HAPANA mkuu [USER]Mshana Jr[/USER] kama tukiweka hoja kuwa Lilith ndiye Ibilisi aliyemlaghai Eva/Hawa inaleta swali la pili, Je, Adamu aliifahamu siri ya uumbwaji wake? kama hakufahamu ni vipi Lilith alifahamu?
Kama Lilith kwa vyovyote aliifahamu siri ya uumbwaji wa mwanadamu basi atakuwa ni miongoni mwa waliomuumba mwanadamu wale waliosema "Na tumfanye mtu kwa mfano wetu" hao ndio wanamjua mwanadamu je Lilith ni mmoja wao?? na kama ni mmoja wao kivipi alikuwa mke wa kwanza wa Adamu, je Adamu alioa mungu mwanamke aliyemzidi nguvu?
Binafsi kwa uelewa wangu na miulizo yangu naikataa hoja ya Lilith kuwa ndiye aliyemrubuni Eva/Hawa kwa vyovyote vile, Lilith hausiki na uovu alioufanya Eva/Hawa na Adamu wake
Labda tujiulize zaidi, je adhabu waliyopewa Adamu na Eva/Hawa ilimjumuisha na Lilith?, hasa ile ya KIFO je Lilith naye alipewa adhabu ya KIFO na kuzaa kwa UCHUNGU? kama ndiyo kwanini na je hakulijua hili kama kweli ndiye aliyemrubuni Eva/Hawa?, kivipi akubali kulipa kisasi kwa kujiadhibu na yeye?, Ibilisi alimtumoa nyoka na nyoka alipewa adhabu lakini Ibilisi yeye hakupewa adhabu yoyote hii inaonesha namna gani Ibilisi alijua namna ya kujikwepesha na adhabu ya Mungu je Lilith hilo hakulijua??
Hakuna namna naona kuwa Lilith ndiye Ibilisi
Pia kama Lilith ndiye Ibilisi kwanini alikuja kumjaribu Yesu/Nabii Issa jangwani alipokwenda kufunga? Kwani Lilith alikuwa na ajenda gani na Yesu/Nabii Issa?
Na kama ndiye je shetani ni nani?, je yule aliyemwambia Mungu amruhusu kumjaribu Ayubu ni nani!?
Sikubaliani na hoja yako ndugu yangu [USER]Mshana Jr[/USER]
VIIXCCCL GrandLodge,ARUSHA