JE UNAMJUA LILITH ?!
Jina hili laweza kua geni masikioni pa wengi labda kwa sababu limetajwa mara moja tu katika Biblia takatifu katika kitabu cha Isaya lakini kuna mengi ya ajabu kuhusu kiumbe huya na zaidi mengi ya kujifunza.
Habari ya Adam na Eva (Hawa) inafahamika na wengi lakini kuna jambo haliko wazi karibu tujifunze pamoja, tuanze kwa kuangazia maandiko ya uumbaji wa Mungu Mwenyezi. Kitabu cha Mwanzo 1:27 kinatujuza kuhusu uumbaji " Kwa mfano wake aliwaumba mwanamume na mwanamke" na Chapter inayofuata Mwanzo 2 ni uuambaji wa Adam na Eva na wengi wanadhani uuambaji huu ndo ule wa chapter ya kwanza. Mungu alipoumba mwanamume na mwanamke chapter ya kwanza huyu mwanamke ni nani hasa ?, sio Eva ni Lilith. Najua unamshtuko, twende taratiibu tukiyasoma maandiko vema na Mungu atujalie utashi wa kujifunza maandiko.
Katika kitabu cha Mwanzo kuna uumbaji mara mbili wa mwanamke. Mwanzo 1 tumeona mungu *aliwaumba* (maana yake aliwaumba mwanaume na mwanamke kwa pamoja) aliwaumba wakiwa sawa kwa pamoja wote kutoka mavumbini wakiwa *sawa* kwa kila jambo maarifa sawa, nguvu sawa, hata urefu na muonekano sawa na hiari sawa. na ndio maana chaptei hiyo hiyo inaelekeza majukumu *sawa* waliopewa Mwanzo 1:28 "Mungu akawaambia zaeni mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha, mktawale samaki na ndege" Ni dhairi majukumu waliopewa ni *sawa* kwasababu walikua *sawa kwa kila jambo*
Baada ya hapo Biblia imekaa kinya kuhusu nini kiliendelea japo chapter za mbele tunakuja kuona tena habari ya uumbaji wa mwanamke kutoka ubavuni kwa Adam (Mwanzo 2:21) na Biblia takatifu inamuita mwanamke huyu Eva, vipi kuhusu mwanamke yule alieumbwa kwa wakati mmoja na Adam wote toka mavumbini ?! yule ni nani ?! haya.., na hata baada ya kuumbwa kwa mwanamke huyu wa pili toka ubavuni mwa Adam, kuna maneno anayatamka Adam nayo yanatupa dondoo muhimu Mwanzo 2: 23 ''Adam akasema, sasa huyu ni mifupa katika mifupa yangu na nyama kaika nyama yangu basi ataitwa mwanamke'' tazama reaction ya Adam baada yakuletewa mwanamke aliyembwa toka ubavuni mwake anaanza kwa kusepa *"sasa huyu ni ....."* maana yake ni kua ameshaishi na mwanamke alieona hakumfaa na ndo maana anasema *"sasa huyu ni ....."* Adam anaonekana kumkubali mwanamke huyu wa pili na anatoa sababu kabisa kua ametoka katika mifupa yake. JE kwanini kuna uumbaji mara mbili wa mwanamke ?. JE nini kilitokea kwa mwanamke wa kwanza ?. maswali haya nitayajibu lakini kwanza lazima kutambua kua uumbaji wa mwanamke uko mara mbili katika biblia na zifuatazo ni ushahadi wa hilo:-
> Uumbaji wa mwanamke wakwanza unafanzika Mwanzo:1 wakati uumbaji wa mwanamke wa pili unafanyika Mwanzo:2
> Mwanamke wa kwanza katajwa kuubwa kutoka mavumbini na wa pili toka ubavuni.
> Mwanamke wa kwanza anatajwa kua sawa na Adam ila wapili anatajwa kua sehemu tu ya Adam.
> Mwanamke wa kwanza anatajwa kuwa na majukumu sawa na Adam wakati mwanamke wa pili anatajwa kua msaidizi wa Adam.
NINI KILIMTOKEA MWANAMKE WA KWANZA ALIEUMBWA TOKA MAVUMBINI MPAKA AKAUBWA WA PILI TOKA UBAVUNI ?!!
Zaidi ya kutupa habari ya kuumbwa mwanamke kwa njia mbili tofauti Biblia takatifu haijasema nini kilitokea kwa mwanamke wa kwanza (Lilith) ila Biblia inamtaja katika kitabu cha Isaya. Vitabu vya theology vya _The Alphabet of Bensira__ pamoja na _The Book of Slenda__* vinamuelezea kwa kina mwanamama huyu na hivi ndivyo ilivyokua karibu tujifunze pamoja:
Baada ya uumbaji wa Adam na Lilith kukamilika, Adam aliishi na Lilith katika Eden ya furaha kwa muda mcheche ndipo kutokuelewana kukachipua, kitabu cha theology _The Alphabet of Bensira_ kinaweka bayana kua katika kufanya tendo la ndoa Adam alimtaka Lilith alale chini "Lie beneth me woman" ila Lilith alikataa kata huku akidai kwanini yeye alale chini wakati ameumbwa sawa na Adam. Adam alikusudia kumshtaki Lilith kwa Mungu lakini kabla hajafanya hivyo Lilith alilitaja jina pekee la Mungu, jina ambalo hapana kiumbe yeyote sio mwamadam wala malaika aliruhusiwa kulitamka ila Lilith alilitamka ndipo akapata nguvu kubwa akajibadili na kua kiumbe wa kiroho. Malaika watatu walitumwa kumthibiti arudi ila alikataa na akapewa adhabu ya kupatwa upweke. Kisha ndio Mungu akaamua kumfanyia Adam mke wa pili toka ubavuni mwake na kumpa Adam kama msaidizi wake. Adam alimpenda Eva sana na ndio maana hata baada ya Eva kula tunda, Adam aliamua na yeye kula akijua ni makosa ila alikula ili asitengwe na Eva aliamua kua pamoja na Eva makosani.
NINI KILIENDELEA KWA LILITH.
Baada ya Lilith kuasi na kua kiumbe hatari wa kiroho alijiunga na Shetani na kuunda utatu mchafu kama jinsi ulivyo utatu mtakatifu (the holy trinity) yani Mungu Baba, Mungu Mwana na Roho basi Lilith, Shetani au Lucifer na Malaika msaidizi wa Lucifer kwa pamoja wakaunda utatu mchafu (the evil trinity) na hata Lucifer alipoenda kumganganya Eva kula tunda alipata wazo hili kwa Lilith ambae alikua na chuki kubwa sana kwa Adam na Eva. na hata baada ya kumfikia Eva sumu ya kutaka usawa ndio alishawishiwa kwayo Eva. Shetani au Lucifer alidanganya Eva kwa kupata ushauri wa Lilith.
YUKO WAPI LILITH
Lilith anatajwa katika tamaduni mbali mbali za Egypt, Greek, Babylon, Budha na Judism kama pepo hatari akitambulika kwa muonekano wa mwanamke mwenye mabawa katika tamaduni za Ulaya anafahamika kama The Queen of Coast. Lilith ni jina toka neno Laila katika lugha ya Kihebrania ikimanisha usiku au giza nene. Lilith ametajwa kua pepo hatari anaeua watoto wachanga wa kiume ikiwa ni malipizi kwa Adam, hii inajibu pia kwanini vifo vya watoto wengi ni watoto wachanga wa kiume ndo maana katika desturi za KiHebrania, Waisraeli hawakuwanyoa watoto chini ya miaka nane nywele, hii ilikua ikiaminika kua pepo hatari Lilith asingewadhuru akijua ni watoto wa kike maana kisasi chake ni kwa watoto wa kiume. Lilith pia anatajwa kua pepo hatari anayepinga amri ya Mungu kua mwanamume ndio kiongozi wa familia bali pepo huyu anashawishi usawa na kampeni za women empowerment zinaratibiwa na pepo huyu. Mpango wa usawa equality ni mpango wa kipepo wenye kusudio la anguko la mwanadamu ila watu hawajui, biblia inasema "watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa"
TUNAJIFUNZA NINI KUPITIA KISA HICHI ?.
Sent using
Jamii Forums mobile app