Uganda kuanza kuunda magari 2018

Uganda kuanza kuunda magari 2018

Tanzania kwa zaidi ya miaka 3 sasa watu wanabishana nani atakua raisi 2015,kweli hayo maendeleo yatapatikanaje??
Vyombo vya habari ndio vinatengeneza ajenda, taarifa za uvumbuzi na teknolojia zinaandikwa mara moja halafu zinapotezewa. Labda kwa vile wajasiriamali hawawezi kutoa bahasha kama wanasiasa...
 
mkuu hii gari imetengenezwa Kenya,na ni purposely kwa rough terrain,Usishangae kampuni za kitalii hata za Tanzania wakakimbilia kununua hizi,maana bei ni cheap tofauti na landcruser,na hizi ni mpya kabisa unanunua ni sawa na 0 millage,Ksh 900,000/= ni kama Tsh Mil 18hivi kwa gari mpya na spear ni guaranteed zipo,kwanini wasiuze?
Wanasema 'function' nyingi za ziada zimeondolewa. Hii ni kazi tu hakuna cha AC wala nini sijui....
 
Watutishe bana, sisi tulishatengeneza magari kibao ya nyumbu, hamyaonagi sabasaba?! kila mwaka wale jamaa wana budget yao kwa ajili ya uvumbuzi mbalimbali, Baba Ritz ondoa shaka uko mbele kaka mkubwa, achana na waganda kwanza gugari gwenyewe gubayaaa!....
View attachment 171269

Samahani hii gari ya wapi??
 
iv nyumbu tulitengeneza au tuliasembo vitu mana kuliunda gari from scratch cdhan na nahisi ata majiran zetu ni ivo ivo tu engine wanaagiza gearbox wanaagiza piston afu wana tengeza bodi,sasa apo umetengeza gari,umeunda au umeuganisha vfaa upate gari??

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums

Mfumo wa uzalishaji wa kisasa ni mass production una assemble siyo "make". Suppliers wana zalisha parts according to design specification kampuni ya gari inassemble tu.
 
Hii nimeipenda,nzuri sana kwa adventure
Hii ya wakenya, tutaendelea kupenda sana za wenzetu, ya kwetu naona huwa inatoka siku za sabasaba tu wanaenda kuionyesha wanairudisha bandani!
 
Hii ya wakenya, tutaendelea kupenda sana za wenzetu, ya kwetu naona huwa inatoka siku za sabasaba tu wanaenda kuionyesha wanairudisha bandani!

Mkuu hizo za Kenya kwani zinatembeaga wapi... Ukiacha kwenye news, sijawahi iona barabarani. Hata huko kwao japo si mwendaji kiviile... Nyumbu mara kwa mara unaweza liona road hasa maeneo ya Kibaha
 
Kilimo Kwanza oyee!!!
NyumbuCamartec Tractor.jpg
Again kwa hisani ya google.

So kama ni magari, hata sisi yapo. Nadhani hayajawa mass-produced kwa sababu mradi haujakaa kibiashara. Manake JW ama JKT ndo wamiliki wa Nyumbu. Kwa stori nilizopewa, huwa yanatumika zaidi kubeba maji (bowsers) kwenda kwenye mafunzo yao.
 
Kwa maana ya EAC: Kenya na 'jeep', Bongo trekta na malori, Uganda tugari tudogo. Nawaza tu!

Ila huwa inakera sana watu humu (ma-GT halafu) kitu kidogo tu wanaanza ooo kulaaniwa, mara kulogwa, mara hiki mara kile. In fact, tatizo kubwa la waBongo wengi ni kutopenda kufikirisha ubongo (imagine na ndo a.k.a ya nchi) na kuishia kulaumu tu. Utalaumu hadi Masiha arudi na hutabadili kitu.

Namna pekee kubadili hali uliyonayo ni kutumia akili, maarifa na juhudi ulivyojaaliwa katika kufanya kazi. Na mtu mmoja mmoja anavyoendelea/anavyoboresha hali yake, ndipo taifa linasonga. Unachokivumbua, unachokizalisha, ukifanya kazi yako kwa weledi, wengi wananufaika kwa kuwa maendeleo/utajiri ni contageous. Yanaambukiza.

MTANZANIA, ACHA KULAUMU NA KUNUNG'UNIKA! FUNGUKA!!!!!
 
Mkuu hizo za Kenya kwani zinatembeaga wapi... Ukiacha kwenye news, sijawahi iona barabarani. Hata huko kwao japo si mwendaji kiviile... Nyumbu mara kwa mara unaweza liona road hasa maeneo ya Kibaha

hahahhaa, wenzako washaanza kuchukua pre-order wewe unazungumzia kuiona nyumbu kibaha?!!...WENZENU WANAUZA, THEY ARE DAMN SERIOUS!

tulia uone sasa, wenzako washaanza
 
Mambo kama haya, utakuta mtu analaumu wakati ilibidi kujadili kwa muktadha wa fursa tarajali ama zilizopo kwenye huo uwanda wa magari. Mfano, namna gani JW wanaweza kuingia PPP na yeyote anaedhani kutengeneza gari hapa nchini inalipa? Na hapo ndo u-GT wa wanaJF utapoonekana. Natambua wapo wengi wenye mawazo pevu sana ila, dah, wanazidiwa sana na mijamaa inayokosoa tu (yenye mawazo mgando).

AGAIN, MTANZANIA FUNGUKA!! Hatima yako ii akilini na mikononi mwako.
Kwa tulipo kimaendeleo na kijamii, fursa ni nyingi sana. Anakuja mgeni bila hata mtaji, anachapa kazi, anavuna mabilioni. Kama kawaida watu wanaanza lawama na kejeli. Ye hapungui katu!! Ndo kwaanza ananawiri kama shina la mgomba... A.T. (Wimbo: Vifuu Tundu)!!
 
hahahhaa, wenzako washaanza kuchukua pre-order wewe unazungumzia kuiona nyumbu kibaha?!!...WENZENU WANAUZA, THEY ARE DAMN SERIOUS!

tulia uone sasa, wenzako washaanza

Hiyo haimpi mtu nafasi ya kulaumu au kunung'unika. Kwani Japan ndo waliovumbua magari? Au ushaona Korea anavyokula share ya electronics ya Mjepu? Ishu ni watu wenye maslahi na hayo mambo kuchukua hatua. Hata mtu alaumu vipi, haibadilishi kwamba jirani yake amemzidi. Upo hapo?

Btw... Nina mashaka kama kweli Kenya wamefikia hadi hizo 'pre-orders'. Wanavyopenda pomp ingejazwa EAC kote, kila chombo cha habari.
 
Sisi bado tuko busy na

Mkukuta

Mkurabita

Mkukurukuta

Nyumbu

BRN

Kilimo kwanza

Sijui ipi itafuata next year

....................
..kuongeza viwango vya ufaulu ili wapate credit ya kisiasa, na kutoa tenda kwa makambuni ya nje!!
 
Kwa maana ya EAC: Kenya na 'jeep', Bongo trekta na malori, Uganda tugari tudogo. Nawaza tu!

Ila huwa inakera sana watu humu (ma-GT halafu) kitu kidogo tu wanaanza ooo kulaaniwa, mara kulogwa, mara hiki mara kile. In fact, tatizo kubwa la waBongo wengi ni kutopenda kufikirisha ubongo (imagine na ndo a.k.a ya nchi) na kuishia kulaumu tu. Utalaumu hadi Masiha arudi na hutabadili kitu.

Namna pekee kubadili hali uliyonayo ni kutumia akili, maarifa na juhudi ulivyojaaliwa katika kufanya kazi. Na mtu mmoja mmoja anavyoendelea/anavyoboresha hali yake, ndipo taifa linasonga. Unachokivumbua, unachokizalisha, ukifanya kazi yako kwa weledi, wengi wananufaika kwa kuwa maendeleo/utajiri ni contageous. Yanaambukiza.

MTANZANIA, ACHA KULAUMU NA KUNUNG'UNIKA! FUNGUKA!!!!!

Kumbe kiwanda cha nyumbu kinapewa pesa za kazi gani kila mwaka kama mnataka tusiilaumu serikali? zile pesa ni za walipa kodi wanataka kuona product siyo mnavimbisha matumbo bila output! Hakuna mtu anayesema serikali itengeneze matrekta iyagawe bure, juhudi za watu mmoja mmoja kuanzisha mashamba, viwanda na shughuli zingine kiuchumi ziko palepale na hazijaiongeja serikali pamoja na serikali kuweka mazingira magunu kwa wazawa wa tabaka la chini na la kati! Maofisini watu wanajambia viti tu, vyuo vinazalisha takataka, mashuleni wanafunzi wanapewa maksi nzuri ili wachafua viti wajipongeze ufaulu umeongezeka kwa asilimia mia nane!...SHAME.
 
Back
Top Bottom