dona zuri uliandae wewe mwenyewe maana utayosha mahidi kwa uzuri zaidi utayaanika ndipo uyasage maana hata sembe nzuri pia uiandae wewe mwenyewe maana hizi za madukani wengi wana koboa na kusaga bila hata kusha kama ilivyi kawaida kitu ambacho hakuna linalo fanyika la maana
kuna ubishani tayari whether ni muhogo au udaga, lkn unamaanisha mihogo haina faida mwilini au ugali wa muhogo?
Dunia mzima, muhogo ni stachi nö 1! stach za vyakula vyote vilivyobaki haviwezi kuifika ya muhogo!
But muhogo unapokaushwa na kutwangwa! Ni kama hindi linapokobolewa! (nimeskia tu)
Cc: MziziMkavu
Hapo ni kazi bure. Mkiacha nyama choma na rosti rosti, hata mngeendelea na sembe mngekuwa kwenye njia lishe sahihi.
MAFUTA na SUKARI katika milo yetu ndo tatizo kubwa zaidi.
Nikutahadharishe tu kuwa sio mara zote dona ni nzuri, hasa nchi zetu za kitropiki. Uki-google kidogo tu utaona kuwa zaidi ya 80% ya mahindi yaliyopo sokoni yamekuwa contaminated na fungi ambao hutoa sumu zinazoitwa mycotoxins. Sumu hizi hususani zile za aflatoxins hazina rangi wala harufu, lakini zina madhara makubwa sana hasa kusababisha saratani ya ini. Ingawa madhara ya papo kwa hapo sio mengi (mfano walipokufa watu zaidi ya 150 Kenya mwaka 2004), madhara ya muda mrefu ndio ndio makubwa na hatari.
Zaidi ya kansa ya ini, sumu hizi husababisha kudumaa (kwa watoto), na upungufu wa kinga za mwili unakopelekea mhusika kupata maambukizo ya magonjwa kama malaria, kuharisha, typhoid, mafua na mengine mara kwa mara. Kwa wamama wajawazito kunakuwa na hatari ya kujifungua watoto wenye ulemavu au kuharibika kabisa kwa mimba.
Kwa bahati mbaya, fungi humea zaidi kwenye kiini na ganda la nje la mbegu ya mahindi, hivyo kuwaweka watu wanaokula chakula kinachotokana na mahindi ambayo hayajakobolewa katika hatari kubwa zaidi. Hapo ndipo linapokuwepo tatizo kwa kula dona, kwani imethibitishwa (huko Benin, Kenya na kwingine), kuwa kuosha na kukoboa mahindi kunaweza kupunguza hadi kiasi cha 60% ya mycotoxins zilizopo...
Pamoja na faida ya kuwa na protini na fibre kwenye dona, hasara ya kuwepo kwa mycotoxins inafanya wataalamu washauri watu wale sembe zaidi na kupata protini, vitamini na fibres kwenye vyakula vingine kama maharage, kunde na mboga za majani...
cc MziziMkavu Matola miss neddy Joseph
Hakuna njia mahususi ya kuondoa hawa fungi ukiacha kuosha na kukobia ambako kunapunguza asilimia 40. Napenda sana kula dona kuliko sembe na hata ugali umechanganywa ulezi
Ni ngumu sana kwani hata ukiondoa fungi lakini sumu zake bado zinabaki. Kwa sisi watu wazima exposure ya mara moja au 2 kwa wiki ya hivi viwango vilivyopo kwenye mahindi haina effect.
Hata hivyo nimekuwa nikijiuza ongezeko la wanawake wenye ndevu na wanauma wenye nyonyo kama inachangiwa na exposure ya zearalenone ambayo ni mojawapo wa hizo sumu.
Kwa bahati mbaya pia siku hizi kiasi kikubwa cha mahindi yanayofika sokoni yanakuwa yalihifadhiwa na pesticides kama actellic super na zingine, so kuosha na kukoboa bado kunabaki njia sahihi na rahisi ya kujiepusha na haya masumu...
Ahsante Tuko! Vpi kuhusu ule unga wa ngano isiyokobolewa nao unapata watumiaji wengi kwa sasa je hakuna madhara kwenye hiyo ngano.?
Hakuna njia mahususi ya kuondoa hawa fungi ukiacha kuosha na kukobia ambako kunapunguza asilimia 40. Napenda sana kula dona kuliko sembe na hata ugali umechanganywa ulezi
Kwa bahati nzuri ngano na mpunga zina resistance kubwa kwa hawa fungi ukifananisha na mahindi na karanga (karanga ndio mbaya haswaa). Sina reference ya study iliyowahi kupata sumu kwa wingi kwenye ngano hapa Tz, ingawa kwa nchi nyingine ni common hasa kwenye ngano inayotumika kwenye vyakula vya mifugo (hiyo isiyokobolewa)...