Ufunuo usiosemwa: Je, Lilith ndio nyoka wa Eden? Je, ni mke wa kwanza wa Adam?

Mkuu naheshimu mawazo yako lakini kwanini unaamini kila kitu lazima kiandikwe kwenye biblia ndio kiwe cha kweli?? Kumbuka biblia ni compilation tuya vitabu iliyofanywa na wazungu wachache pale constantinople na baadae alexandria yaani katika vitabu 400+ vilichukuliwa 66-72 pekee sasa inakuwaje useme biblia haijaandika?? Kwanni usiseme biblia iliandika ila watu wachache walivitoa???

Anyway habari za lilith zimeandikwa kwenye pseudipigraphi nyingi tu na kwenye biblia ameandikwa kwenye kitabu cha Isaiah na kwenye moja ya maono akifananishwa na BUNDI ila king james version original inamuita LILITH..... Hivyo si kweli kuwa kwenye biblia hajatajwa.

Ni hayo tu mkuu Karibu for clarification huenda sijakuelewa tu....
 
Mwanzo 1:27. Mungu aliumba mwanamme na mwanamke (Adam na LIlith) kutoka mavumbini

Mwanzo 2:22. Mungu akatoa ubavu akamuumba mwanamke. (Adam na Hawa) Hawa akutoka mavumbini

Mwanzo 4:1 Baada ya Adam/Eva kufukuzwa bustanini Adam akamjua mkewe wakawazaa Habili na Kaini

Mwanzo 4:8 Kaini akamuua nduguye Habili

Mwanzo 4:16. Kaini akaenda inchi ya Nodi Mbele ya Eden

Mwanzo 4:17 Kaini akamjua mkewe na akamzaa Henoko (Je mke wa Kaini alikua Lilith au Lilith alipotimuliwa Eden alikua na mimba na alikimbilia Nodi na kujifungua mtoto wa kike .Maswali ni mengi kuliko majibu je Lilith alikua nani????
 
Nilikuwa nina mwananamke anaitwa LILY,nilimpenda sana lakini alichokuja kunifanyia,mungu ndio anajua,naunga mkono hoja ya Mshana Jr kuwa huyo lilith ndio ibilisi shetani aliyefitinisha ndoa ya adam na eve....
Lily ni ua na huyo ni Lilith!
 
Asante kwa kushiriki mjadala na mchango pia...najua kuna baadhi yetu hatutaki kutoka nje ya kile tulichozoea kukiona kukisikia kufundishwa na kusoma...
Natamani tutoke nje ya box bila kuathiri imani zetu na maandiko ya misahafu yetu
 
Asante kwa kushiriki mjadala na mchango pia...najua kuna baadhi yetu hatutaki kutoka nje ya kile tulichozoea kukiona kukisikia kufundishwa na kusoma...
Natamani tutoke nje ya box bila kuathiri imani zetu na maandiko ya misahafu yetu
Kwa kweli!
Biblia inavitabu vingi sana!
 
mkuu labda nitoe maoni yangu kidogo ila sikupingi sababu tunaweza kuwa na vyanzo tofauti......

1.Adam hakuwepo kwenye pre mortal life mkuu labda kama una reference nzuri zaidi ila nachojua wote lilith na adam waliumbwa kwa udongo ila micha-el aliumbwa kwa mwanga na alipewa jukumu la kuhakikisha Adam harudi kwenye bustani ya Eden hivyo micha-el na Adam ni tofauti kabisa.

2.Lilith alikuwepo wakati dunia ya pili imeumbwa ukiachana na ile ya kwanza ambayo iliharibiwa na vita kati ya leviathans na malaika..... Hivyo lilith baada ya kuvurugana na adam akaamua kuolewa na malaika shamael aliekuwa anaishi mbingu ya saba ambaye inasemekana alimpeleka lilith kuzimu and the rest is history
 
Kazi kwelikweli tuache ufia dini wakuu kama yameanzia karne ya 19 mbona viumbe wengi tu wa kale wanatambuliwa na manabii wa biblia mfano LILITH kwenye original king james version anatajwa na nabii Isaiah ina maana nabii isaya aliishi karne ya 19?? Ukisoma agano jipya mara kibao tu Yesu anamtaja HADES Mungu wa kigiriki ya kwamba watu wanaokufa huwa wanaenda kwake HADES je ina maana Yesu kazaliwa karne ya 19??? Tuache ufia dini na tutafiti mshana junior kaleta mada fikirishi tuitafakari sio kuanza kuitana shetani ilihali hata biblia unayoitetea inawatambua miamba hawa unaodai wametajwa karne ya 19!!
 
[emoji23][emoji23][emoji23] yani vitu mnavyoongea ni vya miaka 500 nyuma huko
 
Hayo nimawazo ya watu tena potofu nimesoma PhD ya Theology na nmesoma pia Missiology hamna vitu kama hivyo its better kutoendelea kusambaza uongo huu kwa wengine
 
Huu niuongo
 
Kama lilith waliumbwa siku moja na adamu basi lazima walilingana nguvu na uwezo na pengine adamu akazidi kidogo za lilith maana adamu aliambiwa kuwatawala. Kinachoua hii hoja ni Lilith anatoa wapi uwezo wa kujigeuza nyoka ili hali adamu hana? .
Mkuu labda nimsaidie Mshana Jr kujibu hili..... Ni kweli Adam na Lilith walikuwa na nguvu sawa actually zaidi hata ya malaika ila Adam aliondolewa nguvu hizi za kiungu pale alipokula tunda ila unachosahau ni kwamba lilith aliondoka bila kula hilo tunda actually mambo ya tunda yalikuja baada ya Hawa kuletwa kuziba pengo la lilith.... Hivyo Lilith aliondoka na nguvu zake kama ambavyo shetani aliondoka na nguvu zake alipotolewa mbinguni... Ila Adam nguvu zake ziliisha siku anakula tunda hicho muhim tutambue

Lilith hakula tunda mkuu hivyo ile hukumu ya Adamu ya kwamba atakufa ni ya Adam na hawa pekee ndio maana shetani yeye mpka leo yupo hai na lilith pia sababu wao bado walibaki na nguvu zao za siku zote ila kama Mungu angetamka kuwa wote waliomfanya adam afanye dhambi wafe basi lilith na shetani wangeshakufa kitambo sana kma adam na hawa.

Kama hilo ni dogo kwanni usishangae Yesu aliyekuja kuleta wokovu aliishi miaka 33 pekee hapa duniani ila aliyepinga wokovu toka Yesu wa hapa duniani amekufa yeye bado anaishi milele na anazidi kupotosha watu?? Ukipata jibu la hapo ndio utaelewa kwanni Mungu hakumhukumu lucifer/ lilith kifo siku ile Adam ameasi kwa kula tunda.

Ni hayo tu
 
Mkuu uongo na ukweli unategemeana na source..... Wwe unaposema ni uongo unatumia msingi upi?? Hapa tupo kueleweshana so unaweza ukasema uongo hapo ukwapi ili utusaidie ila kusema ni uongo bila kuweka facts unakuwa hutusaidii.
Nmesoma Missiology pia nmesoma Theology hamna vitu kama hivyo hayo nimachapisho yaliyo andikwa na wale waliokuwa wanajitahidi kumkosoa Mungu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…