Ufunuo usiosemwa: Je, Lilith ndio nyoka wa Eden? Je, ni mke wa kwanza wa Adam?

Haya majina ya Lily nishakutana nayo mara mbili hv 1.Alikua mpenzi wangu wa shule ambaye tuliachana baada ya kuzalishwa na mwanaume wa kwanza..akakaa mtoto hajakua vizuri akapata Mimba nyingine sasa ivi ana watoto wawili ILA madai yake ni kamrudia MUNGU yani ni mlokole unaeza hisi hajui dhambi yule dada.

wa 2. ni shangazi yangu mke wa mjomba angu kaka wa mama angu huyu wifi ake mama au shangazi angu Aliolewa kwa harusi kubwa nadhani ktk ukoo wetu hapa WACHAGA walijikakamua ila Ndoa haikudumu Shangazi akapata kibwana akamuacha mjomba angu wakiwa tyr kashamzalia watoto wa 3 akaenda kwa mwanaume huko akazaa tena watoto wawili huko.

Sasa ivi karudi anamsumbua wifi ake ambaye ni mama angu amsaidie muombea msamaha kwa Mjomba anataka mrudia MJOMBA angu...Mama angu kila siku akisikia LILY anasema ni SHETANI.

kwa story hiii Hawa kina LILY wana asili ya Huyo Lilith walai...sjawahi ona mtakatifu yani wote VURUMAI....kuna majina sio ya Kuita watoto eti.
 
Ndugu [USER]Mahana Jr[/USER] habari ya Lilith naweza nikaongeza jambo kuwa huyu anaonekana ni kiumbe mwanadamu kama alivyokuwa Adamu, pia upo uwezekano kuwa alikuwa na kizazi kilichoogopwa miongoni mwa binadamu wa mwanzo yaani Adamu,Eva/Hawa,Abeli na hata Kaini.

Hili nitalionesha pale Mungu alipomuuliza Kaini alichokifanya kwa ndugu yake, kuna sehemu Kaini alitakiwa kuhama nchi na hapo akauliza juu ya usalama wake huko aendapo.

Hapa panatupa swali ina maana kulikuwa na wanadamu wengine mbali na familia ya Adamu na Eva/Hawa?

Jibu ni ndio na familia hii inauwezekano ikawa ni familia ya Lilith na Adamu, haiwezekani ikawa ni Familia ya Lilith na shetani/Ibilisi sababu familia ya malaika na wanadamu ilikuja baadae sana kipindi cha Nuhu kwa tamaa za malaika.

Kwa kuwa hakuna panaposema Adamu hakuzaa na Lilith na kwa kuwa kulikuwepo wanadamu wengine mbali na watoto wa Adamu na Eva/Hawa na kwa vile Adamu alikuwa na mke kabla ya Eva/Adamu basi wanafamu hao watakuwa ni watoto wa Lilith na waliishi miongoni mwa wanadamu hadi leo.

Na hichi kizazi kuna uwezekano kikawa ni 'Mzungu' maana ndio kiumbe mwenye mtazamo wa ajabu juu ya imani tangu kale.


VIIXCCCL GrandLodge,ARUSHA
 
Taja hayo maandiko mengine tuyatafute na tuhakiki wenyewe, la unajitekenya na kucheka mwenyewe
 
 
Uchambuzi fikirishi asante sana.. Na kuhusu huyo mzungu nilishawahi kuandika mada hii hapa Je, wazungu sio wakazi asilia wa hii dunia? - JamiiForums

Jr[emoji769]
 
[emoji44][emoji44][emoji44][emoji848][emoji848][emoji848][emoji144][emoji144][emoji144][emoji144][emoji144][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Jr[emoji769]
 
JE UNAMJUA LILITH ?!


Jina hili laweza kua geni masikioni pa wengi labda kwa sababu limetajwa mara moja tu katika Biblia takatifu katika kitabu cha Isaya lakini kuna mengi ya ajabu kuhusu kiumbe huya na zaidi mengi ya kujifunza.

Habari ya Adam na Eva (Hawa) inafahamika na wengi lakini kuna jambo haliko wazi karibu tujifunze pamoja, tuanze kwa kuangazia maandiko ya uumbaji wa Mungu Mwenyezi. Kitabu cha Mwanzo 1:27 kinatujuza kuhusu uumbaji " Kwa mfano wake aliwaumba mwanamume na mwanamke" na Chapter inayofuata Mwanzo 2 ni uuambaji wa Adam na Eva na wengi wanadhani uuambaji huu ndo ule wa chapter ya kwanza. Mungu alipoumba mwanamume na mwanamke chapter ya kwanza huyu mwanamke ni nani hasa ?, sio Eva ni Lilith. Najua unamshtuko, twende taratiibu tukiyasoma maandiko vema na Mungu atujalie utashi wa kujifunza maandiko.

Katika kitabu cha Mwanzo kuna uumbaji mara mbili wa mwanamke. Mwanzo 1 tumeona mungu *aliwaumba* (maana yake aliwaumba mwanaume na mwanamke kwa pamoja) aliwaumba wakiwa sawa kwa pamoja wote kutoka mavumbini wakiwa *sawa* kwa kila jambo maarifa sawa, nguvu sawa, hata urefu na muonekano sawa na hiari sawa. na ndio maana chaptei hiyo hiyo inaelekeza majukumu *sawa* waliopewa Mwanzo 1:28 "Mungu akawaambia zaeni mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha, mktawale samaki na ndege" Ni dhairi majukumu waliopewa ni *sawa* kwasababu walikua *sawa kwa kila jambo*

Baada ya hapo Biblia imekaa kinya kuhusu nini kiliendelea japo chapter za mbele tunakuja kuona tena habari ya uumbaji wa mwanamke kutoka ubavuni kwa Adam (Mwanzo 2:21) na Biblia takatifu inamuita mwanamke huyu Eva, vipi kuhusu mwanamke yule alieumbwa kwa wakati mmoja na Adam wote toka mavumbini ?! yule ni nani ?! haya.., na hata baada ya kuumbwa kwa mwanamke huyu wa pili toka ubavuni mwa Adam, kuna maneno anayatamka Adam nayo yanatupa dondoo muhimu Mwanzo 2: 23 ''Adam akasema, sasa huyu ni mifupa katika mifupa yangu na nyama kaika nyama yangu basi ataitwa mwanamke'' tazama reaction ya Adam baada yakuletewa mwanamke aliyembwa toka ubavuni mwake anaanza kwa kusepa *"sasa huyu ni ....."* maana yake ni kua ameshaishi na mwanamke alieona hakumfaa na ndo maana anasema *"sasa huyu ni ....."* Adam anaonekana kumkubali mwanamke huyu wa pili na anatoa sababu kabisa kua ametoka katika mifupa yake. JE kwanini kuna uumbaji mara mbili wa mwanamke ?. JE nini kilitokea kwa mwanamke wa kwanza ?. maswali haya nitayajibu lakini kwanza lazima kutambua kua uumbaji wa mwanamke uko mara mbili katika biblia na zifuatazo ni ushahadi wa hilo:-

> Uumbaji wa mwanamke wakwanza unafanzika Mwanzo:1 wakati uumbaji wa mwanamke wa pili unafanyika Mwanzo:2

> Mwanamke wa kwanza katajwa kuubwa kutoka mavumbini na wa pili toka ubavuni.

> Mwanamke wa kwanza anatajwa kua sawa na Adam ila wapili anatajwa kua sehemu tu ya Adam.

> Mwanamke wa kwanza anatajwa kuwa na majukumu sawa na Adam wakati mwanamke wa pili anatajwa kua msaidizi wa Adam.

NINI KILIMTOKEA MWANAMKE WA KWANZA ALIEUMBWA TOKA MAVUMBINI MPAKA AKAUBWA WA PILI TOKA UBAVUNI ?!!

Zaidi ya kutupa habari ya kuumbwa mwanamke kwa njia mbili tofauti Biblia takatifu haijasema nini kilitokea kwa mwanamke wa kwanza (Lilith) ila Biblia inamtaja katika kitabu cha Isaya. Vitabu vya theology vya _The Alphabet of Bensira__ pamoja na _The Book of Slenda__* vinamuelezea kwa kina mwanamama huyu na hivi ndivyo ilivyokua karibu tujifunze pamoja:

Baada ya uumbaji wa Adam na Lilith kukamilika, Adam aliishi na Lilith katika Eden ya furaha kwa muda mcheche ndipo kutokuelewana kukachipua, kitabu cha theology _The Alphabet of Bensira_ kinaweka bayana kua katika kufanya tendo la ndoa Adam alimtaka Lilith alale chini "Lie beneth me woman" ila Lilith alikataa kata huku akidai kwanini yeye alale chini wakati ameumbwa sawa na Adam. Adam alikusudia kumshtaki Lilith kwa Mungu lakini kabla hajafanya hivyo Lilith alilitaja jina pekee la Mungu, jina ambalo hapana kiumbe yeyote sio mwamadam wala malaika aliruhusiwa kulitamka ila Lilith alilitamka ndipo akapata nguvu kubwa akajibadili na kua kiumbe wa kiroho. Malaika watatu walitumwa kumthibiti arudi ila alikataa na akapewa adhabu ya kupatwa upweke. Kisha ndio Mungu akaamua kumfanyia Adam mke wa pili toka ubavuni mwake na kumpa Adam kama msaidizi wake. Adam alimpenda Eva sana na ndio maana hata baada ya Eva kula tunda, Adam aliamua na yeye kula akijua ni makosa ila alikula ili asitengwe na Eva aliamua kua pamoja na Eva makosani.

NINI KILIENDELEA KWA LILITH.

Baada ya Lilith kuasi na kua kiumbe hatari wa kiroho alijiunga na Shetani na kuunda utatu mchafu kama jinsi ulivyo utatu mtakatifu (the holy trinity) yani Mungu Baba, Mungu Mwana na Roho basi Lilith, Shetani au Lucifer na Malaika msaidizi wa Lucifer kwa pamoja wakaunda utatu mchafu (the evil trinity) na hata Lucifer alipoenda kumganganya Eva kula tunda alipata wazo hili kwa Lilith ambae alikua na chuki kubwa sana kwa Adam na Eva. na hata baada ya kumfikia Eva sumu ya kutaka usawa ndio alishawishiwa kwayo Eva. Shetani au Lucifer alidanganya Eva kwa kupata ushauri wa Lilith.

YUKO WAPI LILITH

Lilith anatajwa katika tamaduni mbali mbali za Egypt, Greek, Babylon, Budha na Judism kama pepo hatari akitambulika kwa muonekano wa mwanamke mwenye mabawa katika tamaduni za Ulaya anafahamika kama The Queen of Coast. Lilith ni jina toka neno Laila katika lugha ya Kihebrania ikimanisha usiku au giza nene. Lilith ametajwa kua pepo hatari anaeua watoto wachanga wa kiume ikiwa ni malipizi kwa Adam, hii inajibu pia kwanini vifo vya watoto wengi ni watoto wachanga wa kiume ndo maana katika desturi za KiHebrania, Waisraeli hawakuwanyoa watoto chini ya miaka nane nywele, hii ilikua ikiaminika kua pepo hatari Lilith asingewadhuru akijua ni watoto wa kike maana kisasi chake ni kwa watoto wa kiume. Lilith pia anatajwa kua pepo hatari anayepinga amri ya Mungu kua mwanamume ndio kiongozi wa familia bali pepo huyu anashawishi usawa na kampeni za women empowerment zinaratibiwa na pepo huyu. Mpango wa usawa equality ni mpango wa kipepo wenye kusudio la anguko la mwanadamu ila watu hawajui, biblia inasema "watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa"

TUNAJIFUNZA NINI KUPITIA KISA HICHI ?.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa mkuu kama hizo sehem mbili zimeongelea wanawake tofauti,vipi kuhusu mwanaume...

Maana ulikosema ameumbwa lilith,ilisema "aliwaumba mwanamke na mwanamme"

Huyo mwanaume ni nani then??
 
Sasa mkuu kama hizo sehem mbili zimeongelea wanawake tofauti,vipi kuhusu mwanaume...

Maana ulikosema ameumbwa lilith,ilisema "aliwaumba mwanamke na mwanamme"

Huyo mwanaume ni nani then??
Ni Adam Mkuu...rudia kusoma upya
 
Utata na mkanganyiko kuhusu Lilith. Je alikuwa mke wa kwanza wa Adam? - JamiiForums

Jr[emoji769]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…