Ufunuo usiosemwa: Je, Lilith ndio nyoka wa Eden? Je, ni mke wa kwanza wa Adam?

Hata hiyo habari ya Adam na Hawa nayo ni tungo ya watu tu. Si ya ukweli.
 
Asante naomba nijibu hoja ya tatu....kwanza umeona kabisa nyoka akitambulishwa kwa uwerevu,...vilevile bado ishu yao inabaki kuwa ya kiroho zaidi kuliko kimwili...
Mwili wa nyama una limitatations nyingi lakini mwili wa roho ni powerful vast n very deep
 
Mwanzo 1:27
Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimuumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba..

Mwanzo 2:18
Bwana Mungu akasema, si vema huyo mtu awe peke yake, Nitamfanyia msaidizi wa kufanana nae.
Ndipo Bwana alipomletea Adamu usingizi mzito na kumuondolea ubavu mmoja na kumfanyia msaidizi nae alikuwa ni mwanamke (Eve).
Hii ilikuwa ni baada ya Adamu kupewa mamlaka ya kuitunza bustani ya Edeni..

Je, kuna uwezekano mkubwa huyu Lilith anayetajwa kuwa mke wa kwanza wa Adamu akawa ndiye?

Ukisoma maandiko matakatifu Mwanzo 1:27
Inazungumzia uumbaji wa mwanadamu, maandiko yanasema Mungu alimuumba mwanamume na mwanamke kwa mfano wake....hii ni kabla ya uwepo wa Adamu katika bustani ya Edeni...Na baada ya hapo ndipo Mungu alipo mfanyia Adamu msaidizi wa kufanana nae. Alimuumba Eva kutoka katika ubavu wa Adamu.

Je, huyu mwanamke aliye umbwa pamoja na Adamu (Mwanzo 1:27) kuna uwezekano mkubwa ndiye akawa Lilith???

Maandiko matakatifu hayajaeleza habari za Lilith wala habari za Adamu kuwa na mke kabla ya Eva.. Lakini tukienda nje ya biblia inasemekana Mungu alimuumba Lilith pamoja na Adamu kwa wakati mmoja.

Lilith alikuwa ni mwanamke mwenye akili na nguvu nyingi hivyo kupelekea kushindwa kumtii Adamu na mwisho wa siku aliamua kulikufuru jina la Mungu nae Mungu akamuadhibu na kumlaani yeye pamoja na uzao wake..
 
Hili nalifahamu vizuri kabisa,
Lakini hakuna sehemu kwenye Biblia kuna ushahidi wa kwamba pepo kamvamia pepo.
Yeah ulimwengu wa roho ni replica ya ulimwengu wa nyama ....chochote cha kiroho kina mfanano na tafsiri ya kimwili na kinyume chake
 
Nimesema wazi habari za Lilith hazitajwi almost kabisa kwenye Bible
 
Mimi ambacho nataka hapa ni ushahidi wa roho kuingia roho,
Au kiingereza nisema "An evidence of a demon possessing a demon"
 
Ukijua habari za Mungu ni hekaya tu, hivi vibwagizo vya habari hiyo sijui Adam na Hawa na Lilith haviwezi kukusumbua.
[emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3] missed you
 
Daah kazi kweli kweli

I nashangaza sana yaan Lucifer aliyemuasi Mungu na akasababisha Kina Adam na Hawa kula tu hakuhukumiwa kufa ameachwa tu anadunda ila aliyepewa tunda akala akaondolewa nguvu zote na mamlaka plus kufa
 
[emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3] missed you
Huo nao ni ushahidi Mungu hayupo.

Angekuwepo tungekuwa tuna uwezo wa kuwasiliana muda wote bila kutumia kifaa chochote na hakuna ambaye angem miss mwingine.
 
Mimi ambacho nataka hapa ni ushahidi wa roho kuingia roho,
Au kiingereza nisema "An evidence of a demon possessing a demon"
Sidhani kama utaweza kupata ushahidi kama huu kwakuwa roho sio visible sanasana nitakupa tu mifano ya haunted souls nk
 

Unaandika habari za biblia ila kwa vyanzo vya kufikirika,huna hata reference yoyote kwenye maandiko unakotoa title ya story yako,just tu unaandika "INASEMEKANA" inasemekana na nani?,umeona wapi ilipoandikwa kwenye maandiko hayo unayosema inasemekana? how tu uje na neno lilith umelitoa wapi?,na pia INASEMEKANA wewe ni muongo unajiandikia andikia tu kwakuwa una bundle ya kutosha!
Na pia INASEMEKANA unamatatizo kama TULIVYOONA kwenye post zako za nyuma ndio hayo matatizo yanakupelekea uwe unatamaa ya kupost post mara kwa mara hata kama huna hoja wala evidence za msingi
Ndugu mshana next time unapokuja na hoja kama hizi useme mapema kama ni swali unauliza unaomba ufafanuzi au ni habari ambayo umeireserch so unataka wenzio tujue au ni story tu ya kusadikika iliyosheheni habari za "inasemekana"
 
Huo nao ni ushahidi Mungu hayupo.

Angekuwepo tungekuwa tuna uwezobwa kuwasiliana muda wote bila kutumia kifaa chochote na hakuna ambaye angem miss mwingine.
[emoji15] [emoji3] [emoji3] huo ndio ushahidi sasa wa uwepo wake....mawasiliano yanakuwa yapo kama kuna nishati kisababishi kati ya pande mbili ambazo ziko controlled na main server
God as main server amesababisha nikumiss lakini kisabishi cha mawasiliano (JF) kilikuwa hakipo
 
Asante sana kwa kushiriki na kuchangia mjadala....endelea kuufuatilia una mengi ya kujifunza...
Nami pia najifunza kama wengine wanavyojifunza....hii ndio aina yangu ya uandishi si kila mmoja anaweza kuipenda....cha muhimu ni kwamba tunapata wote maarifa hata tusipokiri
 
kwa hiyo lilith ni shetani au mke wa Adam
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…