Ufunuo usiosemwa: Je, Lilith ndio nyoka wa Eden? Je, ni mke wa kwanza wa Adam?

Ufunuo usiosemwa: Je, Lilith ndio nyoka wa Eden? Je, ni mke wa kwanza wa Adam?

View attachment 692867Lilith anayesemekana ni mke wa kwanza wa Adam... Hatajwi popote kwenye Biblia takatifu zaidi ya kwenye kitabu cha Isaya 34 : 14, na ambapo hata hivyo kutajwa kwake hakuna mahusiano kabisa na Adam
Kuna simulizi nyingi nje ya Biblia zinazokinzana na nyingine kushabihiana kumhusu mwanamama huyu Lakini zote zinakubaliana katika jambo moja kuwa Lilith alimwacha Adam kwakuwa hakutaka kuwa chini ya amri za mwanaume... Hakutaka kuongozwa wala kutawaliwa na mwanaume kwa utetezi kwamba, wote waliumbwa siku moja na kwa malighafi zinazofanana.. Hivyo hakuna mkubwa kuliko mwingine....

Sasa asili ya Lilith ni nini!? Ni wapi?
Lilith anaonekana mara nyingi kwenye Biblia ya kiebrania na huko anajulikana kama malkia wa usiku, pepo katili la usiku lenye tamaa kubwa ya ngono... Huku kazi yake kubwa ikiwa ni kuiba watoto gizani usiku... Lilith sio jina jema popote zaidi ya kwenye imani za kipagani na kishetani
Asili ya Lilith inatajwa sana kwenye simulizi za wayahudi (c 700-1000)... Hapa anatajwa kama mke wa kwanza wa Adam waliyeumbwa pamoja (mwanzo 1:27, kisha akafuatia mke wa pili wa Adam baada ya Lilith kuondoka (mwanzo 2:22)... Hapa inasemekana Lilith alimuacha Adam kwenye bustani ya Eden na hakutaka kurudi huko na kwenda kugawa kipochi manyoya kwa malaika muasi aliyeitwa samael.... Lakini pia simulizi nyingine zinasema aliondoka na kwenda kungonoka na shetani ili kuendeleza kizazi na uzao wa shetani....
Hii inaweza kuleta uhalisia kidogo kutokana na vile satanism wanavyomchukulia Lilith... Kumuamini na kumwabudu kama mungu mwanamke, mke wa baba yao shetani

Hizi zote ni simulizi nje ya Biblia takatifu lakini kitu kimoja kilicho wazi ni kwamba kuna hicho kiumbe chenye jinsia ya kike kiitwacho Lilith ambacho hakuna popote kinatajwa kwq wema... Kuna mahali anaelezewa kama mchawi, pepo aliyengonoka na shetani kwa makusudi mazima ya kuendeleza kizazi chao kama tulivyoona hapo juu.... View attachment 692866
Ibada za kutoa kafara katika satanism
Nabii Wa uwongo! Katika mafungu yote uliyotoa has a LA isaya linasema kitu kingine. Ole wao wanaoongeza ama kupunguza neno LA mungu!! Jamani someni magombo mtapotoshwa
 
Nabii Wa uwongo! Katika mafungu yote uliyotoa has a LA isaya linasema kitu kingine. Ole wao wanaoongeza ama kupunguza neno LA mungu!! Jamani someni magombo mtapotoshwa
Ni hili tu au una lingine
 
Hiyo Mwanzo 1 ni basharafu ya uumbaji wa Mungu. Mwanzo 2 ni ufafafanuzi wa jinsi Mungu alivyo wa umba hao Adam na Hawa. Kiko chengine ambapo kimewachanganya na mwahitaji ufafanuzi.? Bado na kumbushia Nabii wa uongo ni yupi kati ya hawa maarufu wanaojinasibisha na Mungu mmoja wa kweli?

Mwanzo 1
27 Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba.

Huu mwanzo 1:27 unaonyesha adam na mwanamke wameumbwa muda mmoja na ndipo wanadai Lilith aliumbwa muda mmoja na adam akaishia kumdharau na hakumheshimu adamu kabisa na wakadai mwisho wa siku akaolewa na malaika shamael wakaenda kuishi kuzimu!! Na hoja hii yao wanaipa nguvu na mstari huu hapa

Mwanzo 2: 21-
21 BWANA Mungu akamletea Adamu usingizi mzito, naye akalala; kisha akatwaa ubavu wake mmoja, akafunika nyama mahali pake,

22 na ule ubavu alioutwaa katika Adamu BWANA Mungu akaufanya mwanamke, akamleta kwa Adamu.

23 Adamu akasema, Sasa huyu ni mfupa katika mifupa yangu, na nyama katika nyama yangu, basi ataitwa mwanamke, kwa maana ametwaliwa katika mwanamume.

Kuendana na walioibua hoja hii Mstari wa 23 unaonyesha wazi Adam anamlinganisha huyu aliyetoka kwenye nyama zake KWA yule alieumbwa muda mmoja na yeye (lilith) hasa aliposema SASA HUYU!!!

Hivyo wanaamini baada ya lilith kuwa na dharau kwa adamu na kumpelekea adam kuwa mpweke ikabidi Mungu amtengeneze replacement ya lilith ambaye atatokana na nyama za adam kabisa ili amuheshimu na ndio hoja hii imejengewa hapa

Ni hayo tu
 
Acha kulinganisha uwezo wa Mungu na huo wa shetani na wasaidizi wake majini maana kifo kimewashinda shetani na majini yake. Eti majini wema huwa wanasali.

Mkuu kama wwe ni mkristo umeshawahi jiuliza Yesu aliwezaje kuzaliwa bila baba??? Si uliambiwa mimba imekuja kwa NGUVU ZA ROHO MTAKATIFU sasa kma ni hivyo kwanni usiamini hata jini anaweza kuweka mimba kwenye tumbo la mwanamke na mtoto akazaliwa !!!

Na kingine kumbuka malaika na majini wanaweza kuvaa mwili wa binadam kma unakumbuka kwenye biblia Walimtembelea Abraham wakiwa na mwili kabisa na wakala chakula baadae wakaenda kwa Lutu wakala chakula na mwishowe wakazi wa pale wakataka kuwaingilia.... Ssa hujiulizi wangewezaje kuwaingilia malaika??? Kma wanaweza kuwaingilia malaika huoni viceversa pia inawezekana ??

Anyway mawazo yangu tu
 
Acheni ubabaishaji hakuna cha stori moja wala nini. Ni uongo mtupu na upotoshaji. Kwa mfano hata kwa Ibrahim/Abraham Baba wa Imani kati ya Ishmail na Isack kuna upotoshaji mkubwa linapokuja suala ni yupi mtoto wa Agano/Ahadi kati ya Mungu na Abraham.

Agano hilo lilikuwa la kiroho/kiimani na wala si la kimwili. Na lilikuwa ni jinsi gani/njia gani wanadamu wangeweza kumfikia Mungu ili kuupata uzima wa milele au kufika ahera. Hilo agano lilikuwa kupitia kwa Abraham, Sara na Isack period, hakuna mbadala wake na hatima ya hili agano ni Bwana Yesu kuukomboa ulimwengu.

Na kwa kupitia yeye Bwana Yesu ndio binadamu wataweza kuona huo uzima wa milele.

Mkuu nimesoma hoja yako ila kuna kitu hujakielewa...... Dini karibu zote duniani zilianzia mashariki ya kati hivyo basi zinatambua historia ya kwanzia bustani ya edeni... Gharika la nuhu mpaka kuja kwa Yesu ila tofauti ni kwamba kila mtu ana namna ya kuielezea mfano ukienda iran utakutana na iran mythology inayocopy na kupaste kila kitu kuhusu story ya adam na bustani ya edeni ila tofauti watakwambia shetani alimtumia chura na wanaolinda bustani ile ni samaki.....

Kwa ufupi story ni moja ila UELEWA na MAJINA ndio tofauti..... Kma umefuatilia hata vitabu vya CS Lewis kuhusu Chronicles of Narnia utagundua anaongelea story nzima ya biblia ila katika uelewa wake..... Hata greek mythology inaongelea story nzima ya uumbaji hadi kuja kwa Yesu ila katika UELEWA na MTAZAMO wa kigiriki ndio maana story zote zinafanana tofauti ni majina location na MTAZAMO basi

But story ni moja and its real brother
 
Mmmh nyabhingi hapana Yesu Kristo aliwahi kuwepo hata kihistoria tumesoma hili...... Kumbuka hata mabadiliko ya tarehe yametajwa kama AD (Anno domino ) na BC (Before Christ ) na kuna evidence na footage nyingi tu zinazomhusu

Kapotosha mpaka uomeona aibu na nafsi imekusuta imebidi tu umsahihishe hata kwa shingo upande maana huyu ni muumini na mfwasi wako/mwenzako katika upotoshaji.
 
Hiyo Mwanzo 1 ni basharafu ya uumbaji wa Mungu. Mwanzo 2 ni ufafafanuzi wa jinsi Mungu alivyo wa umba hao Adam na Hawa. Kiko chengine ambapo kimewachanganya na mwahitaji ufafanuzi.? Bado na kumbushia Nabii wa uongo ni yupi kati ya hawa maarufu wanaojinasibisha na Mungu mmoja wa kweli?
Mkuu mie nimenyoosha tu maelezo kuhusu hoja hiyo sijasema nimesupport au nmepinga so hakuna cha nabii wa uongo wala nini so jifunze kupanua ufahamu sio kukashifu mtoa mada maana wote tuko apa kujifunza na kubadilishana mitazamo

Tukirudi kwenye hoja.... Hao wanaoamini kuhusu theory hii wanakandia hasa hapo wanaposema SASA HUYU....... Embu tueleweshe na sisi wengine je hapo adamu alikuwa na maana gani

Pia aliposema ametwaliwa kutoka kwa mwanaume'' je haionyeshi kwamba yule aliumbwa ila huyu alitwaliwa......

Kwa msaada wa wengi embu tudadavulie ili tusipotoshwe

Ahsante
 
Kumbuka Adam aliletewa wanyama wote walio umbwa na Mwenyenzi Mungu awape majina na wampe kampani. Mungu akaona Adam hakuonekana kuvutiwa na hiyo kampani ya wanyama ndio akaja na wazo la kuumba kiumbe kitakacho mpaka kampani Adam. Soma mwenyewe Biblia yako uone huu ukweli.

Mkuu mie nimenyoosha tu maelezo kuhusu hoja hiyo sijasema nimesupport au nmepinga so hakuna cha nabii wa uongo wala nini so jifunze kupanua ufahamu sio kukashifu mtoa mada maana wote tuko apa kujifunza na kubadilishana mitazamo

Tukirudi kwenye hoja.... Hao wanaoamini kuhusu theory hii wanakandia hasa hapo wanaposema SASA HUYU....... Embu tueleweshe na sisi wengine je hapo adamu alikuwa na maana gani

Pia aliposema ametwaliwa kutoka kwa mwanaume'' je haionyeshi kwamba yule aliumbwa ila huyu alitwaliwa......

Kwa msaada wa wengi embu tudadavulie ili tusipotoshwe

Ahsante
 
Acha kulinganisha uwezo wa Mungu na huo wa shetani na wasaidizi wake majini maana kifo kimewashinda shetani na majini yake. Eti majini wema huwa wanasali.
Mkuu nimetoa mfano wa malaika walioenda kumtembelea lutu.... Tunaona wananchi walitaka kuwaingilia je kma wanadamu wanaweza ingilia malaika kwanni malaika washindwe kuingilia wanadamu??

Kuliko kukashifu tu jifunze kujibu hoja maana wengi wanajifunza humu kupitia hizi debate.... Wwe unasema majini na malaika kuza hawawezi mie nmetoa hoja malaika wanaweza kuvaa mwili wa binadamu je akivaa mwili wa kibinadamu hawezi kuzaa na mwanadamu?? Mbona kula walikuwa na kula na maji walikunywa hao malaika walipomtembelea abraham..... Pia kuna mmoja alipigana na yakobo kabisa sasa kwanni waweze yote ya kibinadamu alafu NGONO washindwe??

Embu tutoe tongotongo
 
Acheni ubabaishaji hakuna cha stori moja wala nini. Ni uongo mtupu na upotoshaji. Kwa mfano hata kwa Ibrahim/Abraham Baba wa Imani kati ya Ishmail na Isack kuna upotoshaji mkubwa linapokuja suala ni yupi mtoto wa Agano/Ahadi kati ya Mungu na Abraham. Agano hilo lilikuwa la kiroho/kiimani na wala si la kimwili. Na lilikuwa ni jinsi gani/njia gani wanadamu wangeweza kumfikia Mungu ili kuupata uzima wa milele au kufika ahera. Hilo agano lilikuwa kupitia kwa Abraham, Sara na Isack period, hakuna mbadala wake na hatima ya hili agano ni Bwana Yesu kuukomboa ulimwengu. Na kwa kupitia yeye Bwana Yesu ndio binadamu wataweza kuona huo uzima wa milele.
Unaijua greek mythology??? Unajua kwanni Yesu kwenye biblia alimtaja HADES?? Unapajua Tertullus?? Kwanni biblia iliitaja kma ni upotoshaji??

Unaijua iran mythology?? Vipi kuhusu Brahma kwa kihindu?? Na gilgamesh wa sumeria??

Kama hujawahi wasoma basi uisiseme upotoshaji maana story zao zinaendana na biblia kabisa sema tu wanatumia majina ya miungu yao ila events ni zile zile....kuanzia edeni mpaka gharika hadi MUNGU kushuka kuwaokoa!!! Utaelewa kma umesoma kuhusu zeus kuwaokoa wana wa cronus kutoka makucha ya Baba yao

Tanua fikra mkuu usibishe kila kitu ilihali biblia inatambua greek mythology
 
Kapotosha mpaka uomeona aibu na nafsi imekusuta imebidi tu umsahihishe hata kwa shingo upande maana huyu ni muumini na mfwasi wako/mwenzako katika upotoshaji.
Naona wewe ni mgeni wa hili jukwaa. Hapa tunaeleweshana na kushare maarifa hakuna mwenye wafuasi hapa kwakuwa hiki sio chama cha kisiasa, kikundi cha kiimani au group la wasanii.

Huku ni intelligence kunakojadiliwa yasiyojadiliwa kwingine
 
Mkuu LILITH kwa tafsiri ya kiingereza ndio wametumia SCREECH OWL kma ambavyo mmetumia Jesus ilihali jina lake halisi ni ya'shuah

Ukitaka kutafiti linganisha original text ya kiebrania sio kiingereza

Mfano biblia ya kiebrania ayubu anamuita mnyama mkubwa kuliko wote ni Dinasour ila biblia ya kiswahili inatafsiri KIBOKO!!

Biblia ya kiebrania na english inadai wanyama waliokuwepo kabla ya ulimwengu kuumbwa waliiitwa LEVIATHANS ila biblia ya kiswahili inatafsiri kma MAMBA !!!

Hivyo ukitaka tafsiri halisi uwe unatumia hebrew dictionary ndio utagundua screech owl ni LILITH

ahsante
Mkuu hapo kwenye uwepo wa wanyama kabla ya ulimwengu kuumbwa mbona ni tungo tata
 
Mimi kinachonishangaza mpk leo ni pale Adam alipoamka na kusema "Sasa" huyu ndio mke....kutumia neno sasa ina maana kuna kingine kama hicho ulikuwa nacho but hakikuwa bora so kutamka "Sasa" it means hicho kipya ni bora...

So je adam alipewa mwanamke mwingine kabla?
 
Mimi kinachonishangaza mpk leo ni pale Adam alipoamka na kusema "Sasa" huyu ndio mke....kutumia neno sasa ina maana kuna kingine kama hicho ulikuwa nacho but hakikuwa bora so kutamka "Sasa" it means hicho kipya ni bora...
So je adam alipewa mwanamke mwingine kabla???
Lilith...!?
 
Mkuu hapo kwenye uwepo wa wanyama kabla ya ulimwengu kuumbwa mbona ni tungo tata
Soma biblia ya kiingereza Job 41 nzima inamchambua huyo kiumbe...... Pia isaya 27... Zaburi 74 na 104 bila kusahau Amos 9..... Anachambuliwa kma kiumbe ambaye alikuwa hawezekaniki na kutisha kuliko wanyama wote duniani maana Ayubu anasema CHUMA KWAKE NI KAMA NYASI!!
 
Duuu chuma kwake ni kama nyasi!? [emoji102] [emoji15] [emoji15] [emoji15]
 
Dah hatari sana huyo kiumbe ukiona manabii watano wanamtaja kiumbe mmoja basi jua alikuwa ni moto wa kuotea mbali..... Soma ayubu 41 sura nzima inamchambua huyu kiumbe wa ajabu ambaye hajapata tokea mpaka sasa
Tuwekee hapa tusome na sisi
 
Back
Top Bottom