Uganda: Waangalizi wa Uchaguzi waitaka Serikali kutochapisha Karatasi za Kura

Uganda: Waangalizi wa Uchaguzi waitaka Serikali kutochapisha Karatasi za Kura

Shadida Salum

Journalist at JamiiForums
Joined
Sep 11, 2020
Posts
69
Reaction score
105
Waangalizi wa Uchaguzi wa ndani wameitaka Tume ya Uchaguzi Nchini humo (EC) kupinga shinikizo lolote la kuchapa karatasi za kura za Uchaguzi ujao wa 2021 ndani ya nchi kwa kuhofia kuharibu mchakato wa Upigaji kura.

Waangalizi wanaamini kuwa uhuru wa Tume hiyo unajaribiwa, hivyo wamesema kuwa EC inaweza kuaminiwa na Wapiga Kura na Wagombea kama tu karatasi za Kura zitachapwa nje ya Nchi hiyo.

Mamlaka ya Ugavi na Uuzaji wa Mali za Umma (PPDA) Octoba 26 iliiagiza Tume kutathmini tena ofa za Makampuni ya ndani na nje yaliyoomba kupewa Zabuni ya kuchapa karatasi za Kura 187 kwa ajili ya Uchaguzi mkuu wa 2021.

Aidha Tume hiyo ilikuwa kwenye mchakato wa kusaini Mkataba na makampuni matano ya Nje kwa ajili ya kuchapa Karatasi za Kura, lakini PPDA ikakazia pingamizi lililowekwa na Taasisi ya Uchapaji na Ufungashaji ya Uganda (UPPA).

Katika Pingamizi hilo, Taasisi ya UPPA ililalamika kuondolewa bila haki katika hatua za awali kabla ya kutathmini uwezo wao wa kuchapa karatasi za Kura.

Sarah Bireete, Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Utawala wa Katiba (CCG) amesema kuwa kuchapa Karatasi za kura nje ya Nchi itapelekea kuwepo kwa Uchaguzi Huru na wa Haki.

Kwa upande wa Tume ya Uchaguzi EC kupitia Mwenyekiti wake, Jaji Simon Byabakama alisema kuwa agizo la kutathmini tena Ofa za kuchapa karatasi za Kura itaathiri kifungu cha Katiba kinachotaka uchaguzi ufanywe ndani ya siku 30 za kwanza za mwisho wa siku 122 za muhula. Ambapo hii itaangukia katikati ya January 9 na Februari 10,2021.
 
Back
Top Bottom