Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
na dona je?
Safari ni Safari badilika sasa lol, naliona sembe kwa mbali tena LIVE, halafu mbona mboga hazitoi harufu?
hiyo chachandu ndio naiona, alafu huwa ni kwa ajili ya mdudu (Noah) au yumo ndani ya mboga>?
Ni Mara chache sana kutokea mycotoxins kuwa katika kiwango kikubwa kwenye mahindi Kama unavyosema ilitokea huko Kenya na vyakula vingi tu vinakuwa na viwango vya mycotoxins Kama vile wheat,rice, barley,oats and rye lakini ni kwa kiwango cha chini sana ambacho mwili wa binadamu kwa kupitia ini inaweza kuondoa hizo sumu bila shida na mycotoxins kwenye mahindi haiwezi kuondolewa kwa kukoboa, ikitokea mahindi yakawa highly contaminated na mycotoxins hayawezi kuliwa na binadamu! Cha msingi ikiwezekana mahindi yangekuwa yanapimwa kabla hayajamfikia mlaji na wakulima kufundishwa jinsi ya kuhifadhi mahindi/mazao kwani kinachosababisha mycotoxins ni mazingira yanapohifadhiwa na sababu kuu ni mbili temperature na humidity .Nikutahadharishe tu kuwa sio mara zote dona ni nzuri, hasa nchi zetu za kitropiki. Uki-google kidogo tu utaona kuwa zaidi ya 80% ya mahindi yaliyopo sokoni yamekuwa contaminated na fungi ambao hutoa sumu zinazoitwa mycotoxins. Sumu hizi hususani zile za aflatoxins hazina rangi wala harufu, lakini zina madhara makubwa sana hasa kusababisha saratani ya ini. Ingawa madhara ya papo kwa hapo sio mengi (mfano walipokufa watu zaidi ya 150 Kenya mwaka 2004), madhara ya muda mrefu ndio ndio makubwa na hatari.
Zaidi ya kansa ya ini, sumu hizi husababisha kudumaa (kwa watoto), na upungufu wa kinga za mwili unakopelekea mhusika kupata maambukizo ya magonjwa kama malaria, kuharisha, typhoid, mafua na mengine mara kwa mara. Kwa wamama wajawazito kunakuwa na hatari ya kujifungua watoto wenye ulemavu au kuharibika kabisa kwa mimba.
Kwa bahati mbaya, fungi humea zaidi kwenye kiini na ganda la nje la mbegu ya mahindi, hivyo kuwaweka watu wanaokula chakula kinachotokana na mahindi ambayo hayajakobolewa katika hatari kubwa zaidi. Hapo ndipo linapokuwepo tatizo kwa kula dona, kwani imethibitishwa (huko Benin, Kenya na kwingine), kuwa kuosha na kukoboa mahindi kunaweza kupunguza hadi kiasi cha 60% ya mycotoxins zilizopo...
Pamoja na faida ya kuwa na protini na fibre kwenye dona, hasara ya kuwepo kwa mycotoxins inafanya wataalamu washauri watu wale sembe zaidi na kupata protini, vitamini na fibres kwenye vyakula vingine kama maharage, kunde na mboga za majani...
cc MziziMkavu Matola miss neddy Joseph
Ni Mara chache sana kutokea mycotoxins kuwa katika kiwango kikubwa kwenye mahindi Kama unavyosema ilitokea huko Kenya na vyakula vingi tu vinakuwa na viwango vya mycotoxins Kama vile wheat,rice, barley,oats and rye lakini ni kwa kiwango cha chini sana ambacho mwili wa binadamu kwa kupitia ini inaweza kuondoa hizo sumu bila shida na mycotoxins kwenye mahindi haiwezi kuondolewa kwa kukoboa, ikitokea mahindi yakawa highly contaminated na mycotoxins hayawezi kuliwa na binadamu! Cha msingi ikiwezekana mahindi yangekuwa yanapimwa kabla hayajamfikia mlaji na wakulima kufundishwa jinsi ya kuhifadhi mahindi/mazao kwani kinachosababisha mycotoxins ni mazingira yanapohifadhiwa na sababu kuu ni mbili temperature na humidity .
Mkuu ingekuwa poa ukitoa references. Ninavyojua mimi high percentage ya mahindi sokoni yana contamination higher than the accepted 20ppb...
Itakuwa zoezi gumu kidogo kwasababu siwezi kufanya attachment kwa kutumia simu, ila fahamu 20ppb isn't harmful to your body na nazungumza hivyo kwasababu nilishapata kuwa exposed na fungi na kupimwa mycotoxins gani nilikuwa exposed to, najua kiwango gani ambacho kila mwanadamu anacho kwenye mwili ambacho hakina madhara mkuu, huwezi kuondoa mycotoxins kwa kukoboa kwasababu ni sumu (toxins) na Kama nilivyokwisha kusema level ya mycotoxins kwenye mahindi inatofautiana kutegemea na mazingira uliohifadhi hayo mahindi. Kumbuka mycotoxins ni secondary metabolites produced by fungi ili fungi waote wanahitaji vitu viwili temperature and humidity. We all have mycotoxins in our body but at very low level ambayo sio harmful. Hata ukila mkate, maandazi na vyakula vingine vingi tu vina kiasi kidogo cha mycotoxins ambayo your liver can get rid of it na pia nafikiri unafahamu kuna aina nyingi za mycotoxins.
Mkuu asante kwa maelezo yako, duh hii dunia ukitaka ufaidi vizuri jilimie chakula chako mwenyewe
huo ni ugali wa mtama...sijui ugali wa mhogo au wa ngano vile