Uganda: Waliokufa kwa maandamano waongezeka, Jeshi latoa tamko

Uganda: Waliokufa kwa maandamano waongezeka, Jeshi latoa tamko

joto la jiwe

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2017
Posts
26,117
Reaction score
46,617
Idadi ya watu waliopoteza maisha katika maandamano na vurugu nchini Uganda wanaodai Robert Kyagulanyi maarufu kama Bobi Wine aachiwe huru imeongezeka na kufikia 37, kwa mujibu wa taarifa ya Jeshi la Polisi nchini humo.

Polisi walimkamata Bobi Wine Jumatano wiki hii katika mji wa Luuka akituhumiwa kuvunja kanuni za kudhibiti maambukizi ya virusi vya corona kwa kufanya mkutano wa hadhara.

Baadhi ya vijana wamechoma matairi na kufanya maandamano katika maeneo ya Jiji la Kampala na maeneo mengine wakidai mwanamuziki huyo aliyegeuka kuwa mwanasiasa aachiwe huru.

Polisi inawatuhumu waandamanaji kwa kufanya vurugu, kuharibu mali kama magari na kuwarushia mawe maafisa wa polisi.

Msemaji wa Polisi katika Jiji la Kampala, Patrick Onyango amesema kama hali itaendelea hivi huenda vifo vikaongezeka. Amesema watu 350 wanashikiliwa kutokana na vurugu hizo.

Sky News wamemkariri msemaji wa Jeshi la Uganda, Brigadier Flavia Byekwaso akieleza kuwa jeshi liliingilia kati kwa sababu hali ilikuwa ‘kama vita’ ambayo polisi peke yao wasingeweza kuimudu.
===

MY TAKE: Kama Uganda wameanza kuchinjana mapema, Vipi jirani mwenye historia ya kuchinjana ambaye hata kabla ya kampeni kuanza watu wameshaanza kupigwa risasi, itakuaje hapo 2022?
 
Zanzibar sio Tanzania
Tunaomba ushahidi tafadhali, kumbuka mlisema mlisema Hospital za Tanzania zimejaa wagonjwa wa Corona, na kwamba watanzania walikua wanakufa kwa wingi barabarani bila ushahidi wowote ule. Tunaomba ushahidi tafadhali.
 
Tunaomba ushahidi tafadhali, kumbuka mlisema mlisema Hospital za Tanzania zimejaa wagonjwa wa Corona, na kwamba watanzania walikua wanakufa kwa wingi barabarani bila ushahidi wowote ule. Tunaomba ushahidi tafadhali.
Walete hao waganda 37 hapa, nataka ushahidi hala wala sio upuuzi tu
 
Back
Top Bottom