Ugali wa Rowe unafaa sana kutumiwa na wanajeshi vitani, Chakula asili cha Wamanyema na Waha hapa kwetu Kigoma

Mbona unakuwa mkali utadhani weye pekee ndiye ulipita jeshini?Muda mwingine muwe mnatulia.JF ni sehemu ya kutaniana na kuburudishana.Siyo kila kitu ni kutembea kwa kapani.😝😝😝😝😝
🤣🤣🤣Mkuu wangu ni uasilishaji tu wa hoja mkuu...hamna ukali....samahani kama nimekukwaza hau!!!!
 
Umenikumbusha mbali sana,maeneo ya kumhama,kazura mimba kidahwe,Rusesa n.k huko Kigoma vijinini,nikiwa field work huko tumekula sana,unabeba ugali tuu,huko mbele utakutana na visamaki au nyama za mbuzi za kuchoma,unapiga. sema ni kama mpira/plastic hivi. unakaa saana tumboni huu ugali.ukila unashind umeshiba
 
Nilishawahi kuula huu ugali ila ni kitambo sana.
 
Ahsante sana mtaalamu wa lishe ndani ya jeshi
 
Ugali wa Rowe baada ya kusongwa unahifadhiwa kwenye majani maalum ya mgomba, unaliwa kwa mboga ama bila mboga, unaweza kusafiri nao popote kwenye begi.
Hapo kwenye kuweka chakula kwenye bag ndipo pameniacha hoi, anyway hongereni sana kwa ubunifu, je mnaonaje mkifanya maarifa ya kuwa na mboga ya muda mrefu kama ugali wake ulivyo
 
Fanyeni mpango wa kuboresha umbo lake fyatueni uwe na mwonekano wa block au circle
 
Hapo kwenye kuweka chakula kwenye bag ndipo pameniacha hoi, anyway hongereni sana kwa ubunifu, je mnaonaje mkifanya maarifa ya kuwa na mboga ya muda mrefu kama ugali wake ulivyo
Inafungwa vizuri, haichafui mazingira ya begi lako. Ugali unabebwa kwasababu maalumu, mfno: Wawindaji wa maporini wanaokwenda kuwinda wanayama maeneo ya mbali, wasafiri wa masafa marefu, wakulima, wavuvi wanaolala kwenye maji huko mbali n.k. Mboga ya muda mrefu ni dagaa zilizo kaangwa.
 
Niliukuta Burundi daah nilishindwa kula wa baridi hatari
 
Mara paap unalisha wapiganaji wanabanwa kuhara halafu muda huo adui analiamsha.

Chakula maalumu kinahitjika kwa askari aliyeko uwanja wa Vita lazima kizingatie usalama na virutubisho maalumu ambavyo Askari hatakiwi kipungukiwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…