyika kwa amani na utulivu"

Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango: Jeshi lina wajibu wa kuhakikisha amani, utulivu na usalama wakati wa uchaguzi huu wa Urais, wabunge na udiwani. Uchaguzi huu unahusisha wadau wengi wakiwemo wananchi wenye itikadi mbalimabali za kisiasa, wagombea wa nafasi mbalimbali iko tume huru ya uchaguzi, vongozi wa dini na mila lakini wapo na wanaharakati pamoja na waandalizi wa uchaguzi wa ndani na nje ya nchi. Sasa ili kufanikisha jukumu hii, ni muhimu Jeshi la Polisi kuimarisha ushirikiano wa karibu na wadau wote wa uchaguzi.

Hatua hii itasaidia kuhakikish kila mdau anatendewa haki. Mitandao ya kijamii hutumika kusambaza sera na ilani ya vyama vya siasa pamoja na wagombea wao. Hata hivyo Mitandao hii pia inaweza kutumiwa kusambaza taarifa za uongo, kueneza uchochezi na upotoshaji wa makusudi jambo ambalo linaweza kusababisha taharfuki.
 
Kumekucha... Kumekuchaaa... Kumekucha, kazi imeanza
 
Back
Top Bottom