Carica_papaya
JF-Expert Member
- Nov 22, 2018
- 767
- 1,272
Kuna msemo wa Kiswahili usemao Rafiki/ Jirani wa kweli utamjua wakati wa shida. Tanzania imekua nchi ya kwanza kwa kuondokewa na Rais wake kipenzi aliyekuwa madarakani. DKT. JOHN JOSEPH POMBE MAGUFULI.
Ukweli ktk msiba huu nimeamini Nchi za Kenya na Uganda ndio jirani na rafiki wa kweli wa Tanzania. Uhuru Kenyata alitangaza siku 7 za Maombolezo kwa taifa la Kenya. Yoweri Museveni na yeye Alitangaza siku 14 za maombolezo kwa wananchi wa Uganda. Uhuru Kenyata pia hakusita kufika Tanzania kutupa mkono wa pole.
Televisheni za Kenya ( KTN) na Televisheni ya Uganda ( UBC) zimekua zikiripoti taarifa za msiba kwenye taarifa zake za Habari.
Leo Dodoma kwenye Maombolezo ya kitaifa Televisheni za Uganda ( UBC) na Kenya ( KTN) zipo Mubashara kurusha matukio yote.
Ila Mwenzetu Rwanda ( RTV) yupo na mambo yake anayoyajua.
Ukweli utabaki wazi Kenya na Uganda ndio Marafiki na Ndugu wa Tanzania.
Wakenya nimewaheshimu sana.