Unaongeza mapato kwa kunyonga walipa kodi?Siku zote mapato ya Serikali yanatokana na "kodi" za wananchi. Hili pia ni wazo la kuongeza mapato hayo ya Serikali. Ni kweli ndiyo Serikali haina hela, na hela huwa hazijai.
Hiyo ni kweli ndiyo, lakini pale ambapo Serikali inapoweza kupata chanzo kingine cha kukusanya kodi mimi sioni ni kwanini isifanye hivyo. Isitoshe sasa hivi viwanda vingi vinaanzishwa hivyo Wananchi wengi zaidi watapata ajira na watumiaji wa mitandao ya kijamii pia wataongezeka na mapato pia yataongezeka, kama Serikali itaanzisha kodi hii maalumu ya watumiaji wa mitandao ya kijamii.pato la serikali lenye tija kwa wananchi huonhezeka pale serikali inapo anzisha miradi mipya inayotoa ajira ya moja kwa moja na isiyo ya moja kwa moja hapo kutakua na kulipana Na kodi itapatikana ila sio kuongeza mzigo wa kodi kwenye vyanzo vichache vilivyopo hapo ni sawa na kujila mkia wako mwenyewe
Ukweli ni kwamba mitandao mingi ya kijamii ni bure na haina malipo yoyote kwa wanaoitumia mfano ni Facebook, Instagram na Youtube. Mitandao mingi ya simu inatoa huduma hizi bure kabisa. Sasa imefika mahali Serikali ianze kujikusanyia mapato ya ziada kutoka kwa watumiaji wa hii mitandao.Unaongeza mapato kwa kunyonga walipa kodi?
Kuifunga hii mitandao siyo jambo la busara sababu kwa wengine ni ajira zao za kudumu. Jambo la busara ni kuanzisha kodi nyingine ya ziada ambayo kwa hiyo Serikali itajipatia mapato zaidi. Ikiwekwa kodi ya sh. 200 kwa siku kwa mtumiaji ni sawa na Trilioni 1 kwa mwaka. Hilo ni ongezeko kubwa sana kwenye bajeti yetu.Ingefungwa Kabisa turudi Enzi za Mwalimu.
Uganda wanajadili sasa hivi namna ya kuanzisha "kodi" hii maalumu ya watumiaji wa mitandao. Siyo vibaya na sisi tukiianzisha mapema kwani kuiga kitu kizuri siyo jambo baya, jambo baya ni kuiga mambo ya kipuuzi yasiyokuwa na faida.Mkuu huyo mleta uzi kaisoma fb imetokea Uganda maana kwao wanakusudia kuianzisha
Unapofanya kazi mwisho wa mwezi unakatwa kodi kwenye mshahara wako. Na bado ukienda dukani unakatwa kodi ya VAT kwa kila bidhaa unayonunua. Hivyo basi hata kama tunalipia VAT kwenye kila Vocha ya simu tunayonunua, pia ni sawa tu ikiwekwa "kodi" maalumu ya sh. 200 kwa siku, kwa kila mtu atakayeingia kwenye mitandao ya kijamii.Hivi wewe ujinga wako unadhani kodi inakatwa kwa kila pesa unayoiona mkononi mwa mtu?? Basi wajikate kodi kwa pesa yao ilitunzwa BOT, hujui kila vocha inakatwa kodi 18%?? Au hiyo mitandao ya kijamii inafanya kazi nje ya hizo vocha tunazoweka??
Hiyo inayokatwa kwenye vifurishi vya Internet ni VAT, mimi nazungumzia tozo maalumu ya kutumia mitandao ya kijamii ambayo napendekeza iwe sh. 200 kwa siku kwa mtumiaji. Ni kama vile mfanyakazi anayepokea mshahara mwisho wa mwezi anakatwa kodi kwenye mshahara wake lakini akienda dukani kununua bidhaa pia anakatwa kodi kwenye kila kitu anachonunua.Tayari tunakatwa hiyo kodi tunaponunua vifurushi vya internet
Hivi huwa ni kwanini mambo mabaya ya uonevu huwa mnaiga Ulaya na Marekani lakini ikija kwenye huduma za afya, elimu, haki za binadam, maendeleo, ulinzi mnakana kuiga?Hiyo inayokatwa kwenye vifurishi vya Internet ni VAT, mimi nazungumzia tozo maalumu ya kutumia mitandao ya kijamii ambayo napendekeza iwe sh. 200 kwa siku kwa mtumiaji. Ni kama vile mfanyakazi anayepokea mshahara mwisho wa mwezi anakatwa kodi kwenye mshahara wake lakini akienda dukani kununua bidhaa pia anakatwa kodi kwenye kila kitu anachonunua.
Jambo hili la kuanzisha tozo maalumu ya watumiaji wa mitandao ya kijamii sasa hivi linajadiliwa hata kwenye nchi za Ulaya ambapo wameona kuna mapato zaidi na wanaonufaika ni waanzishaji wa hii mitandao. Sasa ili Serikali zinufaike zaidi, zinatakiwa kuanzisha tozo hizi maalumu. Kwa hapa "Afrika", Uganda tayari wameanza kujadili mfumo huu ambao ulipendekezwa na Rais Museveni.
Hayo mambo yanaboreshwa vipi kama Serikali haina pesa za kutosha?? Ulaya huduma hizo ni bora sababu wao wanapesa za kutosha kufanya hayo yote kwa ubora.Hivi huwa ni kwanini mambo mabaya ya uonevu huwa mnaiga Ulaya na Marekani lakini ikija kwenye huduma za afya, elimu, haki za binadam, maendeleo, ulinzi mnakana kuiga?
Sawa igeni kutoza kodi lakini pia igeni na kutoa huduma.
Hivi ni kwa nini lakini mnajifungia kwenye vifungo vya umaskini, ujinga, maradhi kwa miaka yote hii????
Gamba, mtafika lini huko (ni miaka 60 sasa)? Siku moja kifaranga wa kuku alimwona mama ngo'mbe akimnyonyesha ndama wake, akamgeukia mamake na kumwuliza mama yake je aweza kumnyonyesha? Mama kuku akajibu kuwa ndio anaweza, na kuwa siku moja naye atamnyonyesha huyo kifaranga wake. Leo hii huyo kifaranga ni mtetea mkubwa na bado anasubiri ahadi itimizwe!Hayo mambo yanaboreshwa vipi kama Serikali haina pesa za kutosha?? Ulaya huduma hizo ni bora sababu wao wanapesa za kutosha kufanya hayo yote kwa ubora.
Ili na sisi tufikie huko walikofikia wenzetu, basi tujifunze kulipia kodi. Ndiyo maana napendekeza ianzishwe tozo maalumu ya watumiaji wote wa mitandao ya kijamii ili Serikali ipate mapato zaidi ili iweze kutoa huduma kwa Raia wake. Bila pesa, Serikali haiwezi kutoa huduma bora.
Ndo kuwanyonga walipa kodi huko. Mzigo wa kodi tayari ni mkubwa mno.Ukweli ni kwamba mitandao mingi ya kijamii ni bure na haina malipo yoyote kwa wanaoitumia mfano ni Facebook, Instagram na Youtube. Mitandao mingi ya simu inatoa huduma hizi bure kabisa. Sasa imefika mahali Serikali ianze kujikusanyia mapato ya ziada kutoka kwa watumiaji wa hii mitandao.
Uliota nini mkuuJiwe lazima ataiga hii
jiwe anatamani nchi yetu iwe Kama Uganda au RwandaUliota nini mkuu