Mkuu labda nimsaidie
Mshana Jr kujibu hili..... Ni kweli Adam na Lilith walikuwa na nguvu sawa actually zaidi hata ya malaika ila Adam aliondolewa nguvu hizi za kiungu pale alipokula tunda ila unachosahau ni kwamba lilith aliondoka bila kula hilo tunda actually mambo ya tunda yalikuja baada ya Hawa kuletwa kuziba pengo la lilith.... Hivyo Lilith aliondoka na nguvu zake kama ambavyo shetani aliondoka na nguvu zake alipotolewa mbinguni... Ila Adam nguvu zake ziliisha siku anakula tunda hicho muhim tutambue
Lilith hakula tunda mkuu hivyo ile hukumu ya Adamu ya kwamba atakufa ni ya Adam na hawa pekee ndio maana shetani yeye mpka leo yupo hai na lilith pia sababu wao bado walibaki na nguvu zao za siku zote ila kama Mungu angetamka kuwa wote waliomfanya adam afanye dhambi wafe basi lilith na shetani wangeshakufa kitambo sana kma adam na hawa.
Kama hilo ni dogo kwanni usishangae Yesu aliyekuja kuleta wokovu aliishi miaka 33 pekee hapa duniani ila aliyepinga wokovu toka Yesu wa hapa duniani amekufa yeye bado anaishi milele na anazidi kupotosha watu?? Ukipata jibu la hapo ndio utaelewa kwanni Mungu hakumhukumu lucifer/ lilith kifo siku ile Adam ameasi kwa kula tunda.
Ni hayo tu