pingli-nywee
JF-Expert Member
- Sep 16, 2015
- 11,923
- 13,350
Hii ndio kazi ya mazombie ambao baadhi ya watz huwa wanawashabikia.
Jumamosi iliyopita shambulizi kali liliwaua raia wa Somalia zaidi ya 80 na waturuki wawili, jijini Mogadishu. Huku wasomalia wengine zaidi ya 120 wakijeruhiwa vibaya. Kazi ya mazombie wa alshabaab, ambao walilipua bomu ambalo lilikuwa limetegwa kwenye gari karibu na 'check point' moja kubwa jijini Mogadishu. Ningependa kusikia maoni ya baadhi ya majirani watz, wanaowashabikia alshabaab, wakiongozwa na FaizaFoxy. Kuhusu mauaji haya ya wasomalia wasiokuwa na hatia, tena waislamu, na wanafunzi 16 pia! Shambulizi lingine kama hili lilikuwa mwaka wa 2017, ambapo wasomalia 500 waliuawa na maelfu wakajeruhiwa. Al-Shabab claims deadly attack in Somalia's Mogadishu