Kwa maana ya EAC: Kenya na 'jeep', Bongo trekta na malori, Uganda tugari tudogo. Nawaza tu!
Ila huwa inakera sana watu humu (ma-GT halafu) kitu kidogo tu wanaanza ooo kulaaniwa, mara kulogwa, mara hiki mara kile. In fact, tatizo kubwa la waBongo wengi ni kutopenda kufikirisha ubongo (imagine na ndo a.k.a ya nchi) na kuishia kulaumu tu. Utalaumu hadi Masiha arudi na hutabadili kitu.
Namna pekee kubadili hali uliyonayo ni kutumia akili, maarifa na juhudi ulivyojaaliwa katika kufanya kazi. Na mtu mmoja mmoja anavyoendelea/anavyoboresha hali yake, ndipo taifa linasonga. Unachokivumbua, unachokizalisha, ukifanya kazi yako kwa weledi, wengi wananufaika kwa kuwa maendeleo/utajiri ni contageous. Yanaambukiza.
MTANZANIA, ACHA KULAUMU NA KUNUNG'UNIKA! FUNGUKA!!!!!