Ugali ni chakula ambacho hakijawahi tengwa mahsusi kwenye meza kuu za Wafalme na Masultani, kinahusishwa na uduni wa kiuchumi

Ugali ni chakula ambacho hakijawahi tengwa mahsusi kwenye meza kuu za Wafalme na Masultani, kinahusishwa na uduni wa kiuchumi

Wadau wenzangu wa JF & Watanzania wote

Naandika haya nikiongozwa kwa dhamira nzuri ya kueleza ukweli bila kuwa na nia ya kuwakera baadhi yenu

Sikusudii kupotosha, kukashfu, kudharau historia yetu, au makuzi yetu, au aina fulani ya chakula, kikundi fulani
kwenye jamii yetu n.k

Nazungumza chakula maarufu duniani kinachotokana na mahindi almaarufu Ugali

Nitazungumzia kwa ufupi kuhusu Ugali Chakula ambacho;

Kwa asili hakijawahi kuwa sehemu ya vyakula vinavyote gwa kwenye meza kuu ya Wafalme au Masultani!

Hakijawahi kuwa Maalumu au mahsusi kwa ajili ya wageni

Hakijawahi kuwa Maalumu au Mahsusi hata kwa ajili ya wagonjwa au walio na njaa kali

Ni chakula kinachohusishwa na Utwana au Utumwa au hali ya umasikini

Kimekosa ufahari mbele ya jamii hasa baada ya kukitumia

Kinahusishwa na udumavu wa maendeleo ya taaluma kwa wanaokitumia kwa muda mrefu tofauti na wanaotumia vyakula vinginevyo kama mpunga, ngano, shayiri, mtama, ulezi au hata ndizi n.k

Naomba kuwasilisha

Karibuni kwa mjadala

Aksanteni

Nakala: Paschal Mayala
Hivi wafalme na masulutani ni sawa na hawa machifu wa huku kwwtu africa? vipi umehusisha ugali na tamaduni? maana kama aio utamaduni wao watakulaje ugali na vp kuhusu wasukuma na ugali ukizingatia kuwa chifu HANGAYA HATATENGEWA UGALI KWENYE MEZA YAKE
Mtazamo wako

Sent from my MI PLAY using JamiiForums mobile app
 
Waambie na pilau nalo ni chakula kwaajili ya watumwa inawekwa viungo vingi ili isiharibike haraka waendelee kula kwa muda mrefu wawapo safarimi
 
Mahindi yameletwa Africa na wakoloni wa kireno na si chakula bora ndo maana watu wananenepeana hovyo na kupata kisukari sababu ya kula ugali hasa wa mahindi, chakula gani hichi ambacho panya, dumuzi, scania, madawa shambani, mbolea za chumvi chumvi kama nyumbani .
Nashukuru nimeacha kutumia unga wa mahindi kutengeneza ugali sasa nina mwaka mmoja kamili bila kugusa, na mwili nausikia vizuri na tumbo limekuwa jepesi napata choo kingi kila siku bila ya ugali.
 
Hivyo eh!? Ugali umenikuza mimi siyo kwamba nilikuwa sili vyakula vingine la hasha! Bali nilikuwa naufurahia hata usiku udogoni nimekula mara nyingi tu na hadi hii leo sioni shida kula ugali usiku.
Udogoni maamuzi ya kukataa kula ugali usiku hayakuwa yako ila kwa vile Sasa maamuzi ni yako jaribu kutengeneza ratiba mpya ya kula ugali mchana peke yake tena siku ambayo huna majukumu ya kutumia akili kama mtihani au yanayohitaji akili kubwa.
 
wakati tunasoma shule msingi, ugali kukipikwa tulikuwa tunafurahi ubakipo, Asubuhi unakata vipande ka vya mkate unanywea na chaiii adi rahaaa

ila kiporo cha ugali hakinogi ka kiporo cha Wali - magereza .....aka wali maharagwe - mseto
Labda si ule ugali wetu wa unga wa muhogo uliochanganywa na mtama kisha ukapata na sato au sangara aliyebanikwa na mlenda pembeni [emoji16]

Sent from my CPH2185 using JamiiForums mobile app
 
Mahindi yameletwa Africa na wakoloni wa kireno na si chakula bora ndo maana watu wananenepeana hovyo na kupata kisukari sababu ya kula ugali hasa wa mahindi, chakula gani hichi ambacho panya, dumuzi, scania, madawa shambani, mbolea za chumvi chumvi hutumika sana.
Nashukuru nimeacha kutumia unga wa mahindi kutengeneza ugali sasa nina mwaka mmoja kamili bila kugusa, na mwili nausikia vizuri na tumbo limekuwa jepesi napata choo kingi kila siku bila ya ugali.
Kisukari ni mfumo wako wa maisha mbovu, ikiwa kila kukicha nguvu unatumika mwilini na unazingatia vyakula vingine vya protini na matunda, hiyo sukari inatokea wapi?

Wengine ukitupatia wali umetuonea sababu baada ya nusu saa tu tumboni hakuna kitu, yani huwa sishibi sawa na chipsi tu.

Sent from my CPH2185 using JamiiForums mobile app
 
Namshukuru Mwenyezi Mungu kwamba kwetu wazee walijaliwa uwezo wa kuamua nini cha kupika. Hivyo ikitokea kuna machaguo mawili au hata matatu tofauti vyakula hivyo vyote vilikuwepo hivyo unaweza kula vyote viwili au vitatu au ukaamua kula chakula kimoja. Hivyo hakukuwa na ulazima wa mimi kula ugali usiku zaidi ya mapenzi yangu ya kuupenda ugali.
Ná kula ugali hakusabanishi mwanafunzi ashindwe kufanya vizuri katika masomo yake na ushahidi wa hili uko wa kutosha tu Tanzania na Africa katika nchi zinazokula ugali.

Udogoni maamuzi ya kukataa kula ugali usiku hayakuwa yako ila kwa vile Sasa maamuzi ni yako jaribu kutengeneza ratiba mpya ya kula ugali mchana peke yake tena siku ambayo huna majukumu ya kutumia akili kama mtihani au yanayohitaji akili kubwa.
 
Ugali ni mtamu sana kutegemea unakula na mboga gani. Mchicha na samaki wa kukaanga, bamia na kuku wa kienyeji wa kuchoma au nyama ya kuchoma. Ugali na dagaa na mboga za majani au bamia. Ugali oyeeeee! Mie naula sana tena naupenda sili ugali for the sake ya kula ugali tu bali naufurahia sana. 😋😋😋
Washa videoooo
 
Mahindi yameletwa Africa na wakoloni wa kireno na si chakula bora ndo maana watu wananenepeana hovyo na kupata kisukari sababu ya kula ugali hasa wa mahindi, chakula gani hichi ambacho panya, dumuzi, scania, madawa shambani, mbolea za chumvi chumvi kama nyumbani .
Nashukuru nimeacha kutumia unga wa mahindi kutengeneza ugali sasa nina mwaka mmoja kamili bila kugusa, na mwili nausikia vizuri na tumbo limekuwa jepesi napata choo kingi kila siku bila ya ugali.
Mkuu unatumia ugali gani?
 
Kuna sehemu mbili tolea ufafanuzi

Kwanza tujue meza kuu unamaanisha nini, sherehe au?

Pili tujue jiografia ya hao wafalme unaowazungumzia


Vyovyote utakavyoelezea lakini hoja ya kwanza itabaki kuwa kila sehemu wana vyakula vyao vya kujikimu na vile ambavyo ni vya sherehe na mikusanyiko. Kama ni wafalme sijui masultan na wakubwa wowote wale watakula vyakula hivyo (ikiwemo ugali kwa sehemu nyingi za Africa) kulingana na muktadha (sherehe au kujikimu) bila kujali uheshimiwa wao. KITAKACHOTOFAUTIANA NI NAMNA TU YA UANDAAJI WA VYAKULA HIVYO!

Kwenye hoja ya pili katika majibu yako kumbuka... ukiangalia habari za masultan na wafalme zilitawala sana maeneo ya Asia huko hususani Arabuni na Hindi sasa angalia katika vyakula vyao (vya kujikimu, vya hamu na vya sherehe) je ugali umo!? Kama ulikuwepo tutarudi hoja namba moja na kama haumo basi haihitaji maelezo

Mwisho niseme tu kuwa UTAMU WA VYAKULA VYA HAMU NA VILE VYA SHEREHE USIKUFANYE UKALAANI NA KUHARAMISHA CHAKULA CHAKO CHA KILA SIKU CHA KUJIKIMU. Usitupe mbachao kwa msala upitao ndugu hiyo kitu ndiyo iliyokukuza mpaka leo una miguvu ya kuandika kashifa zote hizi. Tena siyo ajabu ulikuwa ukikata matonge hasa mpaka kummalizia hata mtafutaji mwenyewe (mzee wako) na yeye hakuona vibaya bali akafurahi tu kuona mwanaye amekula na kushiba na kwenda kucheza huku akiwa na furaha tele.

Paragraph hiyo hapo juu nimeongezea kwajili yako wewe uliyekuja kukashifu ugali (mahindi) tofauti na alichokuwa amekusudia mleta mada.
Haya kunywa maji sasa na urelax
 
sio huo, Ugali ulikuwa wa dona na unga wake ulitokana na mahindi fulani ivi ya njanoo (magumuu)
Huo huo ninaula kila kukicha na nikienda Hospitalini kuchukua vipimo vya afya naambiwa sukari yangu ipo ktk viwango vizuri kiafya.


Faida za dona.

1. Husaidia ubongo kutunza kumbukumbu tokana na viini cha mahindi.

Husaidia umeng'enywaji wa chakula kwa urahisi tokana na kiini kuwa na nyuzi nyuzi(finres) na maganda ya mahindi.

3. Nguvu ya mwili itokanayo na wanga ambao hauna madhara sababu ni sukari halisi wala si ya kiwandani.

4. Huongeza kinga ya mwili(heghmoglobin power) kwa kulisha seli za damu virutubisho halisi.

Shtuka achana na wahamasishaji wa mitandaoni hapa wanaodanganya watu ilihali wazazi wetu walitumia unga huo huo na wameishi miaka mingi sana kuliko hiki kizazi chetu cha ujuaji mwingi usio na faida.



Sent from my CPH2185 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom