Ufunuo usiosemwa: Je, Lilith ndio nyoka wa Eden? Je, ni mke wa kwanza wa Adam?

Ufunuo usiosemwa: Je, Lilith ndio nyoka wa Eden? Je, ni mke wa kwanza wa Adam?

Eve na nyoka, Ujerumani, karne ya 15
 

Attachments

  • 20221104_125939.jpg
    20221104_125939.jpg
    128.1 KB · Views: 32
Habari nje ya Biblia sio habari ya kubiblia, ni simulizi za mtaani
Ndivyo ulivyo pumbazwa na kukaririshwa!
Hapa sio kanisani,Hapa ni jukwaa huru la uchambuzi wa kina.. Hofu zako ulizopumbuzwa na kulishwa na vitabu vya dini achia huko huko Maana nazo ni stori za uongo na kusadikika tu zilizojaa Hofu wala hazina uthibitisho wowote.
 
Hamna mjadala mzito hapa ila niufinyu wa akili zenu za kibinadamu ambazo mwafikiri kwa kuzitumia hizo bila kuomba msaada wa Mungu mtayaelewa Maandiko Matakatifu bila kuyapotosha.
ninafuatilia huu uzi kwa makini sana.sijaona mahali Mshana Jr amepotosha,bali anajaribu kutufanya tu reason .tusijifunze vitu kwa kukariri au kukaririshwa.
isitoshe biblia ni mkusanyiko wa vitabu vilivyokuwa vimeandikwa asili ya lugha kiebrania, Aramaic ,kigiriki nk.
ktk kutafsi huenda haijatafsiriwa kwa ufasaha.kwa hiyo ni vizuri tukaendelea kuchimbua asili hizo ili kupata tafsiri ya kweli.
 
Myths that flow into the figure of Lilith
The demon Lilith is probably a "crasis", or a union of several previous myths. Various aspects of goddesses present in different cultures converge in her. For one thing Ishtar is often represented in a similar way and some scholars think that it is she who is represented in the Burney Relief.

In addition to Ishtar, Lamashtu, a demon with the body of a cow and tremendous claws who kidnapped children and tore them to pieces, also seems to have influenced the creation of the demon Lilith.

Lamia for the Greeks was a demon half woman and half snake who sucked the blood of children and also contributes to the birth of the myth of Lilith.

However, most aspects of Lilith derive from the Jewish tradition and from the figures of Ishtar, Iananna and Astarte. Goddesses who are often identified as a single divinity and who have the erotic charge in common with Lilith. The goddesses, or the goddess, in fact are often compared to sacred prostitution.

I would like to remind you that at the time when the myth of Lilith was spreading, Judaism was still in its infancy and since it was characterized by a strictly patriarchal society, an independent female figure, sexually free and eager to satisfy herself as she saw fit, could frighten and arouse concerns [emoji1665][emoji1665][emoji1665]
FB_IMG_1688108971267.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nje ya biblia gani.ya kikatoliki au ya kiprotestant? Maana hizo biblia walianza wakatoliki wakachambua vitabu na kuchukua vichache kati ya vingi.

hivyo kuna maandiko mengi tu ya kidini nje ya biblia yamehifafhiwa tu, wakaja waprotestant nao wakachukua bilia ya kikatoriki wakaichambua na kuchukua vitabu vichache na kuacha vingine kama 8 hivi, maana biblia ya kikatoliki ina vitabu 72 na ya kiprotestant ina vitabu 64
Pia wakaja SDA wakafanya yao wakawa na Biblia yao. Hatujakaa sawa Mashaidi wa Yehova Hawa hapa
 
Lilith anayesemekana ni mke wa kwanza wa Adam. Hatajwi popote kwenye Biblia takatifu zaidi ya kwenye kitabu cha Isaya 34 : 14, na ambapo hata hivyo kutajwa kwake hakuna mahusiano kabisa na Adam.

Kuna simulizi nyingi nje ya Biblia zinazokinzana na nyingine kushabihiana kumhusu mwanamama huyu Lakini zote zinakubaliana katika jambo moja kuwa Lilith alimwacha Adam kwakuwa hakutaka kuwa chini ya amri za mwanaume. Hakutaka kuongozwa wala kutawaliwa na mwanaume kwa utetezi kwamba, wote waliumbwa siku moja na kwa malighafi zinazofanana. Hivyo hakuna mkubwa kuliko mwingine.

Sasa asili ya Lilith ni nini!? ni wapi?

Lilith anaonekana mara nyingi kwenye Biblia ya Kiebrania na huko anajulikana kama malkia wa usiku, pepo katili la usiku lenye tamaa kubwa ya ngono... Huku kazi yake kubwa ikiwa ni kuiba watoto gizani usiku. Lilith sio jina jema popote zaidi ya kwenye imani za kipagani na kishetani.

Asili ya Lilith inatajwa sana kwenye simulizi za Wayahudi (c 700-1000). Hapa anatajwa kama mke wa kwanza wa Adam waliyeumbwa pamoja (mwanzo 1:27, kisha akafuatia mke wa pili wa Adam baada ya Lilith kuondoka (mwanzo 2:22). Hapa inasemekana Lilith alimuacha Adam kwenye bustani ya Eden na hakutaka kurudi huko na kwenda kugawa kipochi manyoya kwa malaika muasi aliyeitwa Samael. Lakini pia simulizi nyingine zinasema aliondoka na kwenda kungonoka na shetani ili kuendeleza kizazi na uzao wa shetani.

Hii inaweza kuleta uhalisia kidogo kutokana na vile satanism wanavyomchukulia Lilith, kumuamini na kumwabudu kama mungu mwanamke, mke wa baba yao shetani.

Hizi zote ni simulizi nje ya Biblia takatifu lakini kitu kimoja kilicho wazi ni kwamba kuna hicho kiumbe chenye jinsia ya kike kiitwacho Lilith ambacho hakuna popote kinatajwa kwa wema. Kuna mahali anaelezewa kama mchawi, pepo aliyengonoka na shetani kwa makusudi mazima ya kuendeleza kizazi chao kama tulivyoona hapo juu.


Ibada za kutoa kafara katika satanism

Tunaterejea tena kutazama yale mambo yaliyoacha utata na pengine hayajawahi kujadiliwa na wengi.

Tumeshajadiliana sana kuhudu Eden, Hawa, tunda la mti wa kati(mti wa ujuzi wa mema na mabaya), nyoka na Adam. Katika vyote hivi kuna mtu pia tumemjadili kwa kiasi, mtu huyu hata maandiko hayamtaji wala kumjadili sana. Mtu huyo ni Lilith, mwanamke anayesemekana kuwa mke wa kwanza wa Adam.

Jambo hili la Adam kuwa na mke aliyeitwa Lilith halitajwi kwenye misahafu yetu hii tunayoijua bali kwenye maandiko mengine lakini ya kiimani pia.

Lilith anayetajwa kwenye maandiko hayo kama mwanamke kiburi na mwenye nguvu, na ambaye pia inasemekana alizaliwa sawa na Adam, aliasi na kutengana na Adam baada ya kushindana tabia. Lilith alitaka kuwa na mamlaka makubwa kwa Adam.

Habari za Lilith zinaishia pale alipoachana na Adam, kisha Adam alirejea Eden kuanza maisha ya upweke akiwa kama mtalikiwa na tunaambiwa Lilith alikuja kugeuka kuwa kiumbe cha kuzimu.

Maisha ya upweke Eden yanamfanya Mungu kumtengenezea Adam msaidizi wa kufanana naye
ndipo Adam sasa anamshukuru Mungu kwa kusema. Sasa huyu ni nyama katika nyama zangu na mfupa katika mifupa yangu? (Wanazuoni wanatafsiri kauli hii kama kwamba mwanzoni alikuwepo mwingine ambaye hakutokana na Adam! ) Je, mtu huyo ni Lilith?

Maisha mapya ya furaha upendo na mapatano ndani ya Eden kati ya Adam na Eva/Hawa yanamvuta nyoka anayetajwa kama ibilisi akijulikana kama malaika aliyeasi mbinguni (Lilith?) Huyu ndio pekee aliyejua siri ya uumbaji (ukiacha Mungu) na siri ya tunda la mti wa kati; mti wa ujuzi wa mema na mabaya!

Kwa hakika Lilith hakupenda kabisa kuona Adam akiwa na mwanamke mwingine na hilo liko wazi hata kwa kizazi cha leo. Ule usemi wa wanawake hawapendani asili yake ni huku. Lilith kwa uwezo alionao anavaa umbo la nyoka na kumlaghai Eva/Hawa ale tunda la mti wa kati; mti wa ujuzi wa mema na mabaya. Mti ambao Adam alizuiwa kula matunda yake.

Bibie Eve/Hawa bila kujua nia ovu ya nyoka anakubali kula tunda la mti wa kati ambalo aliliona ni TAMU na linapendeza kwa macho! Kilichofuatia baada ya hapo kinajulikana wazi. Nyoka akawafitinisha Adam na mkewe Hawa kwa Mungu. Wakafumbuliwa macho yaonayo na kujiona wako uchi.

Nyoka akalaaniwa kuwa atatembea kwa tumbo. Eva akalaaniwa kuwa atazaa kwa uchungu.

Adam akalaaniwa kuwa atakula kwa jasho na wote wakafukuzwa Eden palipokuwa na kila kitu cha bure.

Lengo la Lilith la kulipa kisasi likawa limetimia na kwa mtazamo huo inawezekana kabisa Lilith ndio ibilisi!
Ila Mshana wewe unayo majini mangapi?[emoji16][emoji16]
 
Lilith ambae aligeuzwa samaki nguva ndie mwanamke wa kwanza wa Adamu alipogoma kumtii Adamu baada ya kujazwa kiburi akaenda kuolewa na shetani,ndie mwenye hizi movement zote za ufeminist,aliapa kuzisambaratisha ndoa kwa kuwapa kiburi na ukosefu wa utii kwa Wana wa eva hata Sasa ikiwemo kuleta uadui wa asili kati ya mwanaume na mwanamke
 
.
 

Attachments

  • 09576f2573ce362cd4e58c95e693b9f3.jpg
    09576f2573ce362cd4e58c95e693b9f3.jpg
    11.6 KB · Views: 13
Back
Top Bottom