Uganda: Aliyesomeshwa na mchumba atakiwa kurudisha Milioni 9.8 baada ya kukataa kuolewa

Uganda: Aliyesomeshwa na mchumba atakiwa kurudisha Milioni 9.8 baada ya kukataa kuolewa

Wanawake waacheni ndg zangu
Kenya wamefanya kweli
Sheria imebadilishwa, hakuna paso tena kwenye talaka
Mwanamke kama hajawekeza kitu anaondoka na sufuria lake tu
Screenshot_20230128_150151_Google.jpg
 
Hii nzuri, sio mwingine pesa yake inaisha bila kueleweka inakoishia.
Halafu mkiachana eti mgawane pasu kwa pasu.
Safi sana hiyo
Yaani mtu adai talaka apewe nyumba halafu aingize buzi huku watoto wakiadhirika
Kweli wengine masharti yetu ni simple kwenye ndoa, watoto kwanza
 
Kenya wamefanya kweli
Sheria imebadilishwa, hakuna paso tena kwenye talaka
Mwanamke kama hajawekeza kitu anaondoka na sufuria lake tu View attachment 2498473
Hata kwetu hapa Sheria Iko hivyo. Ila shida Huwa inatokea sehemu mbili tofauti.
Wanandoa kushindwa kutoa ushahidi wanamna kilammoja alivyochangia kuipata Ile Mali ya wanandoa. Pia mitazamo ya watoa maamuzi. Kuna wanaosema huduma za nyumbani zinachangia kupata Mali na Kuna wanaopinga, hapa inategemea aliyesokiliza kesi Yako.

Sent from my TECNO KG5j using JamiiForums mobile app
 
Mkuu hata bongo inawezekana. Ukimchumbia binti, chochote ulichompa katika uchumba na ambacho kilikuwa Kama moja wapo ya vitu ulivyofanya kwake kwa ahadi kuwa yeye ataolewa na wewe. Ikitokea akageuka kuwa hataki kuolewa na wewe anatakiwa avirudishe. That's is the law!
Hii ikifanyika bongo wanawake matapeli wengi watalia
 
Naungana na wewe ije huku kwetu
Ije kwenu kivipi? Nani awaletee?
Wabongo bana kila kitu mnadhani baraka kutoka Mawinguni au mnadhani wenzenu ni viumbe wa kipekee.

nyie kunawashinda kipi hapo, Si na nyie muwe mnaweka risiti kwa ajili ya kumbukumbu za malipo halafu mkizinguliwa muwe mnaenda Mahakamani kudai?

Hilo nalo mnataka Waganda wawaleteeni msaada??
 
Back
Top Bottom