Rev. Kishoka
JF-Expert Member
- Mar 7, 2006
- 4,526
- 1,540
Kila mara naisikia sauti ya Nyani Ngabu Julius ikisema Miafrika Ndivyo Tulivyo. Kisha kwa mbali Bob Mkandara hunguruma watu na mazingira. Kisha FMES humalizia kwa kusema viongozi wetu ni image yetu wenyewe.
Kwa wiki tatu, kauli hizo nimezithibitisha tena kuwa ni sahihi na kwa masikitiko makubwa nikakubali kuwa ndio hali halisi.
Shida ya Umeme, Uhaba wa Maji, Foleni za Magari, Takataka na Mazingira Machafu.
Hivi vitu nilivyovitaja hapo juu, ni vitu tosha kabisa kuelewa Tanzania ni Taifa la namna gani na Watanzania ni watu wa namna gani.
Jiji la Dar Es Salaam, kila siku kuna foleni ya magari inayoanzia saa 11 asubuhi. Ukitoka Kibaha, kwenda Pale Askari Monument, jiandae kutumia si chini ya masaa matatu, iwe ni alfajiri au hata jioni tena ile ya kuondoka mjini saa 2 usiku.
Sehemu nyingi za mji wa Dar Es Salaam, hazina maji ya kutosha au kuaminika kuwa kutakuwa na maji. Dawasco wamekata mabomba ya watu, wakidai kuna maji ya Mchina, halafu Dawasco hao hao hufuata raia na kuwauzia maji.
Umeme ni tatizo sugu, kila siku kuna shida ya umeme, iwe ni viwandani, maofisini na majumbani. Unajiuliza, kama Dar ndio kinara cha uzalishaji wa nchi yetu ina shida kubwa namna hii ya Umeme, ni lini tutapata maendeleo?
Takataka ni kila kona, na kila mtu anajitupia takataka anapopenda. Kila baada ya mita 500, kuna kijilima cha matakataka yaliyozagaa, iwe ni Masaki, Chang'ombe, Manzese au Kariakoo.
Sasa kilichonishangaza na kuniudhi ni ile tabia ya Watu wa Dar Es Salaam, kuonekana kuwa ama wameridhika na hali hiyo ya kukosa Umeme, Maji, Foleni na Takataka au basi wamekubali kuwa hawana jinsi yoyote ile bali kuikubali hali halisi.
Wananchi wanasema "what's a big deal about it" na Serikali nayo inasema "what's the big deal about it"!
Sasa kutokana na tabia hizi, kinachotokea Dar ni vurugu tupu-Chaos, Disorder and Disorganization.
Watu wa Dar ambao ndipo mtu ungetegemea pangekuwa ndio chimbuko la kuiwajibisha Serikali kwa kutaka Serikali itumikie wananchi, wamekaa kana kwamba wao wanamilikiwa na Serikali (very passive and submissive) na hawana sauti.
Matokeo yake, kila mtu anafanya analotaka na thubutu umuulize.
Mfano kwenye foleni za magari, kila mtu anavunja sheria na kanuni za uendeshaji magari ili kuhakikisha anawahi anakotaka kwenda. Lakini ukimuuliza haraka hii ya nini au ina manufaa gani hakupi jibu kama vile anachelewa kazini, anatumia mafuta mengi kwa umbali mdogo au kuwa ni ameudhika kutokana na matuta yaliyojazwa barabarani au udogo wa barabara.
Hali kadhalika kila mtu mwenye pesa yake anajijengea anavyotaka, bila hati, bila kufuata mipango miji tena mbaya zaidi ni Wasomi ndio wanaoongoza kwa hili.
Tabia ya kuombaomba na kutegemea imekuwa sana. Zaidi inakera kuwa watu wanaomba hongo bila woga na si ili wakusaidie upate kitu, bali wanakuambia tupatie chakula. Ukimkatalia anakubeza! Watu kutegemea kupewa pesa au misaada ni uonjwa sugu na donda dugu, na hili si la Dar pekee, nenda mpaka vijijini, watu wanasuiri mfadhili.
Nguvu ziliniishia siku moja nilipoona kwenye gazeti picha ya shule fulani na tamko la uongozi wa shule lililosema kuwa linaomba wafadhili wawajengee Waalimu choo. Sasa mfadili awe ni Mzungu au Mchungaji Kishoka, ni vipi mpaka choo kitushinde kuchimba tusubiri ufadhili?
Serikali ipo, lakini imelala usingizi mzito kabisa na kukoroma. Haijigusi wala kujiuliza kuwa huu mfukuto wa kero , mwisho wake ni mlipuko mkubwa kuliko yale mabumo ya Mbagala.
Hakuna Sauti yenye kutoa agizo wala amri. Hakuna nahodha wa kuonyesha dira au kuongoza Merikebu inavyopaswa.
Lakini Serikali yetu, jamani inajua kuzichuma, ukiangalia nyumba za wakubwa na magari wanayotumia yale ya kifahari, unajiuliza, je hawa ni watumishi wa umma au umma unawatumikia?
Sasa kwa kuwa Ufisadi ni mfumo ulioshamiri na kukubalika kirahisi na kila mtu kama ndio njia sahihi ya kujipatia mahitaji ili kuondokana na kero, basi vita ya kumkaba koo Jeetu Patel, Chenge na Rostam itakuwa ngumu mno na hata zile kauli za Sitta na Mwakyembe nilizozilaani waliposema wapiga kura wakihongwa wachukue hizo pesa na kuzila, inaonyesha kuwa Rushwa, Takrima na Hongo ni kitu cha ulazima na cha kawaida katika maisha ya Mtanzania.
Nikirudi kwenye uongozi, nilichobakiwa nacho ni masononeko. Mfumo mzima wa Uongozi na Kiutawala unabidi kubadilika na kubadilishwa, lakini kazi hiyo ni ngumu kwa kuwa ni wananchi wenyewe ndio wanapaswa kubadilika kwanza.
Kama watu wa Dar wameridhika na dhiki, kero na shida za kila siku na wala Serikali na chama tawala wala havisumbuki au kuhofia kupoteza japo kiti cha Udiwani au Ubunge, je Upinzani Tanzania una kazi gani na manufaa gani?
Waliojitahidi kuonyesha kukerwa ni wale Wanafunzi wa Kibasila na pale Kimara kwa Msuguri ambao walizuia magari yasipite, wenzao walipogongwa na magari na kupoteza maisha.
Kwa unyonge tena mkubwa nakubali, Ndivyo Tulivyo!

- Kwanza, Watanzania wengi sana ni Mafisadi kwa namna yao.
- Pili, Watanzania wengi sana wameridhika na dhiki, kero, shida na umasikini na wanaita ni hali halisi!
- Tatu, Watanzania wengi wamenogewa na kutegemea misaada na kupewa.
- Nne, Rushwa na Takrima si uhalifu tena, bali ni haki na halali ili mtu apate haki yake au atimiliziwwe mahitaji.
- Tano, Sheria, Kanuni na Taratibu zipo, tena nyingi sana, lakini kila mtu anajifanyia analotaka bila kujali matokeo ya yeye kukiuka Sheria au kanuni na wale walio na majukumu na wajibu wa kuhakikisha kuwa Sheria zinafuatwa na zinafanya kazi inavyopaswa, hawafanyi kazi zao na wanafumbia macho kwa makusudi ukiukwaji na kuvunjwa kwa sheria.
- Sita, hakuna Uongozi na Viongozi. Kila mtu na lwake na Serikali iko Likizo.