UGANDA: Serikali yatambulisha kodi mpya kwa mitandao ya kijamii ili kukomesha umbea

UGANDA: Serikali yatambulisha kodi mpya kwa mitandao ya kijamii ili kukomesha umbea

Serikali ya Tanzania inaweza kuongeza kipato kutoka kwenye mitandao ya kijamii ikiwa tu itaanzisha utaratibu wa kuwakata kodi watumiaji wote wa mitandao hiyo kila siku. Inaaminika hapa Tanzania kuna watumiaji wa mitandao ya kijamii milioni 14 kwa siku(14,000,000), hizi takwimu sio, rasmi lakini ikiwa zitafanyika takwimu rasmi idadi hii inaweza kuwa kubwa zaidi.

Ikiwa Serikali yako itaamua kuanza kukata kodi ya sh. 200 tu kwa kila mtumiaji wa mitandao ya kijamii kwa siku, TRA itakusanya sh. 84,000,000,000 (Bilioni 84) kwa mwezi, na kwa mwaka itakuwa sh. 1008,000,000,000 (Trilioni 1 na bilioni 1). Hii ni pesa mingi sana ambayo kama ikikusanywa itaweza kuisaidia Serikali katika kupata pesa za kujenga nyumba za waalimu nchi nzima. Kwa mahesabu haya ya haraka haraka, utaona kuwa hii mitandao ya kijamii ni "migodi" iliyolala.

Mfano ikiwa kila nyumba moja itajengwa kwa sh. 50,000,000 (Milioni 50) basi kwa mwaka zitajengwa nyumba 20,160 nchi nzima na baada ya miaka 5 zitakuwa zimejengwa nyumba 100,800 na hapa tutakuwa tumeondoa tatizo la nyumba sio tu kwa waalimu, bali pia kwa askari polisi, askari magareza, madaktari na wanajeshi wetu. Tena tenda hii ya ujenzi wa nyumba hizi wapewe wanajeshi kama walivyopewa ile tenda ya kujenga ukuta wa Mererani. Na uzuri ni kwamba watumiaji wa mitandao ya kijamii wanaongezeka kila mwaka na hawapungui.

Mheshimiwa Rais Magufuli, nakuomba ulichukue hili wazo na ulifanyie kazi haraka iwezekanavyo kwani huku kwenye mitandao ya kijamii kama Facebook, Twitter, Youtube, Instagram, JamiiForum, snapchat, n.k watumiaji wake, wengi wao wanapesa za kuchezea tu na hazina kazi maalumu. Kuna watu wanashinda kwenye mitandao ya kijamii siku nzima wakipost "ujinga" tu na kutukana wenzao, hivyo itakuwa bora sana kama wakianza kulipia "kodi" maalumu ya kutumia mtandao hiyo kwa siku. Sidhani kama Sh. 200 itakuwa nyingi sana kwa mtu kushindwa kulipia. Mimi binafsi nipo tayari kulipia hiyo Sh. 200 kwa siku.

Mheshimiwa Rais, nchi hii itajengwa na Watanzania wenyewe na hii ni mbinu mojawapo ya Watanzania kuchangia katika ujenzi wa nchi yao. Mitandao ya kijamii siyo chakula wala siyo maji, hivyo atakayeshindwa kulipa hiyo kodi hawezi kufa wala kudhurika kwa namna yoyote ile.

By Son of Gamba.

Nyoko we
 
pato la serikali lenye tija kwa wananchi huonhezeka pale serikali inapo anzisha miradi mipya inayotoa ajira ya moja kwa moja na isiyo ya moja kwa moja hapo kutakua na kulipana Na kodi itapatikana ila sio kuongeza mzigo wa kodi kwenye vyanzo vichache vilivyopo hapo ni sawa na kujila mkia wako mwenyewe
 
Watu wapumbavu kweli unataka ukatwe mara ngapi izo kodi? Saiv ukijiunga halotel kifurushi cha mwezi wanakupa siku 10 tu kama umetumia au hujatumia.
 
Mleta mada wakati inaletwa ile sheria ya kukata kodi kwenye muda wa maongezi ulikuwepo nchini?
 
Internet bundle mnawapa Bure?

Serikali inatoza kodi makampuni ya simu na Internet..Acheni ushamba

Kodi kwenye madini mmeshindwa, sasa mnanyonga wananchi na kuwanyima uhuru wa habari

A - Lengo la serikali ni kufanya wananchi mbumbu mbu...Taifa la watu walio gizani ili wapige ufisadi

B - Je Bloggers kama ya Google/gmail (blogspot.com) na wordpress Ni Platform za Marekani...

Mwenye blog lengo lake ni kupata adverts, je biashara zipi ziko tayari kuongeza bei ya Matangazo?

Mzunguko wa pesa umedorora Tanzania (Uchumi umeyumba) je, kuna mfanyabiashara yuko tayari kutumia pesa kwa hasara?

Bei ya Tangazo (hata unayoyaona JF) ni kipato kidogo sana

Purchasing capacity Ya watanzania imepungua sana,,,,(vyuma vimekaza) biashara iko wapi?

-Wakulima walizuiwa kuuza mazao (bei zikafa)
-Wakulima wananunua pembejeo ghali (Mbolea bei ghali sana, dawa ghali)
- Sukari imepaa bei, sasa ni 2800 kwa kilo
- Umeme ghali, Luku mmeongeza bei
 
200×14,000,000×30×12=1,008,000,000,000( Trillion 1 na billion 8) kwa mwaka.
Mwenzio anashangaa kuona kama kuna m-Tanzania anayeweza kulipa 72,000/= kwa mwaka, wewe budogo unafikri kakosea kukokoto?!!
 
Hata mkusanye fedha kiasi gani hakuna mabadiliko yoyote yakatayofanyika zaidi ya Pesa Hizo kuchukulia na lumumba ziwasaidie kwenye chaguzi Zao

Ova
 
pato la serikali lenye tija kwa wananchi huonhezeka pale serikali inapo anzisha miradi mipya inayotoa ajira ya moja kwa moja na isiyo ya moja kwa moja hapo kutakua na kulipana Na kodi itapatikana ila sio kuongeza mzigo wa kodi kwenye vyanzo vichache vilivyopo hapo ni sawa na kujila mkia wako mwenyewe
ushauri wa kijinga tu mpuuzeni, kuna wilaya tisa hazina ma- dc lbd unasaka u-dc.
 
Hawataweza tutahamia za kimataifa kama bbc, na mitandao ya kibongo itapigwa doro
 
NAUNGA MKONO 100% Mimi hakuna kinachonipiita mitandao yote ya jamii yaani instagram, jamii forum, fb, wasap nk natumia tsh 5000/=kila siku.
 
Bwege nini wewe kwenye vocha tukatwe then na wapi sijui tukatwe... Ukome msiiiiieeeew ukitaka mwambie akukate peke yako.... Kwa pesa gani za kukatana kodi ovyo kichwa chako
 
Bangi na baridi haiwezi muacha mtumiaji salam,lazima stimu zipande mapemaaa,na kesho lazima uamke nazo.
 
Wewe unategemea asikilize ushauri wako??

Yeye mwenyewe alitamka hadharani kuwa Urais ni wake na yeye mwenyewe ndiye aliyekwenda kuchukua fomu ya Urais kwa hiyo yeye ni Rais anayejiamini, kwa hiyo hategemei ushauri toka kwa mtu yeyote!

Akaendelea kueleza kuwa mtu akimshauri ndiyo anaharibu kabisa, kwa kuwa yeye hapokei ushauri toka kwa mtu yeyote yule!
Ushauri mzuri na wenye manufaa kwa Taifa huwa anausikiliza sana tu. Ushauri ambao huwa hausikilizi ni ule unaoendana na mambo ya "uteuzi" wa viongozi, hapo ndipo alipokataa kushauriwa. Tatizo lenu ninyi hamkuelewa alikuwa anazungumzia nini.

Alikataa kushauriwa katika kuteua viongozi sababu kuna wengine walikuwa wanamshauri kuteua watu wao na ndugu zao kwa manufaa yao binafsi.
 
Bwege nini wewe kwenye vocha tukatwe then na wapi sijui tukatwe... Ukome msiiiiieeeew ukitaka mwambie akukate peke yako.... Kwa pesa gani za kukatana kodi ovyo kichwa chako
Kama watu hawana pesa, wanapata wapi pesa za kuingia kwenye mitandao na wanachofanya kwenye hiyo mitandao ni kutukana tu wenzao kama wewe ulivyofanya sasa hivi kwa kuniita "bwege"? Mimi nafikiri atakaye shindwa kulipa hiyo kodi, kama ikianzishwa basi na asiingie kwenye mitandao.
 
Pale ambapo sirikali haina hela..
Siku zote mapato ya Serikali yanatokana na "kodi" za wananchi. Hili pia ni wazo la kuongeza mapato hayo ya Serikali. Ni kweli ndiyo Serikali haina hela, na hela huwa hazijai.
 
Back
Top Bottom