Kama kweli wanataka tuondoke, wangetulia tu hadi mwaka ujao, Ambapo AMISOM wanatarajiwa kuondoka Somalia... Lakini sidhani kwamba wanataka tutoke manake kila wanapo fanya shambulizi, wanakumbusha dunianzima kwamba bado wapo na wana nia na uwezo kwahivyo hio inafanya AMISOM iombe muda zaidi kuwamaliza kabisa.
AMISOM ikishatoka alshabaab watakua wamekosa adui mkubwa... Kumbuka hata kabla AMISOM iende Somalia, Alshabaab walikua ndani ya Islamic Courts Union (ICU) na bado walikua wakipigana na vikosi vyengine kutoka ukoo/clans zengine za kisomali... Sahii wanajifanya kwamba eti wanapigania wasomali kwasababu kuna majeshi ya nje (AMISOM) lakini ni uongo mtupu, hayo majeshi yote ya nje yakitoka Alshabaab bado watatafuta kisababu chengine cha kuendeleza vita vya jihad.... Usisahau ndani ya Alshabaab kuna viongozi na makamanda wengi ambao wametoka nchi za kigenu kama UK,US, uarabuni... alafu mafunzo yao ya kutengeneza mabomu hufundishwa na Alqaeda wa kutoka uarabuni, hata hela na mabunduki, risasi, malighafi za kutengeneza vilipuzi vyote hutoka uarabunu...
Ukipata mda angalia hii documentary ya mji wa Kismayu ambao ulikua ulikombolewa na KDF
Sahii ukifika huko hautaona KDF hata mmoja, mji wenyewe unalindwa na wasomali wenyewe, 90% ya wakaazi wa Kismayu wanasema wanapenda vile Kismayu mji safi wenye amani kuliko miji yote mikuu kusini mwa Somalia, wanaunga mkono jitihada za serekali ya Jubaland kwa kuregesha biashara, amani, utulivu..etc... Lakini bado licha ya hayo yote, Bado alshabaab walishambulia mkahawa/hoteli.
Hii inadhihirisha vile Alshabaab wataendelea kugeuza hadithi ili wandeleze vita, kile kitu ambacho kitawafurasha tu ni Kama Somalia itakua Islamic caliphate.... Na hata Serekali kuu inayotambulika sasa ya Somalia iamue hivi leo kwamba Somalia itakua caliphate na sheria-law ndo katiba mpya ya Islamic State of Somalia, nina uhakika bado hao alshabaab wakinyimwa mamlaka ya kuongoza watatafuta sababu ya kuendelea kupigana na hio serekali hadi hao alshabaab ndo wawe hao ndo serekali pekee bila mpinzani.