Filosofia ya Rorya
JF-Expert Member
- Sep 20, 2021
- 3,211
- 3,611
Nyanja: Utawala Bora/Mahusiano.
(Hili tukio siyo halisi. Majina yametajwa katika mantiki na muktadha wa urithi wa kihistoria ambao unarithishwa vizazi hata vizazi kwa njia ya uandishi)
Advocate Dr. Bishagazi Bishanga Bishaija Bashungwa LLB-Udsm, LLM-Uk, LLD-Usa, ameenda Umoja wa Mataifa kufungua madai dhidi ya Jamhuri ya Uganda ilipe fidia kwa madhara ya vita vya Kagera. Kwenye hati ya madai anauomba Umoja wa Mataifa uiamuru Jamhuri ya Uganda iulipe mkoa wa Kagera 2% ya mapato yote ghafi ya mafuta kwa miaka 50 kuanzia tarehe ya hukumu. Aidha, katika hati hiyo, ameweka mashahidi wake kwenye kesi hii ya kihistoria inayofuatiliwa na dunia nzima kama ifuatavyo:-
- H.E. Kurt Waldheim of Australia – Former UN SG.
- H.E. Edem Kodjo of Togo – Former OAU SG.
- H.E. William R. Tolbert. Jr. of Liberia – Former OAU Chair & President.
- H.E. Julius K. Nyerere of Tanzania – Former President & Commander-in-Chief.
- Hon. Edward Moringe Sokoine of Tanzania – Former Prime Minister.
- Hon. Adam Sapi Mkwawa of Tanzania – Former Speaker of the National Assembly.
- Gen. Abdallah Twalipo of Tanzania – Former CDF.
- Gen. Tumainieli Kiwelu of Tanzania – Former TPDF Chief of Staff.
- Gen. Silas Paul Mayunga of Tanzania – Former TPDF War Brigade Commander.
- Gen. John Butler Walden of Tanzania – Former TPDF War Brigade Commander.
- Gen. David Buzigo Musuguri of Tanzania – Retired CDF.
- H.E. Milton Obote of Uganda – Former President.
- H.E. Tito Okello of Uganda – Former President.
- H.E. Yusuph Lule of Uganda –Former President.
- H.E. Godfrey Binaisa of Uganda – Former President.
- Hon. Narendra M. Patel of Uganda – First Speaker of the National Assembly.
- Hon. Edward Rugumayo of Uganda – Former Legislative Council Chair.
- H.E. Jomo Kenyatta of Kenya – Former President.
- H.E. Juvenal Habyarimana of Rwanda – Former President.
- H.E. Jean-Baptiste Bagaza of Burundi – Former President.
Alipoulizwa na Mwandishi wa BK FM Radio Mujuni Muchuruza Muchwampaka iweje umeweka mashahidi ambao 97% yao hawapo duniani. Advocate Dr. Bishagazi Bishanga Bishaija Bashungwa LLB-Udsm, LLM-Uk, LLD-Usa akajibu kwamba yeye amesoma Komunyo zote na amepata Sakramenti zote hivyo hawezi kusema uongo kwa sababu kwenye hati ya kiapo alisema ataandika mashahidi walioshuhudia vita tu (siyo waliosimuliwa vita), sasa wapo au hawapo hilo silo suala lake bali la Mahakama (UN) kuamua, alijibu. Alipoulizwa anaweza kuwapeleka mashahidi hawa mbele ya Mahakama watapohitajika na kwamba haoni ni hatari kwake kama atashindwa kuwapeleka? Alijibu hivi: “wewe hujui sheria, sheria ni mbinu, sasa mimi kwenye hati ya kiapo sijasema nitawapeleka, la hasha, nimesema nitaandika mashahidi walioshuhudia vita. Kwahiyo sijajicommit kuwapeleka. Ujuwe kupeleka na kuandika vina mantiki na muktadha tofauti, tasnia ya sheria ina utaalam wake wa lugha. Umeelewa Murangira waithu?”