Ufunuo usiosemwa: Je, Lilith ndio nyoka wa Eden? Je, ni mke wa kwanza wa Adam?

Mkuu walioanzisha nadharia hii wanatumia mstari huu

Mwanzo 2:23
23 Adamu akasema, Sasa huyu ni mfupa katika mifupa yangu, na nyama katika nyama yangu, basi ataitwa mwanamke, kwa maana ametwaliwa katika mwanamume

Hapa ndio wakahoji why Adam aseme SASA HUYU.... Ikimaanisha alikuwepo mwingine so anafanya ulinganisho
 
Haya ndo matatizo ya kuzungumzia masuala ya imani kwa kutegemea waganga wa kienyeji, wachawi, wazimu, wapiga ramli n.k
 
Neno la Mungu halikosolewi au halisahihishwi kwa kuweka mapenzi yako liwe utakavyo wewe, huko ni kukengeuka ndg yangu mshana jr
 
kabla ya huo mstari rudi nyuma kidogo Adamu analetewa wanyama wote anawapa majina lkn mwisho haoni wa kufanana nae kwa hali ya kawaida baada ya kumuona mwanamke lzm angetamka maneno hayo hiyo sio hoja labda kama kuna source nyingine zaidi ya biblia tujenge hoja yetu hapo.
 
Fiction tu hamna kitu cha hivyo..!

Ata uandishi wako ni wa kuungaunga tu.
 
Neno la Mungu halikosolewi au halisahihishwi kwa kuweka mapenzi yako liwe utakavyo wewe, huko ni kukengeuka ndg yangu mshana jr
Mkuu nadhani mshana hajakosoa neno la Mungu ila ameanzisha tu mjadala ili kuendelea kujadili kwa uelewa mpana!

Kama tungekuwa kwenye mdahalo Basi tungesema @Mshanar Jr amechokoza mada tu!
 
Kama sikosei, wewe ni wale wasio amini uwepo wa Mungu? right? if that is the case then nadhani hatuwezi kwenda pamoja cause mi nitakua nafanya reference kwenye vitabu ambavyo wewe huviamini and hence utakua ni upotezaji wa muda wa each other!
Kama vitabu vyako haviwezi kuthibitishwa kwamba ni vya ukweli na si hadithi tu, na wewe unavichukulia kama vya ukweli, hata usipojadiliana nami, ukaendelea kuvitumia hivyo vitabu kama vya ukweli na si hadithi tu, hata wewe mwenyewe utakuwa unajipotezea muda tu.
 
sawa twende kwenye Tafsiri yako,ya version ya kwanza ya kiebrania,ambao mstari huujui, uweke hapa tuangalie nani alikua anasema hayo maneno...na mimi nitaangalia...kupata earlier version sio ishu bro...
New jerusalem Translation
Genesis 4:1
........I have gotten a man from an angel of the LORD

Hii ndio moja ya translation kutoka biblia ya kiebrania..... Inakubali kuwa cain hakuwa mtoto wa Adam ila mtoto wa MALAIKA sasa naomba uje uikane biblia hapa
 
Samani mkuu ebu niongeze mahalifa kidogo hayo maelezo umenuku kwenye kitabu gani namie nikapitie maana kwangu mapya kabisa
 
Wao wanaanzia hapa
mwanzo 1
27 Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba

Ndio wakasema huenda mwanzo 1 aliongelewa lilith maana aliumbwa muda mmoja na adam ila hapa mwanzo 2 adam anasema SASA HUYU akimaanisha kuwa eva alitoka kwenye ubavu wake tofauti na lilith aliyeumbwa na udongo kama adam na ndio maana hakumheshimu

Na kuna wanatheolojia wameandika machapisho kukubaliana na hili hivyo sio hoja ya wapagani tu bali hata waliokoka na wasomi wa dini kuliko sisi wanakubali hili
 
Simple n very clear
 
Haya ndo matatizo ya kuzungumzia masuala ya imani kwa kutegemea waganga wa kienyeji, wachawi, wazimu, wapiga ramli n.k
Matokeo yake unapata wachangiaji aina yako waliofungwa kwenye box la nira za kiimani ambao hawako tayari kuona nje kuna nini
 
Neno la Mungu halikosolewi au halisahihishwi kwa kuweka mapenzi yako liwe utakavyo wewe, huko ni kukengeuka ndg yangu mshana jr
Naheshimu mno maandiko na imani yangu juu ya Mungu kwenye maandiko yake ni thabiti kuliko mwamba...tatizo hujaelewa kabisa muktadha wa mada
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…