Ugali kweli mtamu?

Ugali kweli mtamu?

Ahsantum Mwanakijiji. Ama hakika Ugali kweli mtama.

Nilipita tu nikakuona hapa. Nimefurahi sana na nitaungana nawe kitambo

Dr Hamza (Barubaru.
 
Mashkuura yaa jamiiya. Nimefurahi sana huu usanifu wa lugha.

Dr Hamza. (Barubaru)
 
Mashkuura yaa jamiiya. Nimefurahi sana huu usanifu wa lugha.

Dr Hamza. (Barubaru)

Mwalimu, duh nimefurahi kutambua kwamba upo. Natumaini na familia nzima wote wazima. Tunakukaribisha tena na tena. Usipotee hivyo ndugu yangu.

M.M.
 
Mwalimu, duh nimefurahi kutambua kwamba upo. Natumaini na familia nzima wote wazima. Tunakukaribisha tena na tena. Usipotee hivyo ndugu yangu.

Nashukuuru sana. Mimi ndio kwanza nimejiunga lakin insh'Allah mimi na Nasriyah ,kazi ni ile ile ya YA.

Tupo pamoja.

Dr Hamza (barubaru)
 
Sasa narudi tena,kwa usongo na kiburi
Ugali chema chafana,Njaa unasitiri
Wafaa liwa mchana,Chokapo kazi tiririri
Ugali ni kitu chema, kimenikuza nakiri

Napenda tonge mawili,yalonasana kikweli
Kwa kisu na pilipili,na tunda la stafeli
Mboga iwe tumbili,Au kuku wa da' pendaeli
Ugali ni kitu chema,Kimenikuza nakiri

Nasema tena na nena,Unafaa kwa shughuli
Hasa ukiwa kijana,mwenye nguvu na rijali
Mke hamtokosana,'Wazungu' hawatofeli
Ugali ni kitu chema,kimenikuza nakiri.

Nyie kuleni tu wali,mkiibiwa shughuli
Ugali ngoma hailali,Kibada -Gonja Betheli.
Jaribu kula ugali,uvute sigara kkali
Hutapata ile hali,wapatayo wala wali
Ugali ni kitu chema,kimenikuza nakiri

Wageuzwa wapikwa wali,Aku, kamwe mi sili
Ageuzwe perege a-ghali,huyu tamla kwa ugali
Wali harufuye kali,Hakika nasema sili
Ugali ni kitu chema,kimenikuza nakiri

Kadi tamati wa tama,kama malenga wa zama
Nimetoa nlosema,Chumbani kwangu nazama
Nahavacheni wote jama,Ugali kama Obama
Ugali ni kitu chema,Kimenikuza nakiri


Amani...
 
Wote nimewashangaa, mlosifia ugali,
Mmefanya ukang'aa, kwa sifa zisizo kweli,
Wengine mwagaagaa, kushangilia ugali,
Utamu ni wa ugali, au chake kitoweo?

Kila palipo ugali, hapakosi kitoweo,
Kumeza tonge muhali, bila chake kimezeo,
Na huo ndio ukweli, mawio hadi machweo,
Utamu ni wa ugali, au chake kitoweo?

Mnasifia ugali, pembeni mwataja mboga,
Hebu semeni ukweli, mboga ndio inanoga,
Acheni kututapeli, kutugeuza mizoga,
Utamu ni wa ugali, au chake kitoweo?

Mzee Mwanakijiji, ndugu yangu wa daima,
Ugali si kama uji, bila mboga utatema,
Bora wali wa Ujiji, usiokuwa na nyama,
Utamu ni wa ugali, au chake kitoweo?

Yametajwa matembele, mlenda pia kisamvu,
Pweza, dagaa mchele, kachumbari na mnavu,
Nyama nayo vilevile, ya mchuzi ama kavu,
Utamu ni wa ugali, au chake kitoweo?

Ugali huli mkavu, kama ubwabwa wa Kyela,
Yatakuvimba mashavu, tonge huwezi kulila,
Yataka uwe shupavu, vinginevyo ni madhila,
Utamu si wa ugali, bali chake kitoweo!

Msinione mbishi, bali ni yangu maoni,
Wala msinishawishi, niyakubali ya nani,
Maswali siyajalishi, kuweni uhuru moyoni,
Utamu si wa ugali, bali chake kitoweo!
 
Umenikumbusha makange na week end ndo inaanza...Lol

Belinda amejaribu, wa kisamvu amebaini
Nyama choma na chachandu, mchanganyiko makini
Ugali kweli mtamu, jaribu wa ‘rozigadeni’ (Rose Garden! Lol)

Ugali ule kwa ‘makange’, mpishi utamsifu
Haufanani na makande, ingawa nayo nadhifu
Ugali yake makange, kila siku utausifu

Ugali pia mtamu, hata kwa dagaa chaza
Ukitaka dagaa watamu, ni wa Kigoma au wa Mwanza
Ugali dagaa mtamu, hakika huwezi saza

SMU Umenigusa, kwa kutaja jina dagaa
Hakika umenikurupusha, ninabaki nagalagala
Sitamani chochote, si wali si Biriani

Ugali uwe wa Mtama, wa Mhogo hata wa Mahindi
Tonge lake latelezeza, ukiliwa na Mlenda
Ugali Hakika Mtamu, Siwezi kuupimia
 
Wote nimewashangaa, mlosifia ugali,
Mmefanya ukang’aa, kwa sifa zisizo kweli,
Wengine mwagaagaa, kushangilia ugali,
Utamu ni wa ugali, au chake kitoweo?

Kila palipo ugali, hapakosi kitoweo,
Kumeza tonge muhali, bila chake kimezeo,
Na huo ndio ukweli, mawio hadi machweo,
Utamu ni wa ugali, au chake kitoweo?

Mnasifia ugali, pembeni mwataja mboga,
Hebu semeni ukweli, mboga ndio inanoga,
Acheni kututapeli, kutugeuza mizoga,
Utamu ni wa ugali, au chake kitoweo?

Mzee Mwanakijiji, ndugu yangu wa daima,
Ugali si kama uji, bila mboga utatema,
Bora wali wa Ujiji, usiokuwa na nyama,
Utamu ni wa ugali, au chake kitoweo?

Yametajwa matembele, mlenda pia kisamvu,
Pweza, dagaa mchele, kachumbari na mnavu,
Nyama nayo vilevile, ya mchuzi ama kavu,
Utamu ni wa ugali, au chake kitoweo?

Ugali huli mkavu, kama ubwabwa wa Kyela,
Yatakuvimba mashavu, tonge huwezi kulila,
Yataka uwe shupavu, vinginevyo ni madhila,
Utamu si wa ugali, bali chake kitoweo!

Msinione mbishi, bali ni yangu maoni,
Wala msinishawishi, niyakubali ya nani,
Maswali siyajalishi, kuweni uhuru moyoni,
Utamu si wa ugali, bali chake kitoweo!


Maamuma nimekubali, yako mapungufu ugali
Ni kweli umeona mbali, kwa sifa iliyopata ugali
Hata mie sikubali, kwa hayayote ya ugali
Kitoweo unogesha ugali, mie pia nimekubali

Bila kitoweo chochote, huwezi kula ugali
Ili waulize wote, hata wapenzi wa wali
Weye pitia kokote, na tia hilo swali
Kitoweo unogesha ugali,mie pia nimekubali
 
Ugali kweli mtamu,
Kwa huo ninayo hamu,
Kwa mboga yenye saumu!

Ugali tangu shuleni
Jamani hadi jeshini
Nikaula na chuoni

Ugali iwe mchana
Kwenye upepo mwanana
Mwenzenu ninajichana

Ugali hata jioni,
Mezani au jikoni
Nikishatoka kazini

Ugali iwe kwa mboga
Sima kwa kweli yanoga
Kwa tembele na maboga!

Ugali kwa kurumagia
Vidole kujilambia
Na nyama inanukia!

Ugali ule kwa mchuzi
Wa samaki hata mbuzi,
Mwanawane kama kazi!

Ugali msosi wa nguvu
Haupikwi kwa wavivu,
Au walio wachovu

Ugali uwe kiporo
Alfajiri na mmajoro
Kwa mapanki ya Nyamanoro!

Ugali nimesifia
Wali ninautungia
Beti nitaupangia,

Ugali nafakamia
Matonge navingiria
Nakula nafikiria

UGALI KWELI MTAMU!!


Na. M. M. Mwanakijiji (Sauti ya Kijiji)

raha ya ugali dona
sio sembe hapana
dona ile mchana

mwili takingwa maradhi
utajenga stamili na hadhi
hakika hutamhitaji 'kadhi'
 
Nashindwa kustahimili,
Na kuusifia Ugali,
Hata upikwe na mwali,
Kamwe sijuvunii Ugali,

Ni chakula cha mifugo,
Wanakiweza wagogo,,
Nipe wali na Pongo,
Hapo Napata usongo,

Wali si lazima na nyama,
Japo umevikwa heshima,
Na kama utaupa nyama,
Basi ndoa himahima.

Vigori wetu mkoleni,
Tuwafunde kishuleni,
Nao wakiwa nyumbani,
Wali wapike jikoni,

Wali ukitiwa nazi,
Kama uchi wenye vuzi,
Hata kama mwanafunzi,
Utadinda kama tozi.
 
Wali ukitiwa nazi,
Kama uchi wenye vuzi,
Hata kama mwanafunzi,
Utadinda kama tozi.


Hodihodi Jamvini, naomba nipokeeni,
Mja wenu najirudi, mwenzenu nisameheni,
Nimechanganya maneno, niliyotoa jamvini,
Sikutumia busara, matusi kuyathamini,

Nikaanika jamvini, maneno yasoakili,
Nikasahau watoto, eti napinga ugali,
Huyu shetani gani, nimtafutie nauli,
Aende zake mwituni, akale wake ugali,

Naapa kutorudia, nikichangia mawazo,
Nitaheshimu maneno, sio kama vile mwanzo,
Niacheni nikalale, nipate tuliza mawazo,
Abbybonge ni mnyonge, msiniwekee vikwazo.
 
Ugali kweli mtamu,
Kwa huo ninayo hamu,
Kwa mboga yenye saumu!
........UGALI KWELI MTAMU!!
Na. M. M. Mwanakijiji (Sauti ya Kijiji)

Choveki ninarejea
Ilani kuwatolea
Ugali kuusifia
Uchuro mwajitakia?

Duniani kuna mambo
Ambayo yaleta shombo
Ugali kama makombo
Na hepa na lake shombo!

Mnaliita ugali
Lifananie na wali
Dona kamwe siyo wali
Pia hata kwa asili

Dona lapigiwa debe
Na kelele kebekebe
Nashangaa wenye ngebe
Tatizo lenu ni shibe!

Jina halisi ni dona
Tangia juzi na jana
Wazee pia vijana
Wajua jina ni dona!

Pia bondo ni jengine
Amekumbusha mwingine
Majina mengi mengine
Zaidi yake manne

Chakula hicho cha jela
Napata shida kukila
Sababu miye kabwela
Ndiyo maana nakila!

Dona kwangu la ugwadu
Na tena sili husudu
Lafanania kibudu
Nawaachia wa Ngudu!
 
Last edited:
Back
Top Bottom