Kwanza nimpongeze mtoa mada kwa hoja fikirishi
Hii hoja imepata nguvu kupitia kitabu cha mwanzo ingawa hao walioanzisha theory hii ''walitafsiri'' kwamba mwanamke wa Mwanzo sura ya kwanza ni tofauti na mwanamke wa mwanzo sura ya 2 sababu ya mistari hii miwili
Mwanzo 1
27 Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba.
Huu mwanzo 1:27 unaonyesha adam na mwanamke wameumbwa muda mmoja na ndipo wanadai Lilith aliumbwa muda mmoja na adam akaishia kumdharau na hakumheshimu adamu kabisa na wakadai mwisho wa siku akaolewa na malaika shamael wakaenda kuishi kuzimu!! Na hoja hii yao wanaipa nguvu na mstari huu hapa
Mwanzo 2: 21-
21 BWANA Mungu akamletea Adamu usingizi mzito, naye akalala; kisha akatwaa ubavu wake mmoja, akafunika nyama mahali pake,
22 na ule ubavu alioutwaa katika Adamu BWANA Mungu akaufanya mwanamke, akamleta kwa Adamu.
23 Adamu akasema, Sasa huyu ni mfupa katika mifupa yangu, na nyama katika nyama yangu, basi ataitwa mwanamke, kwa maana ametwaliwa katika mwanamume.
Kuendana na walioibua hoja hii Mstari wa 23 unaonyesha wazi Adam anamlinganisha huyu aliyetoka kwenye nyama zake KWA yule alieumbwa muda mmoja na yeye (lilith) hasa aliposema SASA HUYU!!!
Hivyo wanaamini baada ya lilith kuwa na dharau kwa adamu na kumpelekea adam kuwa mpweke ikabidi Mungu amtengeneze replacement ya lilith ambaye atatokana na nyama za adam kabisa ili amuheshimu na ndio hoja hii imejengewa hapa
Ni hayo tu
CC: mshana jr