UGANDA: Serikali yatambulisha kodi mpya kwa mitandao ya kijamii ili kukomesha umbea

UGANDA: Serikali yatambulisha kodi mpya kwa mitandao ya kijamii ili kukomesha umbea

Siku zote mapato ya Serikali yanatokana na "kodi" za wananchi. Hili pia ni wazo la kuongeza mapato hayo ya Serikali. Ni kweli ndiyo Serikali haina hela, na hela huwa hazijai.
Unaongeza mapato kwa kunyonga walipa kodi?
 
pato la serikali lenye tija kwa wananchi huonhezeka pale serikali inapo anzisha miradi mipya inayotoa ajira ya moja kwa moja na isiyo ya moja kwa moja hapo kutakua na kulipana Na kodi itapatikana ila sio kuongeza mzigo wa kodi kwenye vyanzo vichache vilivyopo hapo ni sawa na kujila mkia wako mwenyewe
Hiyo ni kweli ndiyo, lakini pale ambapo Serikali inapoweza kupata chanzo kingine cha kukusanya kodi mimi sioni ni kwanini isifanye hivyo. Isitoshe sasa hivi viwanda vingi vinaanzishwa hivyo Wananchi wengi zaidi watapata ajira na watumiaji wa mitandao ya kijamii pia wataongezeka na mapato pia yataongezeka, kama Serikali itaanzisha kodi hii maalumu ya watumiaji wa mitandao ya kijamii.
 
Unaongeza mapato kwa kunyonga walipa kodi?
Ukweli ni kwamba mitandao mingi ya kijamii ni bure na haina malipo yoyote kwa wanaoitumia mfano ni Facebook, Instagram na Youtube. Mitandao mingi ya simu inatoa huduma hizi bure kabisa. Sasa imefika mahali Serikali ianze kujikusanyia mapato ya ziada kutoka kwa watumiaji wa hii mitandao.
 
Ingefungwa Kabisa turudi Enzi za Mwalimu.
Kuifunga hii mitandao siyo jambo la busara sababu kwa wengine ni ajira zao za kudumu. Jambo la busara ni kuanzisha kodi nyingine ya ziada ambayo kwa hiyo Serikali itajipatia mapato zaidi. Ikiwekwa kodi ya sh. 200 kwa siku kwa mtumiaji ni sawa na Trilioni 1 kwa mwaka. Hilo ni ongezeko kubwa sana kwenye bajeti yetu.
 
Mkuu huyo mleta uzi kaisoma fb imetokea Uganda maana kwao wanakusudia kuianzisha
Uganda wanajadili sasa hivi namna ya kuanzisha "kodi" hii maalumu ya watumiaji wa mitandao. Siyo vibaya na sisi tukiianzisha mapema kwani kuiga kitu kizuri siyo jambo baya, jambo baya ni kuiga mambo ya kipuuzi yasiyokuwa na faida.

Jana nilikuwa nasikiliza BBC nao wanasema kuna nchi za Ulaya zinataka kuanzisha utaratibu wa watu kuanza kulipia pesa zaidi pale wanapotumia mitandao ya kijamii, hivyo sisi tukianzisha utaratibu huu hatutakuwa tofauti na wengine ambao pia wameona kuna haja ya kufanya kitu kama hichi.
 
Hivi wewe ujinga wako unadhani kodi inakatwa kwa kila pesa unayoiona mkononi mwa mtu?? Basi wajikate kodi kwa pesa yao ilitunzwa BOT, hujui kila vocha inakatwa kodi 18%?? Au hiyo mitandao ya kijamii inafanya kazi nje ya hizo vocha tunazoweka??
Unapofanya kazi mwisho wa mwezi unakatwa kodi kwenye mshahara wako. Na bado ukienda dukani unakatwa kodi ya VAT kwa kila bidhaa unayonunua. Hivyo basi hata kama tunalipia VAT kwenye kila Vocha ya simu tunayonunua, pia ni sawa tu ikiwekwa "kodi" maalumu ya sh. 200 kwa siku, kwa kila mtu atakayeingia kwenye mitandao ya kijamii.

Mitandao ya kijamii siyo chakula, maji, au dawa; kwamba mtu akikosa anaweza kufa, yeye atakayeshindwa kulipia hiyo kodi basi na asiingie kwenye hiyo mitandao. Mbona pombe na sigara zinaongezwa kodi kila mwaka na watu hawaachi kutumia? Ndiyo kwanza watumiaji wa pombe na sigara wanaongezeka kila kukicha.
 
Tayari tunakatwa hiyo kodi tunaponunua vifurushi vya internet
Hiyo inayokatwa kwenye vifurishi vya Internet ni VAT, mimi nazungumzia tozo maalumu ya kutumia mitandao ya kijamii ambayo napendekeza iwe sh. 200 kwa siku kwa mtumiaji. Ni kama vile mfanyakazi anayepokea mshahara mwisho wa mwezi anakatwa kodi kwenye mshahara wake lakini akienda dukani kununua bidhaa pia anakatwa kodi kwenye kila kitu anachonunua.

Jambo hili la kuanzisha tozo maalumu ya watumiaji wa mitandao ya kijamii sasa hivi linajadiliwa hata kwenye nchi za Ulaya ambapo wameona kuna mapato zaidi na wanaonufaika ni waanzishaji wa hii mitandao. Sasa ili Serikali zinufaike zaidi, zinatakiwa kuanzisha tozo hizi maalumu. Kwa hapa "Afrika", Uganda tayari wameanza kujadili mfumo huu ambao ulipendekezwa na Rais Museveni.
 
Sijajua bado chanzo cha mawazo yako ni nini lakini naona chuki na ulimbukeni kwa sababu:-

1) Ukinunua simu (handset) unalipa kodi

2) Ukinunua vocha, data, airtime iwe cash au kwa mpesa unalipa kodi

3) Utumiaji wa mitandao una mazuri na mabaya, sasa huwezi kuja na sheria za hovyo kama unavyopendekeza kisa tu kuna wachache wenye kuhalifu (abuse).

Na wewe hapa unahalifu (abuse) matumizi sahihi ya neno/dhana '"KODI". Ndio maana TRA imekuwa ikituhumiwa "kutumika" kubambika na kufilisi watu kwa jina la "KODI"!

Nikupe mfano, Mimi sinywi pombe lakini kutaka baa au groceries zote zifungwe au zitozwe kodi kubwa (kukomoa) itabidi kwanza niwe nina hitilafu kwenye ubongo ili kuweza kufikiri au kupendekeza hivyo.

Siha ya ubongo ulioandaliwa vema ni pamoja na uwezo wa kustahimili tusiyoyapenda, na kutumia akili, hekima na maarifa kutatua shida au maudhi tunayokabiliana nayo kila siku. C'mon be civil!!!
 
Hiyo inayokatwa kwenye vifurishi vya Internet ni VAT, mimi nazungumzia tozo maalumu ya kutumia mitandao ya kijamii ambayo napendekeza iwe sh. 200 kwa siku kwa mtumiaji. Ni kama vile mfanyakazi anayepokea mshahara mwisho wa mwezi anakatwa kodi kwenye mshahara wake lakini akienda dukani kununua bidhaa pia anakatwa kodi kwenye kila kitu anachonunua.

Jambo hili la kuanzisha tozo maalumu ya watumiaji wa mitandao ya kijamii sasa hivi linajadiliwa hata kwenye nchi za Ulaya ambapo wameona kuna mapato zaidi na wanaonufaika ni waanzishaji wa hii mitandao. Sasa ili Serikali zinufaike zaidi, zinatakiwa kuanzisha tozo hizi maalumu. Kwa hapa "Afrika", Uganda tayari wameanza kujadili mfumo huu ambao ulipendekezwa na Rais Museveni.
Hivi huwa ni kwanini mambo mabaya ya uonevu huwa mnaiga Ulaya na Marekani lakini ikija kwenye huduma za afya, elimu, haki za binadam, maendeleo, ulinzi mnakana kuiga?

Sawa igeni kutoza kodi lakini pia igeni na kutoa huduma.

Hivi ni kwa nini lakini mnajifungia kwenye vifungo vya umaskini, ujinga, maradhi kwa miaka yote hii????
 
yaani serekali ijichanganye hapo ndo itakapo juu sisi ni vichaa tutaanza tumia WiFi familia ya watu 10 tutalipa miambili hapo bado majirani nao wanataka kutumia bado tutaiibia mpk ikome
 
Hivi huwa ni kwanini mambo mabaya ya uonevu huwa mnaiga Ulaya na Marekani lakini ikija kwenye huduma za afya, elimu, haki za binadam, maendeleo, ulinzi mnakana kuiga?

Sawa igeni kutoza kodi lakini pia igeni na kutoa huduma.

Hivi ni kwa nini lakini mnajifungia kwenye vifungo vya umaskini, ujinga, maradhi kwa miaka yote hii????
Hayo mambo yanaboreshwa vipi kama Serikali haina pesa za kutosha?? Ulaya huduma hizo ni bora sababu wao wanapesa za kutosha kufanya hayo yote kwa ubora.

Ili na sisi tufikie huko walikofikia wenzetu, basi tujifunze kulipia kodi. Ndiyo maana napendekeza ianzishwe tozo maalumu ya watumiaji wote wa mitandao ya kijamii ili Serikali ipate mapato zaidi ili iweze kutoa huduma kwa Raia wake. Bila pesa, Serikali haiwezi kutoa huduma bora.
 
Gamba, mtafika lini huko (ni miaka 60 sasa)? Siku moja kifaranga wa kuku alimwona mama ngo'mbe akimnyonyesha ndama wake, akamgeukia mamake na kumwuliza mama yake je aweza kumnyonyesha? Mama kuku akajibu kuwa ndio anaweza, na kuwa siku moja naye atamnyonyesha huyo kifaranga wake. Leo hii huyo kifaranga ni mtetea mkubwa na bado anasubiri ahadi itimizwe!

Nchi nyingi kama Ghana, Korea Kusini, Singapore, Malaysia au hata Kenya tulianza nazo, kama rika moja wakati tunapata uhuru 1961.....leo hii zimetupita mbali kimaendeleo....lakini bado hizi hadithi za siku moja tutafika zinaendelezwa, je ni mpaka lini???? TUZIKATAE.

Hilo pakacha mnaloliita Hazina linavuja, na kwa mwendo huu hali ya pakacha ni mbaya kuliko jana. Sasa ni lini mtakuwa na huo uwezo ikiwa mmeongeza ufisadi kwenye ujinga, maradhi na umaskini mliokuwa nao??

Mimi nasema kubana uhuru wa mawazo na habari ambavyo sio chanzo cha matatizo tuliyonayo ni uonevu. Kutoza kodi kandamizi pia sio sehemu wala havitaisaidia kutatua matatizo yaliyopo. Inahitajika tupate viongozi wenye maono ya maendeleo (HATUJAWAHI KUWA NAO) ili watusaidie tutoke hapa. Mnaumiza wananchi tuuu lakini hamna nia wala uwezo wa kuwasaidia, huo ndio ukweli na ndio maana nakupinga.
 
Ukweli ni kwamba mitandao mingi ya kijamii ni bure na haina malipo yoyote kwa wanaoitumia mfano ni Facebook, Instagram na Youtube. Mitandao mingi ya simu inatoa huduma hizi bure kabisa. Sasa imefika mahali Serikali ianze kujikusanyia mapato ya ziada kutoka kwa watumiaji wa hii mitandao.
Ndo kuwanyonga walipa kodi huko. Mzigo wa kodi tayari ni mkubwa mno.
 
Back
Top Bottom