Uganda yaondoa mashtaka ya uhaini dhidi ya kiongozi wa upinzani

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Serikali ya Uganda imeifuta kesi ya uhaini dhidi ya kiongozi wa chama cha upinzani Kizza Besigye, ambaye alikuwa akipambana kumuondoa madarakani rais Yoweri Museveni ambaye ametawala kwa kipindi cha miaka 35.

Besigye, amegombea nafasi ya urais mara nne na alikamatwa na kushtakiwa kwa makosa ya uhaini mwaka 2016 kwa kujitangaza mwenyewe kuwa ni rais baada ya huo mwaka wa uchaguzi mkuu.

Kiongozi huyo wa upinzani aliwahi kuwa daktari wa kumtibu rais Museveni , Besigye alikosana na rais mwaka 1999 baada ya kukielezea chama tawala kuwa chama kisichoaminika,wanaoangalia fursa na wasioheshimu demokrasia.

Chanzo: BBC Swahili

 
Watawala wa kiafrika ukiingia anga zao wakahisi utaweza kupata ushawishi na kupewa madaraka wako tayari kukufanyia lolote hata kukuua wanakuua
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…