Ufunuo usiosemwa: Je, Lilith ndio nyoka wa Eden? Je, ni mke wa kwanza wa Adam?

Hatajwi tajwi kwakuwa tayari ni nabii wa uongo
 
Hatajwi tajwi kwakuwa tayari ni nabii wa uongo

Kwa nini unapoelezea mambo kuhusu huyu bwana wenu shetani lazima uhusishe na Mambo ya Mwenyezi Mungu? Hamuwezi kusimamia mambo yenu ya kishetani bila ya kujinasibisha na Mwenyezi Mungu?

Tusaidie tuone hiyo mistari ya kitabu cha Mwanzo 1:27 na 2:22 inavyo husiana na huyu Lilith tafadhali.
 
Tatizo la ku google ndio hilo eti Mtu anasema Hakuna habari za Lilith kwenye biblia baadae anasema isipokuwa Isaya 34:14 Sasa Isaya ni kitabu kutoka kitabu kipi? Okonkwo the Great au. Simulizi tu za ajabu ajabu.
 
Tatizo la ku Google... As if you know the meaning....!!!
 
nimesoma isaya 34:14 nimeashindwa kuuelewa kwa mujibu wa maelezo yako hapo juu kwamba ametajwa kwenye kitabi hicho
Soma king James version achana na zilizochakachuliwa.... Hata ya kiswahili ina upungufu sana wa kilugha mfano english inataja leviathans kma viumbe walioko kabla ya ulimwengu kuumbwa ila biblia ya kiswahili inawaita MAMBA!

Biblia ya king james inawataja dinosaurs kma viumbe wakubwa kuliko wote ila biblia ya kiswahili inapunguza ukali wa maneno imetumia jina KIBOKO !! hivyo unapofanya tafiti kma hizi soma king james version
 
Kwanza nimpongeze mtoa mada kwa hoja fikirishi

Hii hoja imepata nguvu kupitia kitabu cha mwanzo ingawa hao walioanzisha theory hii ''walitafsiri'' kwamba mwanamke wa Mwanzo sura ya kwanza ni tofauti na mwanamke wa mwanzo sura ya 2 sababu ya mistari hii miwili

Mwanzo 1
27 Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba.

Huu mwanzo 1:27 unaonyesha adam na mwanamke wameumbwa muda mmoja na ndipo wanadai Lilith aliumbwa muda mmoja na adam akaishia kumdharau na hakumheshimu adamu kabisa na wakadai mwisho wa siku akaolewa na malaika shamael wakaenda kuishi kuzimu!! Na hoja hii yao wanaipa nguvu na mstari huu hapa

Mwanzo 2: 21-
21 BWANA Mungu akamletea Adamu usingizi mzito, naye akalala; kisha akatwaa ubavu wake mmoja, akafunika nyama mahali pake,

22 na ule ubavu alioutwaa katika Adamu BWANA Mungu akaufanya mwanamke, akamleta kwa Adamu.

23 Adamu akasema, Sasa huyu ni mfupa katika mifupa yangu, na nyama katika nyama yangu, basi ataitwa mwanamke, kwa maana ametwaliwa katika mwanamume.

Kuendana na walioibua hoja hii Mstari wa 23 unaonyesha wazi Adam anamlinganisha huyu aliyetoka kwenye nyama zake KWA yule alieumbwa muda mmoja na yeye (lilith) hasa aliposema SASA HUYU!!!

Hivyo wanaamini baada ya lilith kuwa na dharau kwa adamu na kumpelekea adam kuwa mpweke ikabidi Mungu amtengeneze replacement ya lilith ambaye atatokana na nyama za adam kabisa ili amuheshimu na ndio hoja hii imejengewa hapa

Ni hayo tu

CC: mshana jr
 
katika Quran.mwenyezi Mungu anakiri kuwa hakuwaumba majini na binadamu isipokua wamwabudu...
hivyo unapata kujua ni wajibu wa jini lolote kumuabudu MUNGU..kuna wanaofuata sheria za MUNGU na kuna walio waasi.wapo kama binadamu.kunao wema na wabaya
Mhhh
 
Tatizo la ku google ndio hilo eti Mtu anasema Hakuna habari za Lilith kwenye biblia baadae anasema isipokuwa Isaya 34:14 Sasa Isaya ni kitabu kutoka kitabu kipi? Okonkwo the Great au. Simulizi tu za ajabu ajabu.
Mkuu sitetei uwepo au kutokuwa uwepo wa lilith ila tusipende kuwa na mawazo finyu hata biblia imeitwa biblia haikutoka mbinguni ila ilikuwa na vitabu zaidi ya 400 sema kutokana na sababu mbalimbali vitabu vikapunguzwa hadi kubakia chini ya 80!! Hivyo lilith katajwa kwenye vitabu vingi tu sema vingine ndio hivyo havipo kwenye biblia hii ya sasa kwahiyo tusione vitabu vya biblia kana kwamba ndio hivihivi tokea mwanzo wa dunia ila ukivisoma vingine ambavyo vimeachwa kma historia tu utakuta hadithi za lilith zipo

Ukitaka kuongeza maarifa kubali kujifunza hata kma haukiamini unachojifunza ila just for knowledge sake..... Ssa unaposema simulizi za ajabu ajabu ilihali lilith katajwa kwenye vitabu vingine vya manabii hao hao wa kwenye biblia tukueleweje??? Au kwa mawazo yako kina isaya wameandika kitabu kimoja tu??? Jifunze kutafiti hata Paulo kaandika vitabu zaidi ya 60 ila 21 tu ndio vipo kwenye biblia ya sasa

mshana jr kaleta mada ya kufikirisha tujifunze ila sio kupinga pinga hatutoongeza maarifa..... Samahani kma nimekukwaza lakini
 
Mkuu kama wwe ni mkristo umeshawahi jiuliza Yesu aliwezaje kuzaliwa bila baba??? Si uliambiwa mimba imekuja kwa NGUVU ZA ROHO MTAKATIFU sasa kma ni hivyo kwanni usiamini hata jini anaweza kuweka mimba kwenye tumbo la mwanamke na mtoto akazaliwa !!!

Na kingine kumbuka malaika na majini wanaweza kuvaa mwili wa binadam kma unakumbuka kwenye biblia Walimtembelea Abraham wakiwa na mwili kabisa na wakala chakula baadae wakaenda kwa Lutu wakala chakula na mwishowe wakazi wa pale wakataka kuwaingilia

Ssa hujiulizi wangewezaje kuwaingilia malaika??? Kma wanaweza kuwaingilia malaika huoni viceversa pia inawezekana ??

Anyway mawazo yangu tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…