Ugali ni chakula ambacho hakijawahi tengwa mahsusi kwenye meza kuu za Wafalme na Masultani, kinahusishwa na uduni wa kiuchumi

Kanda ya ziwa ipi? Musoma ugali wa mtama nguvu za mwili kuliko akili, mikoa ya kisukuma ugali wa mahindi nguvu za kulima ila siyo darasani, bukoba hawatumii ugali zaidi ni ndizi kama waganda hao ndo tunawaona Kuna maprofesa hivyo ugali ni nguvu za mwili ila unadumaza akili na siyo kwamba mtu asile ugali ale ugali kwa hamu na vyakula vya kuacha ubongo unafanyakazi vizuri vitumike zaidi mfano zile mboga pendwa kama dagaa zinazopendwa kuliwa na ugali zinaweza kuliwa na mkate na kushushia juice au matunda hasa usiku na mambo yakaenda vizuri sana.
 
Sijawahi kupenda ugali wa mahindi nakula kwa sababu ni hakuna option..ila soon ntaupiga chini...mahindi ni chakula cha mifugo.

#MaendeleoHayanaChama

Sent using Jamii Forums mobile app
Tumia mkate hasa ngano isiyokobolewa nichakula chenye afya hata Sara alikuwa anampikia mume wake Ibrahim mikate ya kuoka kama chakula kikuu mkate nichakula kinachotumika kwa mataifa mengi mbadala ya ugali.
 
Sanaa ya ugali inapatikana Afrika kwenye nchi za watu weusi. Nchi za Ulaya na Asia hawafaham kitu kinaitwa ugali. Baadhi ya nchi za Ulaya wanapika kitu mfano wa ugali lakini ni wa viazi, kinakuwa kati ya uji na ugali.


Ugali ukiuzoea ni msosi mzuri sana.
Hasa ugali nyama choma na safari ya baridi[emoji39][emoji39]
 
katika moja ya tafiti za kipuuzi duniani ni hiyo inayodai ugali unadumaza akili.ni tafiti ya kupuuzwa.
 
Miye nimekuelewa mtoa mada mahindi ni chakula cha mifugo.
Hata ukicheki miili yetu ni dumavu angalia wachezaji wetu na west Afrika wa kwetu kuna kitu wanakikosa ambacho ni chakula
 
Kabla ya kuandika ulitakiwa ku google kwanza, hii ni kukurupuka,ingia google andika peasant food (vyakula vya kimasikini) utagundua kuwa sausages, na pasta zipo katika listi ambapo kwako wewe uliyeposti unaweza kuwaunapoviona supermarkets unachanganyikiwa, kwa ufupi nikuwa mahindi yanalimwa africa na america sasa masultani ambao kwao mahindi hayaoti ulitakaje wale ugali,
 
Mahindi mabichi yana viruyubisho vingi
 
Ugali unadumaza akili. sio chakula bora kwa ubongo na ufahamu.

Tafuna mahindi kidogo kwa kupata wanga kiasi na sio utumie unga wa mahindi kama chakula. Tungekuwa hatuli ugali tungekuwa mbali sana!
Na wali je mkuu haudumazi akili na je hauna wanga unao athiri afya ya ubongo?
 
Ugali una wanga mwingi sana kwa hiyo unafaa kula watu wanaofanya kazi zinazohitaji matumizi ya nguvu nyingi. Sio chakula cha mtu wa kazi za wastani.
 
Mnawasaidia kupasua kuni
 
Kwa hiyo Mkuu siku hizi una puu kinyama yaani. Mzigo mzigo kwelkh
 
unga husagwa kwa mzunguko wa vyuma. Kuna wakati vyuma huwa vimelika kabisa,
Vyuma hivyi baadae huwa nu sehemu ya unga tunaokula.
Ukivila, vinaenda kuziba akili.
matokeo yake, wala ugali wnakauwaga hawana akili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…